Kuna ishara kabla ya kufikwa na mauti

Ila vifo hivi hua vina ishara

Nakumbuka namna umauti ulivyomkuta mzee wangu..mzee wangu alikuwa mpenda ulabu sana na alikuwa na bar zake mbili anazipenda sana usipomkuta kwenye moja wapo Kati ya hizo sijui kwekweli.

Siku ambayo umauti ulimkuta hiyo siku alinunulia sana watu bia..na alikuwa anakaa baa moja anakunywa na kulipia wengine alafu anavuka barabara kwenda bar nyingine ambayo pia hunywa apo ..alifanya hivyo kama mara 3 hivi..mara ya mwisho alicheza sana mziki na kufanya kitendo cha kuwapa mikono watu waliopo pale bar..

Alivyomaliza avuke barabara aende upande wa pili kuchukua usafiri wake arudi home..anamalizia tu barabara boda boda ikaja ikamsomba na kumtupa mtaroni hakuomba hata maji.

R.i.p Baba
 
Kuna dogo mmoja shule ya msingi niliyosoma mkoani kwetu Kilimanjaro. Ilikuwa hivi.

Kwa kawaida shule za vijijini tuna desturi kukimbia mchakamchaka kabla ya kuingia darasani.

Sasa siku ya tukio, tulikimbia vizuri mchakamchaka baadae tukaingia madarasani. Ilipofika mida ya saa nne, dogo alianza kuwaaga wenzake akiwaambia "naenda zangu Marekani na sita rudi tena"

Dogo alipita kila dawati akiwaambia hivyo wenzake. Baadae alirudi kwenye dawati lake akakaa. Ilipofika mida ya break, aliamka kwenda nje.

Bahati mbaya alijikwaa kwenye dawati akaanguka chini sakafuni akapiga eneo ya kisogo. Akadondoka chini akaanza kugeuza macho na mapovu yakimtoka.

Tulienda parokiani kuomba gari, ili kumpeleka hospitali. Tulipofika daktari alisema "kijana hatunae tena"..

Ikawa ndio mwisho wake hivyo. So nahisi kuna connection flani hivi wakati kifo kinapomkaribia mtu.
Na je wakati anawaaga anakwenda marekani mlimdadisi kwamba angeenda kwa njia gani?nauli ya kwenda huko alikuwa nayo?visa alishaandaa?
 
December 24, 2010 nilipata msiba ukweni, nikamwambia bibi naenda mkoani kwenye mazishi.

Aliniuliza unarudi kabla ya mwaka mpya au? Nikamjibu tarehe 29 au 30 tunarudi na yeye akaniambia kama hivyo sawa maana ikizidi mwaka mpya hautonikuta.

Mm na wife tulirudi tarehe 29 bibi akiwa yupo poa akafurahi sana na kusema bora umerudi kama ulivyosema na tarehe 30 nikaondoka na wife mlimani city tupate vitu vya kusherehekea mwaka mpya na hii ilikuwa saa tisa jioni nimemuaga bibi vizuri kabisa.

Nimerudi nikakaa mahali na wife angalau nipate 🍺 mbili napata taarifa ambayo sikuielewa kabisa kuwa bibi alijisikia vibaya na akapatiwa usafiri kwenda hospitali kwenda hospitali ya jirani lkn tangu afikie hali hiyo haikuchukua hata dk kumi akafariki.

Bibi alikuwa na 72 kiumri unaweza sema alikula chumvi ya kutosha lkn aliona kinachofuata.
 
Daaaaah
Ila vifo hivi hua vina ishara

Nakumbuka namna umauti ulivyomkuta mzee wangu..mzee wangu alikuwa mpenda ulabu sana na alikuwa na bar zake mbili anazipenda sana usipomkuta kwenye moja wapo Kati ya hizo sijui kwekweli.

Siku ambayo umauti ulimkuta hiyo siku alinunulia sana watu bia..na alikuwa anakaa baa moja anakunywa na kulipia wengine alafu anavuka barabara kwenda bar nyingine ambayo pia hunywa apo ..alifanya hivyo kama mara 3 hivi..mara ya mwisho alicheza sana mziki na kufanya kitendo cha kuwapa mikono watu waliopo pale bar..

Alivyomaliza avuke barabara aende upande wa pili kuchukua usafiri wake arudi home..anamalizia tu barabara boda boda ikaja ikamsomba na kumtupa mtaroni hakuomba hata maji.

R.i.p Baba
 
Ukarimu...kuangalia chini mda mwingi, kutokupenda kula, kupenda kuona familia ikiwa iko pamoja wakat anaumwa...

La kuangalia chini au kutokuangalia watu usoni hili nimeliona kwa watu wawili walioaga dunia
Kuna Siri kubwa kwenye kifo ila huwa hatujui mengi
Mungu awarehemu wote waliotangulia
 
Back
Top Bottom