Kuna kipindi watanzania watakata tamaa ya kuchangia kwenye maafa yanayolikumba taifa.

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Ukweli itafikia kipind kuna kipindi watanzania watakata tamaa ya kuchangia kwenye maafa yanayolikumba taifa. Kumekuwa na usimamizi mbaya wa misaada inayotolewa.
Wananchi wa Kagera waliopatwa na tetemeko la ardhi watanzania wengi walijitoa sana katika kuwachangia wananchi hao lakini baada ile michango 50% hakuwafikia walengwa.
Wiki iliyopita ndani Jijini la Arusha kuna ajali mbaya ya gari imetokea Karatu ilipoteza wanafunzi 32 pamoja watatu 3. Wananchi kwa kushirikiana na kampuni mbalimbali tukaamua kutoa michango yetu kwa ajili kusaidia zile familia lakini jambo la kushangaza michango ambayo imetolewa na pesa ambazo wamepewa wafiwa haziendani na pesa ambazo zimetolewa. Jana nimejaribu kuwasiliana na familia za wafiwa huko Jijini Arusha nimesikitishwa sana matumizi mabaya ya pesa za wafiwa kwenye matumizi ambayo tuliambiwa serikali inagharamia.
Kama hali ya kupoteza uaminifu kwenye michango kama hii itafikia hatua wananchi watakaa tamaa kutoa michango yao kwenye maafa. Jijini Arusha Mkuu wa wilaya Arusha
Bw. Gabriel Fabian Daqarro anasema wafiwa wamepewa milioni moja, Mkuu wa mkoa Mrisho Gambo anasema milioni tatu laki tatu na elfu themanini.
 
Jamaa alishaongea kwa kiburi kikubwa kuwa alienda Dodoma kuchukua fomu ya Urais mwenyewe...........

Kwa hiyo hataki mtanzania yeyote amuelekeze la kufanya!

Keshasahau kabisa kuwa cheo ni dhamana na sisi wapiga kura wake tuliomwingiza Ikulu, tuna wajibu wa kumuelekeza mambo ya kufanya.

Iwapo ataendelea kuleta kiburi na kujiona yeye ndiye yeye.......

Tunasubiri mwaka 2020 tuone kama kura yake moja na ya pili ya mama Jesca, kama kura hizo ndizo zitakazomrudisha Ikulu!
 
Jamaa alishaongea kwa kiburi kikubwa kuwa alienda Dodoma kuchukua fomu ya Urais mwenyewe...........

Kwa hiyo hataki mtanzania yeyote amuelekeze la kufanya!

Keshasahau kabisa kuwa cheo ni dhamana na sisi wapiga kura wake tuliomwingiza Ikulu, tuna wajibu wa kumuelekeza mambo ya kufanya.

Iwapo ataendelea kuleta kiburi na kiujiona yeye ndiye yeye.......

Tunasubiri mwaka 2020 tuone kama kura yake moja na ya pili ya mama Jesca, kama kura hizo ndizo zitakazomrudisha Ikulu!
Utafanya nini ndugu, dua la kuku, cha msingi tukubali amalize awamu yake, hakuna uwezalo kufanya kwa sasa. Mtazamo wangu waweza kuukosoa.
 
Hilo liko wazi, wanaohusika wajipange. Walisema serikali itashughurikia gharama za mazishi. Taarifa ilipo toka hela za rambirambi ndio zimefanya kazi hiyo mpaka kulipia magari ya jeshi na ambulance kuleta miili uwanjani ajabu. Nawaomba wahusika wajue kuwa kila wanalosema na kutenda linahifadhiwa kwa ajili ya leo na kesho kudanganya ni kazi ngumu sana siku hizi "technolojia" imeshadhibiti mwanya huo. Tunauliza Mchango wa serikali katika janga hili ni shilingi ngapi imetoka? Lazima ieleweke kuwa kuna wajibu na mchango ni vitu viwili tofauti, tukiondoa wajibu mchango wa serikali ni nini katika hili?
 
Jamaa alishaongea kwa kiburi kikubwa kuwa alienda Dodoma kuchukua fomu ya Urais mwenyewe...........

Kwa hiyo hataki mtanzania yeyote amuelekeze la kufanya!

Keshasahau kabisa kuwa cheo ni dhamana na sisi wapiga kura wake tuliomwingiza Ikulu, tuna wajibu wa kumuelekeza mambo ya kufanya.

Iwapo ataendelea kuleta kiburi na kiujiona yeye ndiye yeye.......

Tunasubiri mwaka 2020 tuone kama kura yake moja na ya pili ya mama Jesca, kama kura hizo ndizo zitakazomrudisha Ikulu!
Marekebisho ndg fadhali,ni kura 3 sio 2(mbunge kessi)
 
Utafanya nini ndugu, dua la kuku, cha msingi tukubali amalize awamu yake, hakuna uwezalo kufanya kwa sasa. Mtazamo wangu waweza kuukosoa.
Kama tungekuwa na Tume huru ya uchaguzi, uwezekano wa jamaa kurejea kwenye nafasi ya Upresidaa ingekuwa finyu sawasawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano!

Lakini as far as Tume zetu za uchaguzi zinaongozwa na makada wa kijani wa dizaini ya akina Jecha, nakubaliana na kauli yako kuwa hata kama 2020 atapigiwa kura moja tu ya mama Jesca, lakini bado Mwenyekiti wa Tume atamtangaza yeye kama mshindi!
 
Halaf tumuombee eti,

Huu ni zaidi ya uuaji kiongozi wa juu wa nchi anakosa utu.

Hatari sana.
Siku zote nimekuwa nikisema siwezi kupoteza muda wangu kumwombea mtu mnafiki ambaye hana hofu ya Mungu. Watanzania itafikia hatua hakuna ambaye atachangia maafa kutokana na tabia za mbovu watu wachache kutumia fursa za matatizo kwa maslahi yao binafsi!
 
Yaani hili ni janga kubwa, halafu mkuu wa wilaya anasema wafiwa wamepewa milioni moja, mkuu wa mkoa anasema milioni tatu laki tatu na elfu themanini, inaelekea hata kwenye maandalizi ya kutumia hizi rambirambi hakukuwa na kamati ila kila moja alifanya yake, yaani taarifa zinakinzana, na sijui kwa nini kutumia rambirambi kwenda kuanika yale majeneza pale na kusababisha usumbufu kwa wafiwa kufika usiku kuzika watoto wao, serikali ingependa kutoa heshima ingetumia pesa yake..inasikitisha.
 
mhh.....ila bado ni wetu, tuendelee kuwa wavumilivu kwani nipindi cha mpito naamini mambo yatakuwa sawiya....
 
Kama tungekuwa na Tume huru ya uchaguzi, uwezekano wa jamaa kurejea kwenye nafasi ya Upresidaa ingekuwa finyu sawasawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano!

Lakini as far as Tume zetu zetu za uchaguzi zinaongozwa na makada wa kijani wa dizaini ya akina Jecha, nakubaliana na kauli yako kuwa hata kama 2020 atapigiwa kura moja tu ya mama Jesca, lakini bado Mwenyekiti wa Tume atamtangaza yeye kama mshindi!
Watanzania bila kupiga kelele katiba kufanyiwa marekebisho kuwepo na Tume Huru ya uchaguzi tutaendelea kulalamika kwenye uchaguzi mpaka mwaka 2050 bila Tume ya uchaguzi haya maharamia hayawezi kuondoka madarakani.
 
Hakuna haramia ni mfumo tu jamani ambao uliachwa na mzee wa taifa, ila busara inahitajika au mabadiliko ya katiba ni muhimu.
 
Utafanya nini ndugu, dua la kuku, cha msingi tukubali amalize awamu yake, hakuna uwezalo kufanya kwa sasa. Mtazamo wangu waweza kuukosoa.

Ambacho wengi hatukitarajiii 2020 hakuna kupiga kira za urais.
 
Back
Top Bottom