Kumiliki pesa nayo ni tabia

Mr sule

JF-Expert Member
Oct 14, 2021
607
1,097
Mara nyingi utasikia vijana wakisema mwanamke akupende tabia yako na si pesa zako, miaka nenda rudi naona kabisa hii hoja haina mashiko kwangu kwasababu kumiliki pesa nayo ni tabia.

Eti pesa zikiisha nae anabadilika au atakukimbia, kwani hiyo tabia mnayosema nyinyi huwa ahibadiliki? Mf: alikuwa muhuni, alikuwa tapeli, alikuwa mtulivu lakini siku hizi kibaka. sawa inawezekana mwanamke akakupenda kisa we mpole lakini tabia yako inaweza kubadili na ukawa mtu wa ajabu, kwamba huyo mwanamke ataendelea kuwa na wewe?

Ndugu, jamaa marafiki. usione ajabu mwanamke kukupesa kisa pesa kwani tabia ya kumiliki pesa si kitu cha kawaida.

kikubwa akupende tu. pesa zikipotea na yeye akapotea ni sawa kwani hata ikiwa alikupendea wewe kwa upole wako, baadae ukawa mkali, kumbuka atapotea vilevile.

Kikubwa Endelea kuzitafuta na kuziongeza ili upendo wake uendelee kuongeza. shida yako kupendwa tu

Upendo una sababu zake, na katika sababu hizo amekupenda kisa una pesa hilo si tatizo kikubwa upendo tu.

Asante
 
Back
Top Bottom