Kumshika mkono amekuwa mkali balaa

Kumshika mkono amekuwa mkali balaa

apologize

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2015
Posts
709
Reaction score
570
Habari wakuu,

Kuna kitu leo kimenishitua kidogo kuna binti mmoja tuko naye mtaa mmoja na tunaabudu Kanisa moja kuonana kwetu huwa ni kanisani japo tulikuwa tunaangaliana tu hakuna mtu aliyekuwa anaenda kumpa salam mwezake,lakini sura zetu wote zilionesha shauku ya kila mtu kutaka kuongea na mwezake.

Sasa jumapili iliyopita tuliweza kuongozana wote kurudi nyumbani lakini tulikuwa watatu na kila mmoja alifurahi yaani ndo ilikuwa siku ya 1 kuongea naye,pia leo jumapili baada ya ibada tulikuwa tunatakiwa twende kwenye ibada nyingine tofauti na Kanisa letu akaniuliza utaenda nikamjibu ndio nikamuomba anipitie home akakubali.

Kweli badae akapita na tuanza kwenda huku tukioneshara ishara za mapenzi, nikaona nimtongoze akaniambia nimpe wiki mbili ndo atanijbu, sasa cha ajabu wakati tunarudi home nikajaribu kumbembeleza apunguze hizo wiki mbili huku nikijaribu kumshika mkono akawa mkali ghafla akasema hapendwi kushikwa.

Wanajamvi naomba ushauri, maana hapa mwanzo wakati kaja kunipitia tulikaa ziro distance na nilikuwa namshika mkono kawaida.
 
Anakutaka sana huyo ila unajuwa ni shida sana kwa demu kumtongoza siku hiyo hiyo amekwamba bada wiki2 ukaanza kumshika shika anahisi kama unamfanya rahisi sana kuwa na subra naye acha pupa.
 
Kwan ulkuw umepat idhini ya kuwa wake? Tatz una harak nying,
wanawak wengn hawapendag mwanaum mwmy harak km ww,

pengin kakujudge upo after something.
 
Anakutaka sana huyo ila unajuwa ni shida sana kwa demu kumtongoza siku hiyo hiyo amekwamba bada wiki2 ukaanza kumshika shika anahisi kama unamfanya rahisi sana kuwa na subra naye acha pupa.

Shukran ndugu ntafanya hvyo
 
Hiyo ni ishara nzuri. Wewe mlie timing tu. Hata sisi wazee wenu mama zenu walitufanyaga hivyo hivyo siku za mwanzo. Mabinti wengine ndio zao hizo, kwa hiyo usikate tamaa. Shikilia hapo hapo mwisho wa siku atalegeza tu. Komalia hiyo kitu.
 
Hizo nguvu za kumshika mkono zihamishie katika kukishika kichinjio chako vizuri ili oct 25 tumchinje mkoloni wetu mweusi
 
unampango wa kumuoa au ndio hit and run?
 
Hizo nguvu za kumshika mkono zihamishie katika kukishika kichinjio chako vizuri ili oct 25 tumchinje mkoloni wetu mweusi
Hatuishi kwa siasa peke yake. Kila kitu siasa, tumechoka sasa. Hili ni jukwaa la mapenzi, mahusiano na urafiki. Hayo mambo ya vichinjio, sijui mkoloni mweusi, sijui nini peleka jukwaa la siasa.
 
inaonyesha una nyege kweli kweli aiseee sasa inakuaje unamshika shika mkono mdada wa watu bila makubaliano wakati kishakwambia after 2 week atakupa jibu lako la hapana?!
 
Habar wakuu, kuna kitu leo kimenishitua kidogo kuna binti mmoja tuko naye mtaa mmoja na tunaabudu kanisa moja kuonana kwetu huwa ni kanisan japo tulikuwa tunaangaliana tu hakuna mtu aliyekuwa anaenda kumpa salamu mwezake,lakin sura zetu wote zilionesha shauku ya kila mtu kutaka kuongea na mwezake sasa jumapil iliyopita tuliweza kuongozana wote kurud nyumban lakn tulikuwa watatu na kila mmoja alifurah yaan ndo ilikuwa siku ya 1 kuongea naye,pia leo jumapil baad ya ibada tulikuwa tunatakiwa twende kweny ibada nyngne tofauti na kanisa letu akaniulza utaenda nikamjibu ndio nikamuomb anipitie home akakubali, kwel badae akapita na tuanza kwenda huku tukioneshara ishara za mapenzi, nikaona nimtongoze akaniambia nimpe wiki mbil ndo atanijbu, sasa cha ajabu wakat tunarud home nikajarbu kumbembeleza apunguze hzo wiki mbil huku nikijarbu kumshka mkono akawa mkali ghafla akasema hapendwi kushikwa,wanajamvi naomb ushaur, maan hap mwanzo wakat kaja kunipitia tulikaa ziro distance na nilikuwa namshika mkono kawaida.

Atakuwa ni Apologise lady nini?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom