Kuna liliemfika hili

Kuna liliemfika hili

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Nafasi za kazi zimetangazwa UN. Watu wamepeleka maimbi ukiwa mmoja wapo. Kwa hamaki baada yavwuki mbili unapata email uwende kwenye usaili.

Ni mchujo mkali lakini umefanikiwa kuibuka kidedea. Unapata kazi na procedure za uajiri zinaanza, unatakiwa ufanyiwe medical check up. Majibu yanatokana kwa mshangao unagundua wewe ni HIV+.

Moyo umepata mfadhaiko ukijua ndiyo Mwisho wa maisha yako, baada ya shahada ya uzamili kumbe ki-affair ulichokuwa nacho kwa muda mfupi kilikuwa majanga.

Umewapelekea majibu wamekujibu hakuna wasiwasi mradi utuletee barua ya HIV specialist anaeratibu matibabu yako.

Umefanikiwa kupata clinic nzuri na tiba ni nzuri. Ndani ya miezi sita viral load ni undictectable na una endelea na dawa. Daktari anakwambia immune system ni nzuri sana na sasa hivi imeanza kuimarika.

Tangia upate majibu hata hamu ya sex iliishia pale. Ni mwaka wa pili huu huja date, daktari anakukumbusha kuwa sexual health ni muhimu kwa afya nzima. Una tumia dawa vizuri na daktari anaridhishwa na maendeleo yako kwani unajua ufanyalo. Unamuona daktari Mara moja kwa mwaka na HIV specialist nurse baada ya miezi sita kwa ushauri tu baadavya kupima damu.

Umeshahakikishiwa kuwa kwa hali yako huwezi kumuambukiza mtu lakini ni muhimu kutumia condom ili usipate magonjwa mengine ya zinaa

Uko kwenye mkutano unekutana na mtu ambae unaona kabisa mnaendeana, uko nervous kuchukua mahusiano kwa sehemu ya pili lakini ilynasmua kuendelea na mna sex kwa condom.

Sasa imefikia hatua mmeaminiana lakini unashindwa kumuwleza status yako, hii ni siri yako kubwa hata ndugu zako hawafahamu. Unawasiwasi kuwa ukimueleza atakuacha na pia atatoa siri yako.

Siku moja katika maongezi anakuhadithia jinsi alivyofanta kazi na wagonjwa wa HIV na mmoja alimficha partner wake na varangati likianzia hapo.

Hujui uanzie wapi na hapa ndiyo unaomba uonbewe hii HIV iishe mwilini kwako.
 
Kwani UN,hawa-ajiri H.I.V +??
 
Umewapelekea majibu wamekujibu hakuna wasiwasi mradi utuletee barua ya HIV specialist anaeratibu matibabu..
Nimefanya kazi na UN agencies mbili tofauti. Hakunaga haya mambo ya kuombana HIV status. Ingekuwa balaa!
 
Back
Top Bottom