Kumuelewa huyu Mwanamke ni ngumu sana...

tompoo

Member
Jan 2, 2021
42
25
Wakuu mnaendeleaje na majukumu ya ujenzi wa Taifa?

Kama kichwa cha habari kinavyoeleza kuwa huyu kiumbe muda sometymz ni ngumu kinoma noma, basi bana kunaye demu mmoja hivi tulianza kama marafiki af badaye nikaja kumuelekeza ni jinsi gani namuelewa kimapenzi ikiwemo uzuri wake na nini.

Kilichotokea demu akawa ananitolea nje bana mara ningefanya hivo sema nina mshikaji wangu na mambo mengine kibao basi nikaamua kujiweka kando lakini kadri time inavyozidi kwenda coz bado tunaongea daily vizuri tu, naona demu ana wivu na mimi mfano akinichek naongea na manzi mwingine basi anawaka kishenzi na ikipita time bila kumjulia hali anawaza sana na kama ni nyimbo za mapenzi anan~dedicate sana tu.

Sasa kwa wajuzi wa mambo naomba tusaidiane hapa huyu demu nimuelewe vipi?

Nawasilisha.
 

Umenikumbusha demu fulani hivi, mwezi wa tano niliomba mechi akakubali, baadae jirani yangu akapita nae, nilipogundua akawa mkali kweli basi nikaendelea na mambo yangu lakini tukawa tunawasiliana kawaida tu ila anahitaji anipigie yeye binafsi siyo Mimi kumpigia..

Baadae akapotea kwenye mtaa wangu maana alikuwa na biashara fulani hivi, na jirani yangu nae alikuwa anauza duka sehemu akasababisha hasara boss wake akamuondoa, kuna siku nilijaribu kumpigia kumbe nipigwe block line zangu zote mpaka WhatsApp bila kujua, nikaishia kucheka.

Siku moja kwa bahati mbaya/nzuri nikakutana nae akaniambia ana maongezi na Mimi basi nikasema okay. Sasa kila siku ananipigia simu, nina zawadi yako ninataka kukupa, naomba utafute sehemu nzuri tukutane. Nikaona simu zimekuwa nyingi na namna alivyoonesha tabia yake mwanzoni nikamwambia tayari nimepata mtu mwingine, hivyo inakuwa ngumu kutoka, na vile vile uwezo wangu unakuwa mdogo kuhimili kutunza watu wawili kwa muda mmoja.

Tangu siku aliongea maneno ambayo sikuyaelewa na hajawahi kupiga simu tena, sababu yake ya kujitetea kwangu haikuwa na mashiko hata kidogo na nilikuwa nimepoteza tumaini na mzuka wa kuwa na mtu kama yule ambae ni muongo na mbabaishaji sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom