Kumpoteza Mama

Kumpoteza Mama

Mwaka 2015 ilikua mgumu sana kwangu kwa sababu ndio nilimpoteza bi mkubwa. Ilikua ni kipindi kigumu sana kwangu kwa sababu by the time nilikua chuo halafu ilikua kipindi cha field. Yale mazingira ya nyumbani hasa baada ya msiba yalikua yananitesa sana nilikua nashindwa kuvumilia nikimuona mzee anatoka chumbani anakaa sebleni peke yake. Ila kiukweli nachoshukuru mzee alionyesha ukomavu mkubwa sana tulivuka salama mpaka leo hii. Mambo mengi mengi yalitokea hapa katikati yaliyonifanya nizidi kukua kifikra sana hasa kila napokumbuka mapenzi na mafunzo ya mama kwetu sisi.

R.I.P mama
 
poleni sana jamani kupoteza mama...nimeumia...siwezi vaa viatu vyenu...Mwenyezi Mungu anilindie Mama na Baba yangu😭
 
Dah inatia uchungu mno, mama yangu alienda mapema sana nakumbuka nilikuwa youngster kichizi.

It was really unfair to me sababu pia sikuishi nae mda mrefu nakumbuka ilikuwa ni baada ya mid term ya std 3 tu. Ile likizo imekwisha tu nashangaa naambiwa jiandae na safari ya Dar usiende shule. Nafika mtaani dah nakuta watu kibao huku na huku mara bi mkubwa huyu hapa kwenye jeneza.

Moyo ulikufa ganzi mno kwa uchungu niliokuwa nao sikuweza hata kulia siku ile ila ndio siku ambayo niliona machozi ya mshua alililia sana. Tangu siku ile nilijua maisha yangu hayataweza kuwa sawa tena katika hii dunia baada ya kuona ndugu zangu wakubwa wakihuzunika na kulia kwa uchungu, mimi pekee ndio nilikuwa mziwanda kwa mama na hadi leo namkumbuka kwa upendo mkubwa aliokuwa akinionesha pamoja na ucheshi wake. Rest in Peace my mother siku moja naamini ntakuja kukuona tena.

Uchungu haukuishia hapo baada ya week mbili za kumzika mama nilimpoteza kaka yangu mwengine ambaye nae alikuwa ni kipenzi changu sana pamoja na mama yangu. Naamini alimfuata rafiki yake mama maana asingeweza kuishi bila yeye. Rip my lovely brother Yusuph alias "Makamba" maana alikufa kipindi mzee makamba akiwa ni mkuu wa mkoa wa Dar.

Mwaka 2001 utabaki kuwa na historia chungu sana kwenye maisha yangu yote hapa duniani. Uliondoka na ndugu wengi sana ninaowapenda kama pia ilivyotokea 2021.
Pole sana., inauma.
 
Hivi wewe msimbe umerogwa?

Huu uzi umekutanisha watu wamepoteza wazazi tuko kufarijiana na kukumbushana kuwakumbuka wazazi wetu wakiwa hai wewe unaleta habari za ******* namna hii

Hebu jiheshimu
Jibu swali nililouliza.

Wacha kufafuta huruma za kijinga.
 
Wengine wanatamba humu wao wachawi. Wao wenyewe wale nyama za mama zào halafu wajidai eti wana majonzi.

Wacheni unafik.
 
Dah inatia uchungu mno, mama yangu alienda mapema sana nakumbuka nilikuwa youngster kichizi.

It was really unfair to me sababu pia sikuishi nae mda mrefu nakumbuka ilikuwa ni baada ya mid term ya std 3 tu. Ile likizo imekwisha tu nashangaa naambiwa jiandae na safari ya Dar usiende shule. Nafika mtaani dah nakuta watu kibao huku na huku mara bi mkubwa huyu hapa kwenye jeneza.

Moyo ulikufa ganzi mno kwa uchungu niliokuwa nao sikuweza hata kulia siku ile ila ndio siku ambayo niliona machozi ya mshua alililia sana. Tangu siku ile nilijua maisha yangu hayataweza kuwa sawa tena katika hii dunia baada ya kuona ndugu zangu wakubwa wakihuzunika na kulia kwa uchungu, mimi pekee ndio nilikuwa mziwanda kwa mama na hadi leo namkumbuka kwa upendo mkubwa aliokuwa akinionesha pamoja na ucheshi wake. Rest in Peace my mother siku moja naamini ntakuja kukuona tena.

Uchungu haukuishia hapo baada ya week mbili za kumzika mama nilimpoteza kaka yangu mwengine ambaye nae alikuwa ni kipenzi changu sana pamoja na mama yangu. Naamini alimfuata rafiki yake mama maana asingeweza kuishi bila yeye. Rip my lovely brother Yusuph alias "Makamba" maana alikufa kipindi mzee makamba akiwa ni mkuu wa mkoa wa Dar.

Mwaka 2001 utabaki kuwa na historia chungu sana kwenye maisha yangu yote hapa duniani. Uliondoka na ndugu wengi sana ninaowapenda kama pia ilivyotokea 2021.
Pole sana mkuu
 
Basi ukiwa na mama yako duniani unaweza pita huu uzi.
Poleni mliopoteza Mama zenu. Acha tuwawakilishe kwa hawa mama tuliobaki nao.
3114bbe8ff4c9d93b15e0da572deda3d.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Kuna kitu kuhusu kumpoteza mama ambacho ni cha kudumu na kisichoelezeka - kidonda ambacho hakiwezi kupona milele."
 
Back
Top Bottom