Elections 2010 Kumradhi: Bado niponipo

katika Thread ya CHADEMA kuchuka Kilombero, nimemtumkana Bado niponipo. Naomba Uniwie Radhi maana nilihamanika kwa Sababu toka jana kuna Members ambao kazi yao ni kuleta habari ambazo hata wenyewe wanajua ni za Uongo kitu ambacho kinaweza kupelekea kushusha hadhi ya Jamvi letu

Nachukua nafasi hii, mbele ya Hadhira hii Kumuomba radhi member bado nipo nipo na wengi wote niliowakwaza

Asante


Kaka hope muhusika atakusamehe maana mimi nilikuwa napata wasiwasi na huu u Dr. wako labda nao ni wa KUTUNIKIWA kama viongozi fulanifulani!
 
Ndo utuuzima mkuu, I like umekuwa sincere, u still have morals which most lack
 
Hadhi aipandi kwa kwa kutukana watu. Mtu mwenye hekima anaweza kujirekebisha kama approach yako ni nzuri. Ni ile hadithi ya Mzee ruksa, chizi akichukua nguo yako nawe ukamkimbiza barabarani ukiwa uchi basi watu watajua wewe ndiyo chizi. Kwamba ni premium member haiwezi kuwa chanzo cha jeuri ya kutukana watu hovyo hovyo! Nilifikiri ulinitukana kwa sababu out emotion nilileta habari isiyo kweli leo nilipoona unaendeleza nikajua wewe ni mtu wa aina gani hata kama umemwomba samahani


Isingekuwa busara zake za kuomba radhi, hii thread isingekuwepo hapa na wewe usingepata nafasi ya kuandika comments zako.Ikumbukwe kuwa yeye si wa kwanza ku mkwaza mtu humu JF.Tuondoe boriti kwenye macho yetu ndipo tutakapoweza kuona kibanzi ktk macho ya wenzetu.Upendo daima mbele kwa mustakabali bora wa familia yetu(JF).
 
Tumepata nafasi ya kuongea yote haya kwa sababu ya hekima na busara zake Dr.NU kujitokeza na kuomba radhi.Kwa kitendo hiki tu anastahili pongezi. Tunapo mpongeza mwenzetu na sisi tutathmini kauli zetu kwa kiasi gani zinaweza/zimeweza kuwa kwazo kwa wengine.Kwani humu JF kumejawa na malaika watakatifu wasio kwaza wenzao?Kwani Dr.NU kutumia lugha ya kukwaza ni wa kwanza humu JF?Je, ni wangapi tuliojitokeza kuombana misamaha kama alivyofanya Dr.NU?
Tutafakari.....Tuchukue hatua
 
Back
Top Bottom