Kuna haja wa viongozi wa kisiasa kumuangalia huyu!!!

PAPAKINYI - SJUT 2013

JF-Expert Member
Jun 5, 2017
367
250
Kuna haka kadada kanajiita Gigy Money,..kutwa kucha kazi yake ni kujianika uchi, kutengeneza video za uchi na kuziweka youtube pamoja na kutoa masomo ya umuhimu wa umalaya.

Kama mzaha, lakini taratibu dada huyu anaanza kushika chati kutokana na uozo wa vyombo vyetu vya habari kuwapa kiki watu kama hao. visichana vyetu vya shule navyo vinaanza kuharibiwa na matendo yake kwa kasi tu....

Ijumaa ya trh 2/6/2017 nilikuwa Buguruni malapa ofisi za startimes, wakati natoka nilikutana na vitoto vya shule fulani ya mchepuo wa kiingereza ipo pale nyuma ya zile hostel za st. marks....walikuwa na maongezi yao ya 'social issues' huku wakitumia lugha yao ya kiingereza, nilimsikia mmoja akisema, ' when i grow up i'be twerting like gigy....hahahahahhhh'.

Nafikiri kuna haja kwa viongozi wetu akina Mwakyembe ya kuongea na huyu dada kama walivyofanya kwa Nay wa Mitego pengine atapunguza kidogo haya mambo ya ajabu....najua matendo ya kishetani yapo mengi tu, lakini jinsi alivyokuja huyu dada inanitisha sana aiseee!

Karibuni kushare, najua mko bize na bajeti, mauaji ya Pwani n.k.lakini hili nalo ni kubwa sana.
 
Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
44,074
2,000

Mjini hapa yupo kibiashara zaidi
 
The Businessman

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
7,412
2,000
Watu kama gigy nao wameshajua Watanzania tunapendelea nini!

Ingekuwa ni watu ambao hatupendelei hayo wanayoyafanya watu kama high money wasingekuwepo.

Gigy money ni reaction ya sisi tulivyo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom