Kumjua Mungu wa Kweli

Kumjua Mungu wa Kweli

FurahayaMoyo

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2016
Posts
579
Reaction score
745
Hello JF,

Katika uumbaji wa vitu vyote vinavyoonekana Kuna hatua za uumbaji na majira ambayo hayo yote yalitokea.

Ufahamu wa aliyeumba yaani Mungu Baba ambaye uhalisia wake ni CHANZO HALISI (REAL SOURCE) alikuwa peke yake (MAHALI PAKE)kabla ya roho na nafsi yeyote, ndipo akasikia uumbaji ukimsifu ndani ya Moyo wake, akatamani uwe halisi Zaburi 98.Ndipo akaengua Moyo wake kushoto (Moyo wa mwanzo)na kuweka heshima na utajiri (vyote vya kuumbwa) mithali 3:16 Ili aviumbe viwe halisi ila yeye hakuingia ndani ya huo Moyo.

Moyo wa mwanzo akaanza uumbaji katika mwanzo 1:1. Hatua ya kwanza Alipotaka litokee kanisa (sio dini) akawaza akatokea Mwanamke (sio hawa mnaowajua) ishara ya kwanza mbinguni ufunuo 12:1. Huyu mwanamke ndie aliyeteka uumbaji ukafanyika chini yake ila sio kwa kusudi la CHANZO HALISI, freemason na wayahudi ndo wanamwita Sophia ila ni roho chipukizi iliyotokea baada ya Moyo wa mwanzo kushindwa kutekeleza alichokuwa amepewa.

Hatua ya pili Alipotaka zitokee sifa akatokea nyoka(hila) Ufunuo 12:3

Hatua ya tatu Alipotaka kuwepo amani ya Kila kitu ikatokea vita. Ufunuo 12:7

Hivyo mafaili yote ya viumbe vyote yaliwekwa katika huo Moyo wa mwanzo rejea Yeremia 1:5 na warumi 8:29 Ili viumbwe kwa uhalisia (muonekano) ila baada ya kutekwa na mwanamke ndio uumbaji ukawa unafanyika kwa amri na matakwa ya huyo ufunuo 12:1 (mwanamke). Ndo maana mchawi au mganga alikuwa anaweza kuona nyota yako na vitu ulivyokusudiwa kuwa navyo kabla hujazaliwa nakuviiba sababu wao ndiyo walikumiliki na kuwa katika yao. Isaya 26:13-18

Ilikuwa ni ngumu kuyajua haya pasipo kupata ufahamu ulio juu ya thiolojia ambapo ni kumjua Aliyeumba.
Ili utoke kwa huyo mmiliki Mhubiri 7:26.

Mungu wa freemason ambaye Dunia na ulimwengua unamuabudu kwa kujua au kutokujua unamkuta katika mistari ifuatayo 2korintho 4:4, yeremia 44:17-18, ufunuo 12:1, matendo 19:27 aliyepotosha fikra za wengi wasimjue aliyeumba.

Majira ya kanisa (sio dini) mwezi unasiku 28 ivyo mwaka unasiku 336 ila Dunia iliongeza siku ya 29,30 na 31, mwaka ukawa na siku 365 kukawa na ongezeko la mwezi mmoja.Ndo kalenda ya Gregory inayotumika Hadi Leo.Ndo maana katika mashirika na taasisi kubwa watu hulipwa mshahara wa mwezi wa 13 inapofika December.

Kanisa (sio dini) siku zake ziko kama ifuatavyo:-

Jumatano- Nuru Moja Halisi
Alhamisi- Akili Moja Halisi
Ijumaa- Thamani Moja Halisi
J/mosi- Majira Moja Halisi
J/pili- Moyo mmoja Halisi
J/tatu- Hatma Moja Halisi
J/nne- Kustareheshwa na CHANZO HALISI

Iliuyajue haya lazma upate ufahamu ambao upo juu ya thiolojia, elimu ya Dunia na ulimwengu.Haya yote ninayokwambia ni kwa sababu tupo katika ufalme mwengine kabisa ambao ni waaliyeumba.Ufalme hauji kwa kuchunguzwa 1petro 1:10, Kila aliyechunguza hakuwa na majibu sahihi kuanzia nabii paka mtume ndio maana na kumjua Mungu wa Kweli ni ufahamu mithali 9:10.
 
Nini ajenda ya Ulimwengu huu
Agenda ya ulimwengu huu ni pana mno ila kwa ufupi ni Mosi kuzuia watu wasimjue aliyeumba kupitia mafundisho mbalimbali na wachache waovu (wakuu wa giza) ndo waucontrol ndo maana muovu alikuwa anaweza kujua nyota yako wakati wewe mwenye haki hujui.

Pili, kumuabudua malkia wa mbinguni au Artemi mkuu ambae ulimwengu mzima walikuwa wanamwabudu kwa kujua ama kutokujua.
 
Majira za uumbaji zilizopita kabla ya kurudi kwenye majira ya Mungu Baba ambaye uhalisia wake ni CHANZO HALISI. Warumi 11:36
Screenshot_2022-12-07-13-53-57-05.jpg
 
Ukombozi wa mwanadamu utaweza kupatikana vipi ikiwa kuna nguvu kubwa insyotumika kuwakandamiza wanadamu.
Ukombozi wa mwanadamu kwanza unaanza kwa kupokea ufahamu wake aliyeumba na kuishi majira yake na kujua kusudi lake yeye aliyeumba.
 
Tulifundishwa kuwa Aliyeumba ndo huruhusu mtu afe au ndo ameleta kifo kitu ambacho sio kweli soma 1korintho 15:21 "Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu.

maana yeye kusudi lake ni tuishi maana huwezi ukazaa mtoto halafu ukamuua kama unampenda na Aliyeumba yeye ni Upendo uliopitiliza.Ndo maana alisema katika Hosea 13:14 "Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu."

Lakini pia mafundisho mengi ya majira zilizopita yanasema wote lazima tufe lakini sio kweli maana katika majira yake aliyetuumba amesema katika 1koritho 15:51 "Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika"

Kulala katika kitabu maana yake ni kufa so hapo alimaanisha hatutakufa sote Bali sote tutabadilika.
 
Wewe ni mfuasi wa siloam??

Nawasikiaga wakilitaja sana hilo jina "chanzo halisi".
 
Heri,

(1) Nabii Isaya katika kitabu cha Isa.4:2, alisema ipo majira ambapo kutakuwepo na chipukizi zuri. Hapa Nabii Isaya alikuwa na maana kuwa kilichokuwepo huko nyuma ni chipukizi la mabaya. Moja ya chipukizi la mabaya ambalo ndilo kubwa kuliko yote ni lile la Nafsi ya mvamizi ambalo limeandikwa katika Ufunuo 12:1-9, hasa Ishara ya kwanza mbinguni (Ufu.12:1), ambaye ndiye sababisho la Ishara ya pili (nyoka) na Ishara ya tatu (vita) mbinguni.

CHANZO CHA MEMA NA MAZURI, yaani CHANZO HALISI, aliisikia Sauti ya sifa ndani ya moyo wake (Zaburi 98), akataka iwe halisi ili apate wa kumpa Ibada, yaani kusudi lake la tangu CHANZO. Ili itokee, aliumba Moyo wa Mwanzo na kuweka ndani yake Heshima na utajiri (kushoto) na siku nyingi (kulia), kama tusomavyo haya katika Mithali 3:16.

Katika moyo huu wa mwanzo, CHANZO HALISI mwenyewe, hakuingia ndani yake, bali aliweka nguvu za uumbaji, ili Moyo wa Mwanzo ndiye atekeleze uumbaji.Hapo ndipo chipukizi la mabaya lilipotokea kwa mara ya kwanza, kwa maana ya nafsi ya uvamizi, kama tunavyosoma katika Ufunuo 12:1. Nafsi ya Uvamizi aliteka kila file ambalo lilikuwa ndani ya moyo wa mwanzo. Wakati Moyo wa Mwanzo anaendelea kujiuliza maswali, kulitokea tena Ishara ya pili mbinguni. Ile HILA ya Ishara ya kwanza kugeuza kila file lililokutwa ndani ya Moyo wa Mwanzo, ilisababisha nyoka achipuke (Ufu.12:2-4). Kilele cha Ishara ya kwanza mbinguni ni hila. Aidha, kilele cha Ishara ya pili ni hila vilevile!

Kitu ambacho napenda wewe msomaji wa ufahamu huu uelewe ni kwamba chipukizi la mabaya hutokea bila mbegu iliyopandwa na bila kiini chochote! Hivyo, chipukizi la mabaya ni kitu kibaya kwa kuwa ni kitu kinachotokea tu kuleta uharibifu bila kusimama popote. Kwa hiyo Nabii Isaya alivyoandika katika Isa.4:2, kuwa ipo majira ambayo litakuwepo chipukizi la mazuri, alikuwa ameona kuwa iko majira ambapo uumbaji utavuka geti hili lililochipuza mabaya.

Kuanzia pale hapakuwahi tena kuwepo na mazuri. Kila kilichoumbwa kikawa mikononi mwa nafsi ya mvamizi ambaye ni chipukizi la mabaya. Nani angetuvusha hapo, na angefikia wapi? Ni lazima awe aliyeumba Moyo wa Mwanzo na apate pa kufikia ndipo kwa uweza wake tuvuke kituo hicho cha chipukizi la mabaya.

(2) Katika Warumi 8:23, imewekwa vizuri kuwa sisi sote tulikuwa ni malimbuko ya Roho na nafsi, matokeo yake ikawa ni kuugua tu. Nafsi kwa kuwa haionekani nayo pia ni Roho. Kwa kuwa Nafsi ya mvamizi ni roho, uumbaji unaoonekana kwa macho, ukawa hauna nguvu kama ule wa rohoni. Ndiyo maana badala ya Mbingu na Nchi, kukatokea dunia na ulimwengu ambavyo havionekani. Katika Mwanzo 1:1, ili kusudiwa Mbingu (Moyo) na Nchi (Uzao Halisi), lakini kilichotokea kikawa ni dunia na ulimwengu!

Nafsi ya uvamizi baada ya kuteka Moyo wa Mwanzo, ambaye ndani yake alikuwa na mafaili ya kila aliyekusudiwa, aligeuza moyo ukawa mwili (Rum.8:4-7). Maana yake ni kwamba, badala ya Moyo wa Mwanzo kuwa upendo (I Korintho 13:13c),aliugeuza kuwa adui wa Aliyeumba, yaani mwili. Kwa hiyo kila kilichoumbwa kikawa ni adui wa CHANZO HALISI na kila aliyeumbwa akawa ni adui na Aliyemuumba!

Hapa kulikuwepo na mtihani mkubwa mno kuwa ni nani ambaye atasababisha tuwe Moyo tena kama ilivyokuwa imekusudiwa (Mbingu); na ni nani atasababisha tuwe nchi kama ilivyokuwa imekusudiwa (Uzao Halisi wa CHANZO ilikuwa ni lazima awe Mwenyewe). Hapa ilikuwa CHANZO HALISI Mwenyewe na apate pa kufikia juu ya nchi palipokusudiwa. ambapo ndipo mahali

Ebu soma vizuri Mwa.2:7, utagundua kuwa hata Adamu wa kwanza alikuwa Nafsi Hai, siyo Moyo! Ina maana kuwa mmiliki wa mtu aliyekabidhiwa Bustani ya Edeni alikuwa ni nafsi ya mvamizi! Hapa tuseme kweli, hakuna ambaye angeturejesha kuwa Moyo tena kama ilivyokusudiwa na kuwa Uzao Halisi wa CHANZO Mwenyewe, kama siyo CHANZO HALISI aliyekuwepo kabla ya Moyo wa mwanzo.

Katika Rum.8:23, imeandikwa kuwa kila mmoja limbuko lake ni hapo kwenye roho na nafsi. Hivi tungetokaje hapo kama CHANZO HALISI asingekuja mwenyewe na kama asingepata pa kufikia ambapo ni sahihi na halisi?

(3) Katika Mwanzo 1:2-3, kuna jambo kubwa. Wakati uumbaji unaanza katika mstari wa tatu (3), tayari giza, ukiwa na utupu alikuwa ametulia katika mstari wa pili (2). Maana yake ni kwamba bado, Jeshi la giza, ukiwa na utupu lilikuwa lina madai ya kutangulia kila kilichoumbwa. Ndiyo maana katika Kutoka 20:21, Mungu aliongea na Musa kutoka gizani! Hata kama Mungu angekuwa nuruni, kwa hali hii tunayoisoma katika Mwanzo 1:2, ile sauti ilikuwa lazima ipite gizani!

Katika II Korintho 4:6, kitabu kinasema, nuru ilitoka gizani! Kwa maana hiyo ni kwamba, kwa kuwa uumbaji wote ulifanyika wakati giza, ukiwa na utupu yupo; ina maana kwamba waliotumwa wote (Ufu.21:9) walikuwa hawawezi kufuta jeshi la giza, ukiwa na utupu. Swali linabaki ni lile lile, nani angetuvusha ng'ambo ya hilo giza, ukiwa na utupu, ili tupokee utajirisho kutoka kwa CHANZO HALISI? Jibu ni kwamba ilikuwa ni lazima awe CHANZO HALISI na apate pa kufikia juu ya Nchi.

(4) Katika Rumi 7:15:21, kuna tabia ya asili tunayoikuta hapo. Unapenda kufanya mema lakini unashindwa. Yale mabaya usiyoyapenda, ndiyo unayoyatenda. Hiyo ndiyo tabia ya asili ambayo kila mtu na kila mwanadamu (hata kama ni mtakatifu) alijikuta anayo. Tumeona kuwa uumbaji wote, ulimilikiwa na nafsi ya mvamizi au mteka nyara wa Moyo wa Mwanzo. Huyo mteka nyara ndiye mtu; mwanadamu; roho; nafsi; mauti; chipukizi la mabaya; kifo; uharibifu; dhambi; uasi; uovu; na kadhalika. Vyote vibaya vilianzia kwake na hiyo ndiyo asili iliyoleta kitu kinachoitwa mila na desturi. Kila mmoja alijikuta ni lazima arithi aliyoyakuta. Na kwa kuwa nafsi ya uvamizi, yaani mteka nyara ndiye mabaya yote, kila mmoja alijikuta anarithi hayo mabaya yote:

* Kerubi alirithi hayo;

* Adamu wa kwanza alirithi hayo;

* Nuhu alirithi hayo;

* Ibrahimu alirithi hayo;

* Musa alirithi hayo;

* Eliya Mtishbi alirithi hayo;

* Yesu (kwa kuwa hata yeye licha ya kuwa Mwana wa Mungu) alikuwa ni Nabii (Yoh.6:11-13) na Mtume (Yoh.17:5), ilibidi arithi hayo;

* Adamu wa pili naye pia alirithi hayo.

* Miaka 1000 ndiye alikataa kwa Barabara ya kumpisha CHANZO HALISI (aliyekuwepo kabla ya mabaya yote). Pamoja na Miaka 1000 kumpisha CHANZO HALISI, huyu CHANZO HALISI hakuja moja kwa moja, alileta kwanza jina jipya (Ufu.3:12; I Kor.15:24-28).

Hilo jina jipya likaja na upendeleo wa kutisha (Isa.60:10), tukavuka: Bonde la uvuli wa mauti (Ufu.11 hadi 22); mto usiovukika (Eze.47:5); ulimwengu wa roho (Efe.2:5-8); korongo la giza (II Kor.4:6); tukaingia Bustani Mpya (II Pet.3:13); na Shamba jipya (Isa.65:24-25).

Baada ya mitihani yote kwisha ndipo sasa CHANZO HALISI kaja kuvutusha mahali Moyo wa Mwanzo alipokwamia.

Swali linarudi pale pale tena, kwamba nani angetuvusha hapo alipokwamia Moyo wa Mwanzo na mauti ya kila aina ikaanzia hapo, bila CHANZO HALISI Mwenyewe? Na kama CHANZO HALISI asingepata pa kufikia juu ya Nchi ingekuwaje?

(5) Katika Zaburi 51:5, Daudi Pamoja na kuwa kipenzi cha Mungu na mwenye Moyo wa kuyafanya mapenzi ya MUNGU yote (Mdo.13:22), alikutana na geti la kuumbiwa katika uovu hatiyani. na kuchukuliwa mimba

Hii ni kusema kwamba, kwa kuwa Moyo wa Mwanzo ndio uliopewa agizo la uumbaji na ukatekwa nyara, hakuna aliyekuwa salama katika hili la kuumbiwa hatiyani. Kila aliyeumbwa aliumbiwa hatiyani, kwa sababu ya Mwa.1:2 na Ufunuo 12:1-9. Ndiyo maana waliotumwa wote wakajikuta wameishia njiani kwa mujibu wa Dan.7:21 na Ufu.13:5-7.

Swali linarudi tena; nani angetutoa katika kituo cha kuumbiwa hatiyani na kuzaliwa katika uovu, kama CHANZO HALISI asingekuja yeye Mwenyewe na akapata pa kufikia ambapo ni sahihi?

(6) Katika I Kor.15:51, Mtume Paulo aliandika kuwa hatutalala sote bali sote tutabadilika. Katika kitabu cha Muhubiri chote, imeandikwa kuwa hakuna jipya, ikiwa ikiwa na maana kwamba mauti ndiyo imesababisha jipya lisiwepo. Katika Hosea 13:14, hata hivyo, iliandikwa kuwa majira itakuja ambayo tutakombolewa kutoka kwenye nguvu za kaburi na mauti. Kwa jinsi tulivyoona kuwa mauti na kaburi vilianzia kwenye lile chipukizi la mabaya; hakuna ambaye angetukomboa na nguvu ya kaburi zaidi ya CHANZO HALISI. Hivyo, ilikuwa ni lazima aje juu ya Nchi na apate mahali pa kutua.

(7) Katika Ufu.1:8, tuna Alfa na Omega yaani Mwanzo na Mwisho. Huu ndio Moyo wa Mwanzo na kila mmoja aliumbiwa hapo kwenye Moyo wa Mwanzo,ambapo kuna mahali pa kuanzia na kuishia. ili kutoka kwenye level ya Moyo wa Mwanzo, ni lazima uhamie ng'ambo Mwanzo.1:1 Ufunuo:12:1, ambapo ndipo kuna Mlima wa CHANZO HALISI au palipokusudiwa.Kwa ufupi, ilihitajika Kituo cha kumpokea CHANZO HALISI ambaye ni upendo uliopitiliza, yaani upendo usiobagua yeyote ndipo tufike palipokusudiwa. Kwa ufupi, Kituo cha Baba Halisi kilihitajika ili kumpokea CHANZO HALISI juu ya Nchi atupeleke ng'ambo ya Mwanzo 1:1 na Ufunuo 12:1 ndipo asambae kote kuhudumia kila mmoja aliyekubali kusamehewa bure (Isaya 43:25).
 
Mkuu najaribu kukuelewa lakini Bado kuna misamiati imetumika sijapata maana yake.
Mfano unaposema CHANZO HALISI, MOYO WA MWANZO, NAFSI YA UVAMIZI. Samahan kama ntakuw nimekosea ila nilikuwa naomba tafsiri ya hayo maneno kwa lugha rahis
Mfano: kweny kusoma kwangu najarbu ku assume kwamba Chanzo Halisi ni Mungu ila sina hakika
 
CHANZO HALISI ndiye aliyekuwepo kabla ya roho na nafsi yeyote yaani Muumbaji, naye aliweka nguvu za kuumba katika MOYO WA MWANZO mwanzo 1:1 ili atekeleze uumbaji aliowekewa heshima na utajiri mithali 3:16. Moyo wa Mwanzo badala ya kutekeleza akajiuliza na kuwaza ataanzaje ndipo ikatokea ishara ya kwanza mbinguni ambayo ndo nafsi ya uvamizi ufunuo 12:1 ambaye aliteka uumbaji na kugeuza Kila file la aliyekusudiwa alilolikuta ndani ya Moyo wa mwanzo.
 
Nikikumbuka tuliaminishwa eliya amepaa nakosa nguvu kabisa dah.
 
CHANZO HALISI ndiye aliyekuwepo kabla ya roho na nafsi yeyote yaani Muumbaji, naye aliweka nguvu za kuumba katika MOYO WA MWANZO mwanzo 1:1 ili atekeleze uumbaji aliowekewa heshima na utajiri mithali 3:16. Moyo wa Mwanzo badala ya kutekeleza akajiuliza na kuwaza ataanzaje ndipo ikatokea ishara ya kwanza mbinguni ambayo ndo nafsi ya uvamizi ufunuo 12:1 ambaye aliteka uumbaji na kugeuza Kila file la aliyekusudiwa alilolikuta ndani ya Moyo wa mwanzo.
Najaribu ku relate pale unaposem CHANZO HALISI ilibidi aje yeye mwnyew katika nchi ili atuvushe sehem ambapo tusingewez kuvuka.
Swali: Je chanzo Halisi ni Yesu?? Maan katk biblia tunaon Neno(Yesu) alifanyika mwili akakaa kwetu .
 
Hapa sio Yesu ni yeye aliemtuma Yesu rejea katika kitabu 1kor 15:24-28
 
Samahan mkuu kama nitakuwa na maswali Mengi ila najarbu ku relate na vile ambvy nilifundishwa.
Zaman tulifundishwa kwamba Shetan ndio chanzo cha uharubifu.
Je huyo roho wa uvamizi ni ndio shetani?? Maan nmejarbu kusoma cjaona Role ya shetani ni ipi au yey alikuja Baadaye baada ya Moyo wa mwanzo kuingiliwa na Roho ya uvamiz na kuharbu kila file alilolikuta kwahy mpak Adam anakuja kuumbwa tayar kulkuwa na mistake huko nyuma ndio maan shetan akapat chance ya Kuwashawish.
 
Back
Top Bottom