Kuna anayemfahamu Mh Lazaro Nyalandu?

Kuna anayemfahamu Mh Lazaro Nyalandu?

Namfahamu Lazaro kuwa ni Mwana Singida mwenzangu, alitumia Helkopta kusaka Ubunge, Wakati wa kugombea ubunge alikamatwa na TAKUKURU amechinja Ng'ombe Kijiji cha Matumbo, Tarafa ya Mtinko Wilaya ya singida, lakini tangu alipokatwa hajawahi kutiwa hatiani, japo katika sakata hilo kuna Afisa wa TAKUKURU alikoswa na risasi usiku. Hii imebaki siri kubwa. Mwangalizi wa TEMCO katika Jimbo lake alikuwa binti hakusema lolote na baada ya uchaguzi tu huyo Binti wa TEMCO amebaki Singida hadi sasa.

Nyalandu pia alidanganya watoto akawapeleka Arusha akawaambia amewatafutia wafadhili, watoto wakalala Nkwaranga Sekondari, wakacheza mbele ya Wazungu hoteli inaitwa Arumeru Lodge, lakini tangu wametoka kule hawajaambulia kitu. Na sasa wanalalamika ila Kambi yake inasema ni Mafisadi wanamchafua hili sio kweli. Vijana wamedhulumiwa pesa yao, data tunazo, nitaziweka humu kesho asubuhi.

Kuhusu Uraia, madai hayo yalitajwa wakati wa kampeni na anayejua haya alikuwa ni Diwani wa kata ya Merya anaitwa Mutiana na kundi lake..... wana data full kuhusu Nyalandu kuwa na uraia wa nchi mbili.
Huyu huyu aliyedai Rais kamdhulumu
 
Back
Top Bottom