Kuna kitu tunafichwa TRA

Yani wewe jamaa wewe nakukubali sana yani sina cha kukupa maana mara zote unakua na madini hatari hatari
 
Jpm hakurupuki aisee ukiona kafumua sehemu ujue anajua kuliko tunavyojua tatizo ni moja spidi yake ni Kali kuliko mazoea ya watz ndio maana ni kama hatumwelewi ila anajua anachokifanya kumbuka urais ni taasisi
 
Hahaaa tutasikia mengi sana mwaka huu!!! Ijumaa mkurugenzi jumatatatu mtuhumiwa!!!Ijumaa
 
Members wa bodi, yupo governor BOT, katibu Mkuu Mipango, mkuu wa Chuo Ifm, katibu mkuu wizara ya fedha znz, nadhani katibu mkuu wizara ya fedha plus some few guys
 
Hivi bodi ya mikopo aliyoikuta JPM ndio bado inaendelea?
 
Jpm hakurupuki aisee ukiona kafumua sehemu ujue anajua kuliko tunavyojua tatizo ni moja spidi yake ni Kali kuliko mazoea ya watz ndio maana ni kama hatumwelewi ila anajua anachokifanya kumbuka urais ni taasisi
Wewe kumbe ndiyo usiyeelewa ukweli wa mambo; unasema anajua mambo na hakurupuki, ulizia kuhusu yule mkuu wa Muhimbili aliyemtoa na mifano mingine kadhaa halafu utafahamu kama madai yako yana ukweli au hujui unachokiamini.
Usijidanganye kwamba kila anayemuondoa ni kwa sababu ya uzembe au kutokuwa na ufanisi, mengine anaingizwa mikenge anaishia kuwaondoa watu bila hatia.
 
Kilichoongezeka ni pesa hazina baada ya kuamuru pesa zote zilizokuwa zinawekwa kwenye akaunti za benki za idara, mashirika na taasisi za serikali zipelekwe BOT.

Ni sawa na baba aliyewaruhusu wanafamilia wake kila mmoja atunze pesa zake halafu siku moja akaamuru pesa za wanafamilia wote atakuwa anatunza yeye. Baada ya hapo akatangaza kipato chake kimeongezeka!
 
Najiuliza iweje mkuu apangue bodi iliyowezesha mapato kupanda hadi trilion 1.2 kwa mwezi.


Kuongezeka kwa mapato hakujatokana na Bodi kwasababu hiyo bodi ilikuwepo hata kabla ya mapato kupanda, nadhani kupanda kwa mapato nkumetokana na factor nyingine mbali na Bodi
 

Mkuu unauliza au unatupa habari?
 
Kumuingiza rais mkenge sio jambo dogo sio jambo ambalo MTU anatamani kulifanya sio jambo LA kawaida kumuingiza rais mkenge ni kama kauhaini ukimuingiza rais mkenge ni kama umeisaliti nchi na watu milioni 50 walioko nyuma yake bado naamini taasisi ya urais haikosei kwenye maamuzi maana inakuwa na taarifa za kutosha sana na kama wakikosea basi nisehemu ya mapungufu ya kibinadamu
 
Commissioner bado amebakiza kazi yake body imevunjwa; siku siku hiyo akateuliwa deputy commissioner.

The assumption kutokana na majukumu ya bodi chanzo cha kuvunjwa itakuwa internal power struggle za ndani kati ya body na commissioner wa TRA jinsi ya kufanya mambo. Habari za kupanga kodi hakuna mwenye mamlaka hayo zaidi ya waziri wa fedha.
 
Ndo upige bodi nzima chini na hapohapo mkusanya kodi no 2 uteuwe
Soma tangazo vizuri la serikali. Uliotenguliwa ni uteuzi wa mwenyekiti wa bodi siyo bodi nzima. Pia ufahamishwe kuwa Bodi ya TRA inaundwa na ex-official members kama ifuatavyo; Gavana wa BOT, Katibu Mkuu wizara ya fedha, Katibu Mkuu wizara ya fedha Zanzibar, Mwenyekiti Bodi ya Mapato Zanzibar(ZRB), Katibu Mkuu Tume ya Mipango, Mkuu wa Chuo cha IFM, Kamishna Mkuu wa TRA na Company Secretary wa TRA. Hawateuliwi kwa majina bali nyazifa zao.
 
Mkuu mm ndo nimesoma vibaya au ww ebu soma vizuri bandiko la Msigwa apo usikurupuke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…