Kumsimanga Hayati Magufuli hakutaijenga CHADEMA kisiasa

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,377
1,952
Ni kama vile, kadri machungu ya kukaa benchi kwenye siasa za nchi hii. Hususan nje ya bunge! Kunawatesa sana makada na wafuasi wa Chadema. Na Hasa wale ambao walikuwa hawana ajira au shughuli zingine za kuendeshea Maisha yao.

Sasa kinachobakia ni kuamka asubuhi kuweka bando na kuanza kuandika upuuzi wenu mitandaoni! Pamoja na wale watumbuliwa wote. Mnagombana na "kaburi".

Mkijaribu kumfanya Magufuri aonekane alikuwa mbaya.kisa tu mmewekwa benchi na wananchi baada ya sera zake kuwaingia wananchi na kuwafanya wawapuuze!

Jaribuni kutafuta strategy zingine ili kukijenga chama chenu,badala ya kuendelea kuwaudhi wananchi kwa kumtukana Magufuli.

Jifunzeni kwenye matukio ya hivi karibuni!

Mwenyekiti wenu Mbowe,aliingia na hiyo gia Majukwaani,kilichotokea ni kupuuzwa.

Makamu Mwenyekiti wenu Tundu Lissu, nae alikuja na ameendelea na mtindo huo huo,matokeo yake imekuwa ni kuporomoka kwa kasi na kupuuzwa na wananchi.

Matokeo yake,amejikuta analazimika kurudi Ubelgiji kujipanga upya!

Niwaambie kitu Chadema na Pro-asali team mnaolipwa ujira humu kumbomoa Magufuli.

Magufuli amekufa ndio,lakini kuna wafuasi wake nchi nzima!
Magufuli amekufa ndio,lakini miradi yake inabaki kama minara ya kumbukumbu ya Magufuli nchini kote!

Ukianzia na Ikulu mpya ya Dodoma,ambapo kimsingi pia ndipo mlipokuwa mkienda kukutana na Rais Samia,hadi mlipopata muafaka wenu.

Viongozi wenu wote wa kitaifa na kimajimbo,wanasafiri na kutumia miradi iliyobakia kama nembo ya Magufuli.

Mfano ni Daraja la Tanzanite hapo Dsm.
Magufuli terminal Mbezi.
Flyover zote kubwa hapo Dsm.
Njia nne za kimara kutoka nje ya jiji.
Mradi wa SGR Dar - Tabora.
Mradi wa SGR Tabora- Mwanza.
Mradi wa SGR Tabora - Kigoma.
Mradi wa SGR Mwanza-Isaka.

Ujenzi meli kubwa MV hapa kazi ziwa victoria.
Ununuzi wa Ndege za ATCL.
Ununuzi wa helikopta za kijeshi.
Ununuzi wa ndege za jeshi.

Ujenzi wa masoko mapya ya kisasa Mwanza.

Ujenzi wa mradi mkubwa wa bwawa la kuzalisha Umeme Rufiji. JNHP au Stieglers gorge.

Ujenzi wa stendi kubwa za mabasi Dodoma,Morogoro na Mwanza.

Kufukuza vyeti fake toka utumishi wa Umma!

Kuiheshimisha tena CCM iliyokuwa imechokwa na wananchi kipindi hicho.
...kama inavyoanza tena kwa kasi sasa hivi.

Kuanzisha mfumo wa malipo ya serikali,kwa elektronic nchi nzima G-epay!

Hiyo yote ni Minara ya kumbukumbu za Magufuli!

Mkitaka kuibomoa Legacy ya Magufuli,muanze kwanza kuibomoa hiyo na kuifuta toka kwenye uso wa Dunia.

Pia muelewe wafuasi wa Magufuli wapo kila kona ya nchi,wao hawana makali kwa sasa!
Wanashuhudia na kusubiri muda wao uwadie kuwaamgusha kwa pua,kila aliyemtukana mpendwa wao.
2025 sio mbali.
FB_IMG_1675682846039.jpg
FB_IMG_1675682848567.jpg
IMG-20220829-WA0016.jpg


Hao watu wote waliokuwa wakilia mitaani na mabarabarani, msidhani nao wamekufa!

Wako waliokufa ila wako wengi bado hai.
Na bado wanamuheshimu Magufuli mpaka sasa.
 
MAGUFULI LAZIMA ASEMWE TU Wananchi lazima Waujue Ukatili na wizi wake
Kusema sema bila evidence hakuna msaada,na pia wananchi wanauelewa ukweli.

Wananchi wanajua kilichotokea!
Wananchi wanawajua wahusika wote.
Na wahusika wajue kuwa wanajulikana,kukimbilia kuhiji Mecca
Hakuufuti ukweli wa kilichotokea!

Muda utaongea pale tu majira yatakapowadia.
 
Una uhakika, sogelea pembeni usikilize wanavyoitikia mikutanoni ndio ujue yule kisemwa watu wanazibua masikio
 
Wewe unayejaza nyuzi za kusifia sifia ndiyo njaa itakuua kwani sasa hivi mpini wameshika Msoga Gang nyie Sukuma Gang linawawakia sisi tumeshazoea ku hustle. Na mtaliwa sana mjini hapa
Una hustle kwa kugombana na kaburi?
Basi nyingi hamna tofauti na wachawi.
 
Watanzania lazima tukubali ukwel pia mtu kusema maumiv na mateso aliyopitia sio kusimanga bali ndio ukwel halisi!! Cdhan kama kuna chama cha siasa kinajijenga kwa kumsema mtu vby!!!
 
Ina maana bado hamjamaliza msiba?
Toka zilipovuja taarifa kuwa kuna mzigo wa plea bargain umefichwa huko China na Canada wanalia lia sana ili ndugu wa marehemu wawakumbuke kwenye mirathi. Sukuma Gang njaa inawakaanga kwelikweli.
 
Kosa la Jesca ni lipi hadi umuingize katika ugomvi wenu?
Alikuwa kiongozi au alihusika katika baya lolote la mzazi wake?
Alichagua kuzaliwa toka kwa mzazi wake unaye mchukia?
Alikuja kuanzisha mada hii iliyo kukera?

Busara zako ziko wapi katika hili ulilofanya hapa?
Kwa Chadema busara iko kwa Mnyika walau 47%....

Hawa wengine visasi 100%

Wengine bangi 100%

Wengine konyagi 100%

Yaani wengine risasi zilienda na akili.....
Yaani wako vululu vululu tupu!
 
Una hustle kwa kugombana na kaburi?
Basi nyingi hamna tofauti na wachawi.
Hatuhangaiki na mfu sisi, naona nyie ndugu wa hiari wa marehemu ndiyo mnabweka bweka saaana hasa baada ya kusikia kuwa kuna mzigo umefichwa huko China ili ndugu wa marehemu wawakumbuke kweye mirathi
 
Huyo magufuli hiyo miradi aliyoijenga ni pesa zake? Au alikuozesha wewe na Jesca ndio akapata hizo pesa?.
Ni miradi aliyoibuni yeye na kuiona kama dira ya maendeleo kitaifa na kimkakati.

Kwa hiyo huo ndio unabaki kuwa uhalisia,ila kwako kilaza inaweza ikakusumbua,maana uko brain washed tupu kichwani umejaza ujinga ujinga!
 
Wewe ni Jesca?
Haijalishi mimi ni nani wewe angalia hoja niliyo leta hapa.
Utafurahi watu wakianza kutukana au kuwahusisha wazazi wako au wanao kwenye mabisano ya kejeli na matusi apa jukwaani?
Wazazi/watoto wako wanahusika vipi na ufanyayo wewe hapa jukwaani?
 
Haijalishi mimi ni nani wewe angalia hoja niliyo leta hapa.
Utafurahi watu wakianza kutukana au kuwahusisha wazazi wako au wanao kwenye mabisano ya kejeli na matusi apa jukwaani?
Wazazi/watoto wako wanahusika vipi na ufanyayo wewe hapa jukwaani?
Fedha za ujenzi zilitokana na kuozeshwa kwa jesca au wewe?
 
Hatuhangaiki na mfu sisi, naona nyie ndugu wa hiari wa marehemu ndiyo mnabweka bweka saaana hasa baada ya kusikia kuwa kuna mzigo umefichwa huko China ili ndugu wa marehemu wawakumbuke kweye mirathi
Suala ni kwamba Chadema ndio mnahangaika na Magufuli!

Wezi wa mali za umma ndio wanahangaika na kaburi.

Vyeti fake kama wewe SAGAI GALGANO ndio mnateseka na mzimu wa jembe Magufuli.

Na hakuna siku mtakuja na facts za ushahidi juu ya hizo tuhuma fake!

Sana sana itakuwa walioko madarakani sasa hivi,ndio wanataka kukwapua hizo fedha.

Halafu wasema zilikimbizwa China.
 
Back
Top Bottom