Haya mambo huwa ni changamoto sana, 2010 wakati Jakaya anatangazwa mshindi nilikuwa kijijini kwetu enzi hizi sijaoa, baada ya matokeo kutangazwa nakumbuka ilikuwa Ijumaa usiku wa saa 2-3, maCCM huko yakaanzisha shamra shamra kuelekea makao makuu ya kata, mie nimelala zangu home mida ya saa 5 mlango wa chumba changu ukagongwa, kufunga mlango nakuta ni bwana mdogo na demu wangu, kiuhalisia nilikesha, saa 10:30 alfajiri nikamsindikiza home kwao wakiwa bado wamelala umbali wa 1km. Nikarudi kulala na uchovu saa 12:00 asubuhi Jumamosi (sabato) naamshwa kuna mgeni anaelekea Ukerewe nimsindikize kwa baiskeli! Karibu 5-6km kutoka kwetu hadi sehemu ya kivuko! Mgeni mwenyewe alikuwa wa kiume (a pastor) na kilo zake za kutosha, nikakomaa na baiskeli nikamfikisha kivukoni, nikarudi nyumbani, nilivyofika njaa ikawa inauma hatari ukizingatia kijijini kwetu hawana utaratibu wa kupika chai nilikuwa nahisi kizunguzungu nikaamua asubuhi hiyo kwenda kujisalimisha kwenye miti ya maembe ya majirani ndiyo ikawa pona yangu. Baadae namuuliza dogo wewe uliona nimekesha na kiumbe humu halafu asubuhi tena unanipa kazi! Dogo akajitetea kuwa alifanya hivyo sababu mimi ndiyo nilikuwa nafahamiana vizuri na huyo mgeni ( mchungaji), akanambia ningemweleza ampeleke yeye.