Kuna kubwa la kujifunza kupitia huyu rafiki yangu...

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
770
2,408
Miaka 4 iliyopita nilikutana na huyu jamaa. Ilikuwa ndani ya basi la kutoka kwetu huko nyanda za juu kusini magharibi ambako kwa wakati ule nilienda kumzika babu yangu mzaa mama (Rest in peace Grandpa). Tulipofika Morogoro, abiria wengine walishuka na kupanda wapya ili tuimalize safari ya kuingia DSM. Miongoni mwa abiria walioshuka alikuwemo yule niliyekuwa nimekaa nae siti moja kutoka huko tulipoanzia safari. Miongoni mwa waliopanda ni huyu jamaa ambae alikuja kukaa nilipokuwa mimi. Alipofika, alinisalimia nikajibu na safari ikaanza. Ilipita kama nusu saa tukiwa kimya tu kila mtu akiwa na mambo yake ndipo tulipoingia rasmi kwenye mazungumzo.

Na kitu kilichofungua mazungumzo yetu ilikuwa ni movie moja ya Marehemu King majuto (Rest easy Legend). Tulijikuta tumecheka tu na hapohapo zikaanza story mbili tatu hadi tukaingia kwenye maongezi marefu. Nilikuwa 23yrs by then huku jamaa kwa makadirio akiwa kama miaka 31 kwa kipindi hicho. Hii age difference kuna mda ilimpa mamlaka ya kutawala mazungumzo yetu huku akianza kunipa ushauri mbalimbali kuhusu maisha n.k. To be honest, sikuwa interested sana na mazungumzo yake, kwasababu nilikua naona ananibania kusinzia/Kupumzika kwa kunipigisha story.

Mi nishachoka na safari yeye damu bado inachemka. Sikujali sana nikaona sio busara kumpuuza as long as anapiga story za maana. Safari ikaendelea. Jamaa ni mwenyejii wa Dar ila Moro anafanya mishe zake za kujitafutia ridhiki ila makazi yake ya kudumu kama mke na familia ni DSM.

FAST FORWARD:
Baada ya siku 3, jamaa alinipigia simu kuwa kama sitojali nionane nae nimsaidie issue aliyokuwa anaifanya halafu atanilipa ikikamilika. Baada ya kujiridhisha kuwa kitu kinachofanyika ni legal na eneo la tukio ni ofisini tena ofisi ya kuheshimika, nikawa sina shaka nikasema nipe nusu saa nitakuwa nishafika. Kufika pale akanipa vitendea kazi akanielekeza tukaanza kazi...Kazi yenyewe ilikuwa ni kutype documents ambazo zilikuwa handwritten pamoja na kujaza taarifa kwenye baadhi ya fomu.

Nadhani watu ambao huwa wanafanya data recording hapa watakuwa wamenielewa kuhusu ujazaji wa fomu kwenye computer. Document zilikuwa nyingi ni kama vile jamaa alikuwa anafanya research. sasa bora kujaza fomu, ila kutype ndio ilikuwa shughuli maana pages ni nyingi. Sijui hata kwanini hawakuzitype moja kwa moja wakati wanaandika kwa mkono. Kiufupi ilikuwa kazi ngumu na tupo wawili tunaifanya. Tulipiga ile kazi siku 3 mi natoka nyumbani asubuhi narudi jioni. Uzuri gharama za nauli na chakula alikuwa anazisimamia basi mi nikawa napiga kazi kwa moyo wote na sifa ili hata akija kunilipa ujira wangu aone kuwa nimestahili..Tulipambana kazi ikaisha.

Baada ya kumaliza kazi nikitarajia malipo sasa na mimi nikavimbe, jamaa akaanza kuniletea lugha ambazo sizielewi..Akanambia nimpe kama wiki moja arudi morogoro akikamilisha kuwasilisha ile kazi atanitafuta na kunilipa wala nisijali. Nikamuuliza utanilipa shingapi, akasema 150k (Inaonekana ile project ilikuwa inamlipa sana). Akili ya kwetu Temeke ikanambia hapa umepigwa..Jamaa akanipa 10k nauli siku hiyo halafu akanambia niamini mdogo wangu. Sio siri nilichukia sana, kwanini hukunambia mapema mi najitahidi najua napata hela as soon as kazi ikiisha kumbe ninakopwa.

Kingine nikawa najilaumu kwanini nimefanya kazi kabla ya makubaliano japo moyoni nilikuwa naiona ile 150k ni kubwa..Kiukweli sikuitarajia kabisaa. Laiti kama angeniulize anipe shingapi ningejiropokea 50k tu hahaha. Hapohapo nikawa nafurahi kuwa amejikaanga kwa kutaja bei mwenyewe halafu pia najilaumu kuwa nimepigwa maana pesa ni ahadi tu. Basi, kwakuwa jamaa alinitreat fair zile siku tatu nikaona sio kesi acha nimuamni tu maana kama kupigwa nishapigwa. Nikachukua 10k yangu nikarudi home huku niko very disappointed. Hii siku ndiyo nilijifunza kuwa usiipangie hela kabla hujaishika.

Ilipita wiki, zikawa mbili, tatu hadi nne hakuna simu wala muamala. Namimi siku zote hizo nilikuwa sijamtafuta jamaa maana niliamini kuwa nimepigwa. Nikaanza kusahau. Siku moja jioni wakati vuguvugu la bwana Tundu kupigwa risasi likiwa limepamba moto na wakati huo akiwa Nairobi kwa matibabu, simu ikaita kucheki ni namba ya jamaa na tayari namba yake nilikuwaga nishaedit jina nimemsave BORNTOWN hahahah maana nilijua amenipiga kimasihara.Nikapokea akasema Fohadi nilitaka nihakikishe kama hii namba ipo hewani. Muda wowote nitakutumia hela. Siku hiyo nilihakikisha simu haizimi charge hahaha ila nilisubiri sana hadi usiku hakuna muamala. Nikaanza tena kuumia kwa kitu ambacho nilishaga sahau. Kesho yake ilikuwa ijumaa mapema tu asubuhi naona muamala unasoma 155k kutoka kwa jamaa. Baada ya dakika moja akanipigia akaniomba radhi kwa kunicheleweshea...Hapo mi namwambia wala huna ulichokosea mkuu. Huna baya kaka hahaha. Story yangu na jamaa ikaishia hapo...Hatukuwahi kuwa na mawasiliano serious baada ya hapo. Tukapotezeana moja kwa moja.

Sasa leo asubuhi, miaka 4 badae nikiwa nimeingia sehemu moja hivi ambayo huwa naenda mara kwa mara kutafuta huduma..nikakutana uso kwa uso na yule jamaa wa Morogoro. Daaaah! ilikuwa kama ni watu tunaofahamiana muda mrefu. Tulipiga story pale na kufurahi akaniuliza uko wapi nikamwambia akafurahi sana kuniona nazidi kupiga hatua tofauti na tulivyoonana 2017 (To God be the glory). Hata yule mwenye ofisi alishangaa kuona mimi namfahamu huyu jamaa wa morogoro. Hii imemfanya huyu jamaa wa morogoro azidi kuaminika zaidi kwa yule mwenye ofisi maana naona huwa anapata huduma zak pale. Nilimaliza shida yangu nikaondoka pale nikawaacha, njia nzima nikawa nawaza hivi ingekuwaje kama yule jamaa wa morogoro angenidhulumu kipndi kile? Kama reputation yake kwa yule jamaa mtoa huduma si ingeharibika kwa sababu huenda ningemsagia kunguni zaidi ili asiaminike hata siku nyingine ukizingatia kuwa Uhusiano wao kibiashara bado mchanga..Kwa mazungumzo yao wamefahamiana/wameanza kuhudumiana mwezi wa 4 Mwishoni. Niliwaza na kujifunza kitu muhimu sana.

NB: Siku zote jitahidi kuwa fair, maisha sio leo tu. Unaemfanyia dhuluma leo kwa sababu hana uwezo wa kushindana na wewe au kukukamata kesho na kesho kutwa anaweza shikilia hatma ya maisha yako. Neno lake moja tu linaweza haribu mipango yako na imani uliyoijenga kwa watu. Tuache uswahili ili tusiishi kama digidigi siku za usoni.

It's ChooseDay ni uamuzi waku kuchagua kuwa fair au kuwa unfair. Have a blessed moment.​
 
Kinyume chake!
Mimi siku moja niko zangu mkoani kagera wilaya ya muleba,
Saa nne asubuhi naenda kupokea pesa posta kwa njia ya western Union.
Hapo dirishani navuta laki sita na thelathini hivi, na pembeni kulikua na muhaya mmoja umri kama miaka 45-50 ,mnene kitambi kilo mia katoka MAREKANI anatembea na passport mkononi (Philadelphia U.S)
Jamaa tukasalimiana fresh na story za hapa na pale akanambia kaja MSIBANI kijiji fulani.
Basi tukabadilishana namba kila mtu akaenda zake!
Siku mbili baadae kanipgia kunikopa elfu HAMSINI afix gari yake maana credit card yake inatatzo na baada ya siku moja au mbili atanirudishia.....!
Hadi leo mwaka wa tano sijaona pesa yangu
(Nimefupisha sana)
 
Ukute hata hiyo Philadelphia anaijulia kwenye movie😀
 
Hata mi ningemwambia " ishi sana Bro huna baya"
ni watu wachache sana ambao wanatimiza ahadi/waaminifu.
tukiachana na uaminifu kuna kitu kingine kinaitwa Ugomvi/Dharau! Mtu anafanya haya akijua kabisa maisha mzunguko, siku unajikuta mahala unahitaji msaada, wa kukusaidia ndio yule yule, ndo utajua hujui!!
 
Duuuh pole Sana mkuu
 
Hahahaha pole sana mkuu
 
hahahhahahahahah philadephia daaaahah
 
Hata mi ningemwambia " ishi sana Bro huna baya"
ni watu wachache sana ambao wanatimiza ahadi/waaminifu.
tukiachana na uaminifu kuna kitu kingine kinaitwa Ugomvi/Dharau! Mtu anafanya haya akijua kabisa maisha mzunguko, siku unajikuta mahala unahitaji msaada, wa kukusaidia ndio yule yule, ndo utajua hujui!!
wewe ni wakipekee sana Princess ariana..hunaga Baya kabisaa..we mzungu kabisa....uishi sana Boss

hahahahahahaha
 
Umenikumbusha jamaa tuliyehitimu chuo pamoja, wakati tupo tu home wote tunazagaa mitaani kutafuta mishe...

Yeye alipata issue ya data entry yalikuwa ni madodoso fulani kuyajaza kwenye Google form online ..zilikuwa ni karatasi nyingi sana .

Alinipa mishe nimsadie kwa makubaliano ya pesa kiasi fulani kama 150 hivi..

Nikafanya kazi, baada ya siku kadhaa za kupinda mgongo kwenye PC nimemaliza ,nikamkabidhi akasema tusikilizie mafao yetu..

Aisee zilipita week mara mwezi, jamaa hata sikuwa na msumbuwa nilimpigia simu kama mara mbili siku tofauti alinipa ahadi za uongo, kilichofuata aliamua kuniblock kabisa !!

Ikapita muda mrefu nakuja kukutana na yeye uso kwa uso anatetemeka na kucheka kinafki huku anajiongelesha kwa aibu..

I wish angemfanyia mtu mwenye roho mbaya amuitie mwizi!
 
Back
Top Bottom