Na kama utakuwa makini sana kila msg moja unayotuma inakatwa Tsh 300/=.
Kwangu mimi sishangai sana, maana hii inatokana na sisi watanzania kutaka mambo makubwa bila ya kujishughulisha, ndio maana inakuwa rahisi sana kwetu kuibiwa tena kwa urahisi.
Ukilifikiria sana hilo suala la zain, lazima utahisi kuna kitu kisicho na uhalali kinaendelea, haiingii akilini muda ambao msg inaingia na kile kinachozungumziwa katika msg hiyo kinakuwa contrary to each other. Nafikiri hili ni suala la kwanza kabisa la mtu kujiuliza mara mbili kabla ya kutenda.
Otherwise ngoja tusikilize wajumbe wenye ufahamu na jambo hili watoe mchango wao