Kuna haja ya kulala ukweni?

Kuna haja ya kulala ukweni?

Udochi

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2015
Posts
1,073
Reaction score
1,576
Waheshimiwa malijendi,

Tangu nioe ni miaka miwili imepita. Ndoa ilihudhuriwa na wazazi wote na ndugu wachache waliopata nafasi.

Kesho nina safari ya mishe zangu tu za kutafuta riziki. Wilaya niendayo ndiko kilipo kijiji cha wazazi na jamaa wa mke wangu, na nitaenda huko kijijini kuwasabahi na kuwaona baadhi ya ndugu zake.

Je, kuna haja ya lijendi kulala pale ukweni au niwasabahi tu kisha nikalale zangu town?
 
Waheshimiwa malijendi,
Tangu nioe ni miaka miwili imepita.
Ndoa ilihudhuriwa na wazazi wote na ndugu wachache waliopata nafasi.

Kesho nina safari ya mishe zangu tu za kutafuta riziki.
Wilaya niendayo ndiko kilipo kijiji cha wazazi na jamaa wa mke wangu, na nitaenda huko kijijini kuwasabahi na kuwaona baadhi ya ndugu zake.

Je kuna haja ya lijendi kulala pale ukweni au niwasabahi tu kisha nikalale zangu town?
Mie nina miaka 8 kwenye ndoa sijawahi lala ukweni. Hata niwe na issue mpaka saa 4 usiku lazima nisepe au nikalale sehemu nyingine na nimezoea hivyo. Yaani hata wife analijua hilo.
 
Inategemea na mazingira lakini kama kuna shemeji zako wa kiume wenye makazi Yao pumziko hapo kuliko kwa baba mkwe, au lala kwa mshenga
 
Lijendi inategemea na desturi za ukweni kwako na mazingira ya nyumba ila ni vizuri ukafata ushauri wa wengi usilale hapo kama mkeo hayupo ova
 
Waheshimiwa malijendi,
Tangu nioe ni miaka miwili imepita.
Ndoa ilihudhuriwa na wazazi wote na ndugu wachache waliopata nafasi.

Kesho nina safari ya mishe zangu tu za kutafuta riziki.
Wilaya niendayo ndiko kilipo kijiji cha wazazi na jamaa wa mke wangu, na nitaenda huko kijijini kuwasabahi na kuwaona baadhi ya ndugu zake.

Je kuna haja ya lijendi kulala pale ukweni au niwasabahi tu kisha nikalale zangu town?
Malijendari hawalali ukweni.
 
Kama utawaachia mpunga mrefu, lala hapo. Lakini kama ni kuwasalimia tu, na kuacha hela ndogo ya mboga, kalale mjini.
 
Salimia kisha nenda town ukalale ili heshima iongeze kama upo na mke sawa ila siku chache sanaa.
 
Back
Top Bottom