Wakuu Kibunango na Mtu wa Pwani,
Hakuna ambaye anataka maendeleo yaje yenyewe, kuna watu huko vijijini wanavuja jasho la damu na mwisho wa siku hakuna wanachopata. Mfano, juzi JK kapita Sumbawanga na Mby akaahidi kwamba ataongeza fedha za SGR ili kununua mahindi. Hakuna wanunuzi wa mahindi na serikali imepiga marufuku kuuza mahindi nje ya Tanzania, sasa niambie hapo mkulima afanye nini?
Nenda Lindi, wakulima wa Korosho wamevuna korosho zao, wakienda kuuza wanapewa stakabadhi kwamba malipo baadaye. Malipo yake hapo ni mbinde.
Kahawa ukiuza kwa wanunuzi kutoka Uganda unapewa bei nzuri, lakini ukiuza kwa vyama vya ushirika vya KNCU na KDCU, bei yake utalia. Sasa hao wakulima waende kuuza wapi na kuuza kwa waganda mnasema ni walanguzi.
Unasema hosp ni za Dar, umeishafika kwenye zahati za vijijini ambako hata wauguzi hakuna ila kuna wakunga wa jadi tu. Kuna shule zina mwalimu mmoja, hao watoto watasomaje?
Barabara za vijijini hazipitiki mwaka mzima, kila mwaka mnakuja na habari ya kutengeneza barabara ambazo zinahitaji ukarabati tu, feeder roads za vijijini hakuna anayeziangalia, matokeo yake wakulima wanabebeshwa gharama za kusafirisha mazao, pembejeo na mahitaji yao. Mwisho wa siku pembejeo bei juu, mazao bei chini, na bei ya mahitaji ni juu, cost of living inapanda mara 3 zaidi kuliko yule aliye mjini.
Kwa hiyo msiwatukane wananchi wa vijijini ati ni wavivu, wanajitahidi sana but juhudi zao za kujikamua zinakwazwa na matatizo ya barabara, masoko, na huduma duni za jamii.