Kumpiga mwanamke ni jambo la kijinga sana

Kumpiga mwanamke ni jambo la kijinga sana

Huo ndio ukichwa sasa

Wanawake wanahitaji sana kulindwa KIUCHUMI, KIHISIA, KIMWILI na KIROHO na waume zao

Kabla ya kupata mchumba ni jambo la asili mwanamke kutaka kujua mchumba wake kama ataweza kumtunza.

Hatupaswi kushangaa kuona manzi anataka kujua kazi au unajishughulisha na nini kabla ya kumchumbia na kumuoa. Wanataka kujihakikishia ulinzi wa kiuchumi.

Fanya kazi kwa bidii mtunze mpatie mahitaji muhimu maishani mkeo utakuwa umemlinda KIUCHUMI

Mke mshauri kwa upendo na kirafiki hata kama amekosea, akiwa na stress mume unatakiwa umliwaze, mke hatukanwi wala kutupiwa maneno machafu au kudhalishwa, mhakikishie unampenda kwa maneno na matendo hapo utamlinda KIHISIA

Mke hapigwi wala kufanyishwa makazi magumu kisa tu ni msaidizi, mke anapaswa kulindwa dhidi ya maadui wowote pale nyumbani kwako, ikiwezekana mume awe tayari kufa kwa ajili ya mkewe hapo atamlinda mke KIMWILI

Usisahau kumwongoza kwenye ibada ili umjenge KIROHO
Wewe una safari ndefu sana ya kujua maisha. Wewe beta male. Yani Wale wanaume mabwege.
 
Mwanaume mwenzangu ikiwa una suala tata na mkeo - haijalishi ni mwiba jinsi gani - lijadili naye na kulimaliza kwa amani. Usifanye ujinga wa kumpa kichapo.

Kwa kawaida sisi binadamu uwezo wetu wa kuwasiliana ndio unaotutofautisha na wanyama - lakini kitu kingine ndani ya binadamu kinaweza kupatikana katika wanyama kama vile paka, mbwa au farasi.

Mapigano ya kimwili, kuitana majina na kufedheheshana - iwe nyumbani au kati ya mataifa - hutupunguza kuwa mamalia tu. Sisi ni viumbe wenye akili na uwezo wa kutatua masuala.

Haijalishi unajisikia vibaya kiasi gani kuhusu mke wako, kamwe usifanye ukatili wa nyumbani kwa kumpa kipigo.

Una chaguo mikononi mwako - ikiwa ni pamoja na kukubaliana kwa amani na kuachana kwa ustaarabu.

Kwa kawaida ni ukosefu wa usalama wa ndani ndio husababisha mtu kushambulia mtu mwingine.

Wanaume wenye utulivu wa kihisia huheshimu maoni ya watu wengine bila ulazima wa kukubaliana nao.

Leo hii kuna wanaume wenzetu wapo gerezani kisa walipiga wake zao! Naweza kuwaita ni wanaume waliochagua kuwa wajinga.

Yakobo 1:19 - Ndugu zangu wapenzi, kumbukeni jambo hili: Kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, si mwepesi wa kusema na si mwepesi wa kukasirika.

Ubarikiwe
Hayana formula usilazimishe formula na utashi wako kuapply kwa wengine, kumzaba makofi mbili tatu mke anapozingua wakati mwingine inamrejesha ufahamu,.... Halafu inaonekana unamkeraga sana mkeo kwa ujuaji wako .... MUNGU mwenyewe tukizingua anatutandika na miadhabu kibao tupate akili,sembuse we mchambia tishu

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Kuna muda wanakera, sipendi kufanya hivyo japo akikukera sana vibao viwili vitatu sio mbaya
 
[emoji134][emoji134] Wewe usijaribu, mimi nataka kupigwa na ulichokifunga na zipu tu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] vibao viwili tu huwezi vumilia? Viwili tu
Si unajua sometimes mnakua na mdomo sana
 
Sisi huku Kwetu Musoma taratibu zetu
Mwanamke asipopigwa lazima ajisikie vibaya saaana
Ataona humpendi hata kidogo yani unamdharau vibaya mno .
Hivo lazima mwanamke tu mwanamke apigwe ili ajisikie kuwa anapendwa na una wivu nae kutoka moyoni
Hata hao wa makabila hufarahia sana vipigo pindi wakiolewa huku hasa Mabinti wakichaga na Singida... Maaaninerrr
 
Hii mada itakuwa imeandikwa na motivation speaker bila shaka ,zakuambiwa changanya na zako
 
Back
Top Bottom