Kumfunga dawa/hirizi mtoto mchanga ni sahihi?

Okinawan

JF-Expert Member
Apr 10, 2018
253
259
Watu tofauti hutafsiri kuwa mtoto ni baraka,wengine husema mtoto ni bahati,mtoto hana hatia nk.

Na pia maandiko matakatifu(bible) yanasema kwamba "waacheni watoto wadogo waje kwangu .......... "

Sasa katika harakati zangu za hapa na pale nilisikia kunamzozo mkubwa ambao uliniacha nijiulize maswali kadhaa na moja ya maswali ni je,lazima mtoto mchanga agungwe dawa/hirizi mkononi?

Kisa chenyewe kilikuwa hivi

"Jamaa alikuwa na misimamo ya kidini na alibahatika kupata mtoto.Sasa kwasiri kubwa mkewe akishirikiana na mama yake mzazi waliamua kumpeleka kwa mganga na kwenda kumfunga dawa/hirizi mkononi.Mkewe na mama yake mzazi walipatana hiyo iwe ni siri yao.Sasa kwasababu jamaa alikuwa amesafiri hakujua kilichoendelea.

Mwisho wa siku mke alivyojua jamaa anakaribia kurudi mkewe akaanza kujihami akamwambia kwamba mama yako mzazi amemfunga dawa mtoto na mimi nilikubali kwasababu nilijua wewe umemuagiaza afanye hivyo.

HAPO NDIPO NILIPOSIKIA UGOMVI UKIANZA KATIKA MAZUNGUMZO YAO JAMAA AKIMLAUMU MKEWE KWA HILO JAMBO ALILOLIFANYA AKIDAI KUWA HAKUNA UMUHIMU WA MTOTO KUFANYIWA HIVYO.
 
Kuna baadhi ya jamii kwao ni jambo la kawaida.Unakuta msichana mrembo kweli kweli ila ukimchunguza shingoni, kifuani ama mikononi chale !!! lundo!!! hapo ni kumkimbia ukijifanya unaendeleza mahusiano utakuja kuoa mkemia mkuu wa ushirikina. Chale ni prima facie evidence ya uchawi
 
Kwa kuwa umezungumza kulingana uzoefu wa maisha ya kwenu na jamii yako uko sahihi kwetu siye chale ni urembo.
 
ni mila na desturi za jamii nyingi japo kwa sasa zinafifia na pengi zimetoweka kwa kukua elimu na imani za ukristo. kwa mtu mzima humsaidia kiimani. kwa mtoto ni sifuri kwani akili haijafikia uwezo wa kuamini.
 
Watu tofauti hutafsiri kuwa mtoto ni baraka,wengine husema mtoto ni bahati,mtoto hana hatia nk.

Na pia maandiko matakatifu(bible) yanasema kwamba "waacheni watoto wadogo waje kwangu .......... "

Sasa katika harakati zangu za hapa na pale nilisikia kunamzozo mkubwa ambao uliniacha nijiulize maswali kadhaa na moja ya maswali ni je,lazima mtoto mchanga agungwe dawa/hirizi mkononi?

Kisa chenyewe kilikuwa hivi

"Jamaa alikuwa na misimamo ya kidini na alibahatika kupata mtoto.Sasa kwasiri kubwa mkewe akishirikiana na mama yake mzazi waliamua kumpeleka kwa mganga na kwenda kumfunga dawa/hirizi mkononi.Mkewe na mama yake mzazi walipatana hiyo iwe ni siri yao.Sasa kwasababu jamaa alikuwa amesafiri hakujua kilichoendelea.

Mwisho wa siku mke alivyojua jamaa anakaribia kurudi mkewe akaanza kujihami akamwambia kwamba mama yako mzazi amemfunga dawa mtoto na mimi nilikubali kwasababu nilijua wewe umemuagiaza afanye hivyo.

HAPO NDIPO NILIPOSIKIA UGOMVI UKIANZA KATIKA MAZUNGUMZO YAO JAMAA AKIMLAUMU MKEWE KWA HILO JAMBO ALILOLIFANYA AKIDAI KUWA HAKUNA UMUHIMU WA MTOTO KUFANYIWA HIVYO.
Kuna dawa ambazo mtoto hufungwa mkononi lakini sio hirizi, kama unaufahamu ule ubani ambao unapulizwa kanisani na kazi yake? basi vipande vya ubani hufungwa kwenye kitambaa na kufungwa kwenye mkono wa mtoto kama mtoto huyo anatabia ya kuweweseka, watu wengi wenye maroho mabaya hupenda sana kuchezea watoto au kuvuruga amani ya mtoto, sasa akikutana na ubani anashindwa, hili ndilo nilijualo ila hilo la hirizi siwezi kulisemea.
 
ni ushirikina na imani mbovu mbovu

Watoto wakikristu hauwezi kuoa wamevalishwa mavitu yakichawi ila wale majamaa.watoto wao kifuani,kiunoni na mkononi utakuta wamevalishwa uchawi.
 
Huwa nashangaa sana watu kuwafunga hirizi watoto. Ndio maana uchawi unakua mwingi uswahilini. Maana mtu kazaliwa tu kashatundikiwa tunguri. Mwamini Mungu hakuna kitakachokusumbua, tunguri ni mzigo na unamfunga mtoto kwenye nguvu za giza na akikua anakuwa mchawi mchawi tu sio lazima aloge ila hata kufuatilia maisha ya wengine ni uchawi
 
Back
Top Bottom