Kumwambia mwanamke 'FANYA MAARIFA'

Umeoa na mke wako ni mama wa nyumbani. Katikati ya mwezi unajikuta una nauli tu ya kuendea kazini. Asubuhi unamuaga unamwambia hali ngumu afanye maarifa.
Mke amekopa kwa mangi. Kwa mapenzi aliyonayo kwako unakuta wali kuku na Mirinda ya baridi. Huulizi hela alipata wapi. Mbona mnatuacha kwenye hali mbaya?
Tunawapima tu kama nawo wanaweza kutafuta aise, sasa wakipasi huo mtihani basi wanaume roho zetu zawa kwatu kwamba kumbe tusipokuwepo Duniani wenzetu wataweza kutunza familia kwa kutumia akili na rasilimali zao..:);)
 
afanye maarifa ya jamii, yaani afanye improvisation ilimradi chakula kipatikane.
 
MKIAMBIWA MFANYE MAARIFA MAANA YAKE KAKOPENI KWA KINA MAMA NANII YANI MASHOGA ZENU AU UNAENDA KUZUGA KWENU UNACHUKUWA HATA VIMBOGAMBOGA .
 
Mfano miezi miwili iliyopita nimempa mke milioni moja ya matumizi yake binafsi,chakula bili za ndani nagharamia,alafu namuona amenunua wigi na viatu vipya wakati ndani ana viatu kibao,nakulia timing baada ya miezi miwili mingine hata kama nina hela ntakwambia nina pesa ya petrol au nauli masuala ya chakula tumia maarifa huku nakusoma utatumia maarifa gani, na kama ukienda kukopa nyama au unga, na ndani una wigi la laki tano na pea za viatu pea moja labda zaidi hata ya laki tatu ndiyo nitajua nina haina gani ya mwanamke na niishi naye vipi.
 
Nilibahatika kuishi sana na Wanigeria. Wao formula yao ya maisha ni kuwa nwanaume lazima uwe na biashara.

Kazi na biashara viende pamoja. Hata kama unalipwa laki na nusu hiyo ni guarantor ya kuchulia mkopo wa kuongezea biashara.

Mke ndiye ubavu wako, atasimamia biashara wakati wewe uko kwenye paid job.
Umeongea vyema.

Hebu fikiria mwanamke anachojua ni kuajiriwa na hataki biashara, uza maandaz... Sitaki. Uza mkaa.... Sitaki. Fungua duka.... Sitaki. Anataka kuajiriwa alipwe mshahara. Hapa wenyewe mnaleta mtihani,

Hapo mchepuko umeomba hela iongezee mtaji wa duka lake la rejareja au kutengeneza nyavu za kuuza mbogamboga kwa mangi au kununua sukari ya kutengenezea barafu.

Mwanamke mpumbavu ataivunja nyumba yake tu.
 
Ha ha ha ha hilo ni tatizo,ila fomula nzuri kama unauwezo kiasi fulani jaribu kuweka 'stock' hata ya miezi 3 n.k ya vitu vyote vya msingi,tenga fedha ya tahadhari,tenga fedha ya starehe n.k nadhani kufanya hivyo utakuwa umetatua changamoto ambazo si za lazima.
 
Umeoa na mke wako ni mama wa nyumbani. Katikati ya mwezi unajikuta una nauli tu ya kuendea kazini. Asubuhi unamuaga unamwambia hali ngumu afanye maarifa.

Mke amekopa kwa mangi. Kwa mapenzi aliyonayo kwako unakuta wali kuku na Miranda ya baridi. Huulizi hela alipata wapi. Mbona mnatuacha kwenye hali mbaya?
Huwezi kumwambia 'baba fulani maarifa nimekopa dukani' ?
 
MKIAMBIWA MFANYE MAARIFA MAANA YAKE KAKOPENI KWA KINA MAMA NANII YANI MASHOGA ZENU AU UNAENDA KUZUGA KWENU UNACHUKUWA HATA VIMBOGAMBOGA .
Sasa wao wakiambiwa wafanye maarifa wanafikiria kuuza papuchi!
 
Dah,ndio maana namuombea mke wangu akila siku asifikuzwe kazi,maana mambo kama haya yanahuzunisha sana ukianza kuwaza...
 
Hii topic imerudi tena...inaonekana research bado inaendelea donors hawajaridhiswa na matokeo ya awali hahaaaa
 
Umeoa na mke wako ni mama wa nyumbani. Katikati ya mwezi unajikuta una nauli tu ya kuendea kazini. Asubuhi unamuaga unamwambia hali ngumu afanye maarifa.

Mke amekopa kwa mangi. Kwa mapenzi aliyonayo kwako unakuta wali kuku na Miranda ya baridi. Huulizi hela alipata wapi. Mbona mnatuacha kwenye hali mbaya?

"KUNA UNGA NYUMBANI, AKOROGE UJI, KAITWA MWANAMKE, MSAIDIZI, NA SIFA NYINGINE NYINGI, SASA KAMA HAYO MUNGU ALIYOWAPA NA SIFA NYINGI MNAONA NI UMALAYA, TUTAKUWA TUMEKWISHA WANAUME ZENU"
 
Hivi mwanaume unashindwaje hata kumfungulia biashara ya genge mkeo aache kuwa mama wa nyumbani.akiwa busy huko hata kukusaliti inakuwa ngumu kidogo hawezi kuacha genge akaenda Lodge ila Sasa akiwa mama wa nyumbani umekaribisha michepuko tayari na umeipa uhuru.akiwa na biashara yake hamwezi kukosa hela ndogo ndogo za chakula.hiko ndicho nikiwazacho
Hata akiwa manager wa benki anaweza kuchepuka mkuu,Tabia mbaya hailetwi na matatizo ya hela.
 
Kazi yetu ni

1.Kuhakikisha malazi bora ya familia
2.Kuhakikisha matibabu bora ya familia,na shule ada zinalipwa
3.Kuhakikisha chakula kipo nyumbani 24/7
4.Na ustawi bora wa familia

Msamiati wa fanya fanya utaratibu ni uhuni,huwezi kuwa baba usiye na mipango endelevu ya familia
 
Kuna wanawake wana akili. Hela za matumizi unapompa ana-save kiaina siku ukisema kama hivyo hali ngumu anakusaidia siku hazilingani.
 
hio hua nia kauli ya kishenzi wala msizunguuuuuuuuuke oh hv hv yaani ukimuambia mke wako hivo unamaanisha akajibebishe kwa mwanaume yeyote ili apate msaasa alete .

ndio maana hio acheni kung'ata ng'ata maneno...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom