Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,266
Niko maeneo ya nyumbani napunga upepo. Barabarani anapita mbwa jike akienda anakojua huku akichechemea. Ni mzazi kwani ana watoto wadogo kwani nimeshawaona. Wamekua kiasi na wana afya njema. Wanavutia. WIki mbili kabla nilimwona. alikuwa kakonda sana. Bila shaka ni kutokana na uzazi na mishemishe za kujitafutia chakula ili wanawe wapate maziwa.
Miezi michache kabla palikuwa hapatoshi hapa jirani kwani usiku tulikuwa tukisikia makelele ya mbwa wengi sana. Walikuwa wanakuja kumuwania kwani alikuwa kwenye siku zake. Kipindi hicho yeye ndiye alikuwa malkia kati ya msitu wa mijibwa dume. Alikuwa mkali bila shaka akichagua pia nani wa kumpanda. Hatimaye aliyefanikiwa alifanikiwa na matokeo yake tumeyaona.
Sasa kilichonifanya nipate mawazo ni jinsi nilivyomwona akirudi tena. Akimbia kiasi huku mguu wake wa mbele kaunyanya akichechemea. Kuna mtu/jitu limepiga bila shaka. Sasa nafikiria. Huyu mbwa ana watoto. Anajitafutia chakula na watu wanampiga hadi kumtengua mguu (hawezi kuumia huvu hivi tu). Amekonda na matiti yake yanakwenda huko na huko. Anarudi kuwafuata wanawe akiwa katika hali ya hayo mahangaiko. Bahati nzuri sana wanyama (ukitoa binadamu) hasa wa kike ni vigumu sana kutelekeza watoto wao. Najiuliza; yale madume yameenda wapi? Ule umalkia umeenda wapi? Bila shaka watasubiri tena wakati ukifika, watoto wakikua, mama akipata tena afya nzuri, akiwa tena kwenye siku zake ndio wajitokeze kumuwania kumpanda. Sishangai kwanini huwa jike anakuwa mkali sasa. Anajua mzigo na kazi iliyo mbele yake. Lakini kwa kuwa ni jambo lisiloepukika kwake, hukubali kupandwa.
Hata haya kwa wanadamu yapo pia. Wapo kweli wanawake wanaosababisha kukimbiwa na wenza wao. Wengi wao wanaokimbiwa ni wale ambao wanaume walishindwa kuutukuza uanaume wao wakabaki kuwa majina tu. Wakati wa furaha huisha au hukoma. Si kila wakati ni wa kufurahia kwenye mahusiano. Kuna wakati wa kuonyesha umuhimu wa jinsia yako (mwanamke na mwanaume). Tuwaheshimu sana hawa wa jinsia ya kike maana bila kutafakari vizuri hatuwezi kujua wanapitia hali gani bila kujalisha nyakati katika mzunguko wa maisha yao. Nao wanawake wasiwe vyanzo vya wao kufanya wanayofanyiwa. Uhalisia/uasilia unaonyesha kuwa mwanamke atazaa kwa uchungu. Hii inahusisha pia ubebaji wa mimba hadi malezi. Si kujifungua tu. Nae mwanaume atakula kwa jasho. MWanamke uheshimu hali ya mwanaume akiwa katika utafutaji hadi kupatikana kwa kinachotafutwa.
Wakati mwingine kinachotafutwa hakiwezi kukidhi haja ya mahitaji yaliyopo. Hii isiwe tiketi ya mwanamke kufanya maamuzi kihisia kukidhi mapungufu anayodhani ni muhimu kwake. Naye mwanaume aheshimu hali yoyote (ILIYO HALALI) ya mwanamke.
Kila kilichoko mbele yako ni somo.