Kuna haja ya baadhi ya wafanyakazi wa idara kwenye Makampuni Binafsi ziwe na wafanyakazi wa Serikalini

Vikra mbadala

New Member
Aug 18, 2020
2
1
Niende moja kwa moja kwenye hoja yangu.

Baada ya kuona jitihada kubwa za Serikali kusimamia mapato na kukusanya kodi ikiwa ni pamoja na kutambua mchango wa wafanyakazi kutoka Sekta Binafsi na zile za umma, sasa ni muda muafaka awamu hii pia ijaribu kufikiria kama itafaa kufanya hivi:

Makampuni makubwa hasa ya uzalishaji ambayo yanafanya kazi na watu kutoka nje ya nchi (expatriate), idara kama Accounts na HR wajiriwa wake wawe chini ya serikali.

NB: Nimezungumzia makampuni makubwa.

Sababu za kuzitaja hizi idara ni zipi?

Hawa watu wanajua badhi ya janja janja zinazofanyika na wajiri (kama zipo) ila wanaogopa maboss zao au kupoteza ajira zao
 
Back
Top Bottom