Kuna katazo la bajaji kuingia katikati ya jiji la Dar Es Salaam?

lushalila

JF-Expert Member
Feb 23, 2015
283
107
Wanajamii forum,

Toka wiki iliyopita kuna kamatakamata ya bajaji kwa kigezo kwamba kuna katazo la bajaji zisizoendeshwa na walemavu kuingia mjini.

Binafsi sijasikia katazo Hilo naomba anayejua zaidi tujuzane.
 
Kwa uwazi kusema ukweli ili miji iwe endelevu lazima kuwepo na sheria, utaratibu na miongozo ya kuweka mambo sawa!, bila utaratibu ni fujo!!! Sasa kama kariakoo ukitembea Kwa waenda Kwa miguu kumezibwa na biashara, parking hakuna boda na Bajaji kila Kona!! Tunaomba tujitahidi kuweka utaratibu tupunguze siasa, hata mlemavu aandaliwe utaratibu kama uwepo wake mahali unaleta kuwazuia wengine lazima kuwe na utaratibu, ulemavu usiwe ticket ya kuvunja sheria!! Njoo barabara ya uhuru Mtaa WA Kongo barabara imezibwa kabisa haipitiki!! Ndio tuseme ulemavu ndio uzuie wengine kupata riziki Kwa kuwahi wanakokwenda!?
 
Tuwe wawazi tuache siasa, boda boda kama ni biashara rasmi kuandaliwe utaratibu, ila Kwa uendeshwaji WA bodaboda na Bajaji mjini ni hatarishi sana Kwa watumiaji wengine, wabanwe na sheria, huwezi ona abiria na kugeuza chombo hapo Kwa hapo!!
 
Kwa uwazi kusema ukweli ili miji iwe endelevu lazima kuwepo na sheria, utaratibu na miongozo ya kuweka mambo sawa!, bila utaratibu ni fujo!!! Sasa kama kariakoo ukitembea Kwa waenda Kwa miguu kumezibwa na biashara, parking hakuna boda na Bajaji kila Kona!! Tunaomba tujitahidi kuweka utaratibu tupunguze siasa, hata mlemavu aandaliwe utaratibu kama uwepo wake mahali unaleta kuwazuia wengine lazima kuwe na utaratibu, ulemavu usiwe ticket ya kuvunja sheria!! Njoo barabara ya uhuru Mtaa WA Kongo barabara imezibwa kabisa haipitiki!! Ndio tuseme ulemavu ndio uzuie wengine kupata riziki Kwa kuwahi wanakokwenda!?
Hilo no sawa ,Ila wanakamata unatembea barabarani sio umepaki Kama wengine tunaendesha bolt upski mjini ili iweje?
 
Hilo no sawa ,Ila wanakamata unatembea barabarani sio umepaki Kama wengine tunaendesha bolt upski mjini ili iweje?
Nimeongelea zaida sheria na utaratibu utakaosimamiwa na Sio kuleta tafrani!! Sijasema popote watu wakamatwe hovyo!!

Mbona utaratibu ukiwekwa kila mtu atafurahi, na pia siku zote tunaelekezwa mlemavu asibaguliwe na Sio kutoa upendeleo WA wazi, Kwa mawazo yangu uwekwe utaratibu na kwenye kusimamia huo utaratibu ndio angala asilimia Fulani kuwepo na upendeleo Kwa walemavu!! Kila mtu anahitaji riziki!!

Mlemavu WA macho, mlemavu WA miguu, mlemavu WA mikono, inabidi ahakikiwe na uwepo WA leseni yenye kumruhusu kuweza kuendesha chombo Cha kufanya biashara rasmi ya kubeba abiria, zaidi ya hapo ni kuongezeka Kwa madhara Kwa abiria, nk nk Hivyo nasisitiza kuwepo na utaratibu rasmi na Sio upendeleo rasmi
 
Kumekuwepo na usumbufu wa kamatakamata ya bajaji ndani ya jiji la dar es salaam lakini hakuna maelezo kutoka kwa mamlaka, tunaomba wenye mamlaka au yeyote anayejua undani wa sualahili atufahamishe vizuri
 
Wanajamii forum,

Toka wiki iliyopita kuna kamatakamata ya bajaji kwa kigezo kwamba kuna katazo la bajaji zisizoendeshwa na walemavu kuingia mjini.

Binafsi sijasikia katazo Hilo naomba anayejua zaidi tujuzane.

Makelele ya tozo lazima yaje na makasiriko
 
Back
Top Bottom