Kuna baadhi ya wanaume Mungu anawaona

Kuna baadhi ya wanaume Mungu anawaona

  • Thread starter Thread starter Deleted member 485868
  • Start date Start date
D

Deleted member 485868

Guest
Kuna Mwanamke yamemtokea ambayo yanaumiza sana

Huyu mwanamke tunaishi nae mtaa mmoja amepanga kwa mmoja wa majirani zetu hapa mtaani

Ameishi na mwanaume wake kama miaka 3 hivi kabla ya huyo mwanaume kupatwa na matatizo alipokua anafanyia kazi..huyo mwanaume alikua muhasibu kampuni fulani..na hiyo kazi aliipata baada ya kua na huyu mwanamke..walipokutana mwanaume hakua na kazi na alikua anaishi kwao..baada ya kupatana na huyu mwanamke na kupendana mwanamke akamshawishi mwanaume wakapange na wakati huo mwanamke alikua anauza matunda mara mboga za majani ili mradi wapate pesa ya kula na kulipia kodi

Mwanamke ameishia kidato cha nne mwanaume anadegree..baada ya kama miezi mitano katika kuishi kwao mwanaume akapata kazi ya uhasibu..amefanya kazi mara akaanza kunywa pombe pombe na yeye..akilewa matusi na kejeli kwa wingi kwa huyo mwanamke wake mwanamke alikua anavumilia sababu alikua anampenda huyo mwanaume..na hapo mwanamke alikua muislam na mwanaume ni mkristo..kwa mapenzi yake mwanamke akabadili dini kumfuata mwanaume..kwahiyo wakaamua kuokoka ingawa mwanaume alikua cha pombe

Maisha yakaenda kazini kwa mwanaume kukatokea wizi wa pesa na alietuhumiwa ni yule mwanaume..lakini katika kuishi kwao mwanamke akamshawishi mwanaume wakanunua kiwanja uko tungi kigamboni..mwanaume akawekwa hatiani kesi ikaanza unguruma na hapo wakati mwanaume kapata kazi alimwambia mkewe aache kufanya biashara na mwanamke akatii akaacha..kesi imeunguruma weeeh ilibidi mwanaumke auze kiwanja ili kumsaidia mumewe..paamoja na kuhonga kote haikusaidia kitu mwanaume akapigwa nyundo miaka nane jela..na hapo tayari walikua na mtoto wa mwaka na miezi 8 na mwanaume alipofungwa alimuacha mkewe na mimba

Mtihani ukaanzia hapo pesa hakuna mtoto anaitaji lishe mama mjamzito nae anahitaji huduma na walikopanga mwenye nyumba anataka pesa zake..patamu hapo!! Mwanamke kwenda kwao hawezi sababu wazazi walishamkana baada ya kubadili dini..jamani huyu mwanamke alikuaga mrembo ila baada ya matatizo urembo wote ukatoweka yani ukimuangalia waweza sema kazaliwa miaka ya 70 huko kumbe wa 90

Mambo yalizidi kua mabaya ..mwanamke akaona isiewe shida kuna siku akaja nyumbani kwetu kuja kuomba angalau pesa ya mtaji wa biashara bahati nzuri akapatiwa..sasa akaanza kuuza mihogo asubuhi mihogo jioni sambusa na Mungu alivyomwema hakuna siku biashara yake ililala na ..na kila ukifika muda wa kutembelea wafungwa ilikua lazima aende kumtembelea mume..muda ukafika wa kujifungua akajifungua..na kipindi anafanya biashara za kuuza mihogo na sambusa akashauriwa ajiunge na vicoba..huyu mwanamke jamani alijitahidi mpaka akanunua kiwanja maeneo ya kisewe uko mbande

Mume akatoka jela baada ya uchunguzi kufanyika..karudi uraiani hakukaa sana akapata kazi serikalini..wakahama walipopanga chumba na sebule wakaenda kupanga nyumba nzima..mwanaume kapata mchepuko..hasikii haambiwi..huyu mtoto aliemuachaga tumboni kamkana..kaiba hati ya kiwanja kauza..kamuacha mama watoto hana mbele wala nyuma..nyumba waliyopanga mwanamke kafukuzwa

Mwanamke akifikiria aende kwao anajiuliza ataanzia wapi..maisha ya wazazi ni duni nayeye ndie alikua tegemezi..watoto tangu wazaliwe hawajui upande wa Mama unafananaje..ingawa Mama yao alikua anajitahidi kutuma pesa kwao na kusalimia familia yake na kuomba msamaha ili apate kusamehewa

Sasa hivi huyu mwanamke yupo hospitali wiki ya pili sasa hajui anaeingia wala anaetoka..Mwanaume akipigiwa simu anasema hamtambui huyu mwanamke

WANAUME KUWENI NA HURUMA JAMANI
 
Maisha ni safari tena ndefu... Mungu atampa hata kile ambacho hajanyang'anywa.
Aombe Mola ampe afya na anaonekana elimu ndogo aliyonayo ni mtaji sana kwake kuliko mme wake mwenye degree ya ulimbukeni.
Dada mwenyeji wake usichoke kumpa sapot mwenzio na mshauri aanze maisha yake na asije kumkaribisha tena mwenye degree ya dhuruma.

Pole kwake.
 
Kauli yako ya mwisho hajakaaa sawa kabsa labda ulkuwa hujui tu wewe binadam akiamua kuuweka utu pembeni iwe Wa kiume au Wa kike dunia utaiona chungu kwa hyo hapo kila mwanadam na yake Leo ukiambiwa timbwili alilofanyiwa mwanaume na make flan mbona utasanda mwnyw
 
Pole yake mdada,mshauri akitoka hospital aanze maisha upya afanye vibiashara vyake na ,amtumainie Mungu atafanikiwa tu.wanaume wa hivyo wengi wao hawafiki mbali kimafanikio na chozi la mnyonge siku zote haliendi bure.!
 
Back
Top Bottom