Kuna haja ya kuacha nidhamu ya uoga. Here is why...

Babu sea

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
953
742
Nikitafakari mahusiano yetu sisi watanzania kuanzia maofisini,kwenye maisha ya kijamii na kwenye biashara bado tuna tatizo la kuhofiana.

Mtu anaweza kuona kitu flani ni cheusi lakini hawezi kusema hisia zake katika jambo hilo kama ni ofisini anaogopa bosi wake atachukia kwa hiyo anaishia kucheka cheka nakujifanya hakuna kilichotokea.

Sisemi tuwe agressive, No! Namaanisha ule uwezo wa kusema nini unakitaka na kujielezea kile unachotaka bila kufeel gulty(assertiveness) bado kwa wa tz ni mtihani mtanzania anweza kuuziwa hata kitu kibovu dukaani na wala asiseme No.

Kuna kampuni moja ya mchina Singida ilikua inawadhalilisha wanawake kwa walinzi wa kiume kupapasa maungo yao wakati wa ukaguzi getini na kuwavua hadi nguo za ndani lakini cha kushangaza mchina huyo hakufanyiwa chochote.

Mkuu mmoja wa wilaya aliwatandika walimu wa shule flani mikwaju cha kushangaza hakuna hata Mwalimu mmoja aliyesema hapana.

Kiongozi mmoja anaweza akaingia na kuondoa demokrasia pasipo ha mtz mmoja kusema No; madhara yake ni kuzalisha viongozi wanaotu-manipulate ili wapate wanachotaka kwa kututisha, kutuonea na hatakutuburuza.

Nini kifanyike?

Watanzania tuache kujijengea hofu zisizokuwa na faida kisa kazi; unakubali hata kunyanyaswa eti kisa urafiki. Ndio unakubali kuuziwa hata nyanya mbovu; kisa mmezaa watoto ndio unakubali mke/mme achepuke.

Leo ningependa kutoa suggested assertive rights, zipo nyingi ni tataja chache kama:

1. You have the right to say I don't care
2. You have the right to say I don't love it
3. You have the right to say I don't know

Nimekumbuka hizi chache lakini kama na wewe unazo unazozijua weka hapa ili na wengine wafaidike.

Pia jitahidini kusoma vitabu kama vile "How to heal toxic shame", Vitabu vya communication skills na vitabu vya argument kama vile cha Neil Brown pia "Thank you for arguing".

Kuna vitabu vingi sana kwenye mitandao, hivi nilivyo vitaja ni miongoni mwa vingi sana. Naomba kama kuna mtu mwingine anafahamu vitabu vingine aweke hapa kwa faida ya wengi
 
Babu sea
Kuna kamsamiati fulani tulikuwa tunasisitizwa sana kukatii na walezi/wazazi/viongozi wetu

1."JIFANYE MJINGA SIKU IPITE"

2."KUNGURU MWOGA HUISHI MIAKA MINGI"

3."FUMBA MAJI KINYWANI"

Hizi sijui methali,sijui vitu gani,vilihubiriwa sana karibu nchi nzima,matokeo yake watu wakajenga dhana kwamba kukaa kimya ndiyo ustaarabu,kumbe ni ujinga kweli kweli!

Watu wanafanyiwa unyama wa hali ya juu lakini ili aonekane shujaa eti ni anakaa kimya!

Sijui hizi dhana zitakwisha lini,mbaya zaidi anayejitahidi kusema inapotokea anaonewa anaonekana hana nidhamu,ni mtukutu na sio mstaarabu!jamii kwa sehemu kubwa itakuina usiyefaa!!!

Hii ndiyo nchi yetu!
 
Back
Top Bottom