Kumewahi kuwepo au kuna vyoo vya shule za sekondari ukiingia lazima uvue nguo nje

Kuna mahali nimesoma kwamba kuna mojawapo ya sekondari nchi hii ilikuwa ukiingia chooni lazima uvue nguo uziache nje vinginevyo utanuka sana harufu ya mavi kwa muda mrefu sana!

Story yenyewe inaelezewa kwa bashasha sana kana kwamba ni jambo mojawapo la kujivunia na wala sio la kusikitisha la shule hiyo! Pia hii ni story ya pili nasikia shule za aina hiyo.

Ni kweli kumewahi kuwepo na shule zenye vyoo vya aina hiyo au ni changamsha genge tu?
Yes,
tena mojawapo ipo mkoa wa Pwani,

kwanza ni Lazima uvue nguo zote nje lakini pia ukiingia kufanya mambo ukimaliza ni sharti uende bafuni moja kwa moja kuoga vinginevyo utanuka kama ambavyo umesema hapo juu 🐒

kama hujaoga, kila utakae pishana nae atajua tu umetoka kujisitiri msalani lakini hukutawadha mujarabu 🐒
 
Da umenikumbusha mbali sana mwenge singida 2010-2012.vile vyoo vya bweni la azimio.hatari tupu vilikuwa vinatema balaa.enzi za kipilinva na jemsi
 
Sinon Secondary Arusha..,miaka ya 2002 aseee sio story ni kwl na Mimi nilikuwa muhanga.....yaani unakuwa kama umejispry harufu ya nyaaa.....
 
Tabora boys,
Wanasema Huwa kina absorb harufu za watu wote wanaoingia halafu kina zi combine ukiingia humo unatokaa nazo.
Nadhani sababu ni ukongwe wa vyoo hovyo.
 
Kweli kua uyaone. Mimi toka shule ya msingi nimesoma shule mbili hadi sekondari sijawahi kukata gogo chooni.
Shule ya msingi nilikuwa nakaa nyumba za shule, sekondari nimekaa nyumba ya shule baadaye nikahamia nyumba binafsi karibu na shule.

Shida ya vyoo vya shule zote yaani ukiingia hamu ya kunya inakata kabisa, unakuta mavi yamepangana kama madini ya uranium. Wabishi wengine wakiona nya zimepangana, wao wanaenda mbali zaidi wanakunya pembeni au mlangoni kabisa.
 
Kuna mvuta bangi mmoja alikuwa anavulia nguo bwenini halafu anaenda you ilikuwa taabu unakuta mtu kadondosha gogo tangu mwaka juzi halijagiswa na kiumbe yeyote! Yaani Ile harufu Hadi unahisi Europe Europe a.k.a kizunguzungu. Nakumbuka vyoo vya shimo vilijaa likaja gari la kuvuta waliishia kuvuta ndoo mbili tu mataulo neti suruali zikawa zinaziba kwenye zile pipe ikabidi kabla ya kuvuta apatikane mzabuni wa kuloa hayo mataulo ilikuwa shughuli pevu Hadi Kuna jamaa alikuwa ana sura ya Buti tukawa tunamtania kuwa yeye ndo angekuwa mzamini wa ku hook lakini ukimtania aidha kuwe na bodaboda karibu au uvae helmet maana jamaa alikuwa na makonzi ya excavator
 
Nimesoma PUGU secondary miaka ya 2009 mpaka 2011 aisee hali ilikuwa mbaya sana kuvua nguo ilikuwa lazima ukitaka kuingia choooni lazima uvue nguo zote ili usiondoke na ile harufu mbaya ya chooni kutokana na uhaba wa maji kipindi hicho
 
Kuna mahali nimesoma kwamba kuna mojawapo ya sekondari nchi hii ilikuwa ukiingia chooni lazima uvue nguo uziache nje vinginevyo utanuka sana harufu ya mavi kwa muda mrefu sana!

Story yenyewe inaelezewa kwa bashasha sana kana kwamba ni jambo mojawapo la kujivunia na wala sio la kusikitisha la shule hiyo! Pia hii ni story ya pili nasikia shule za aina hiyo.

Ni kweli kumewahi kuwepo na shule zenye vyoo vya aina hiyo au ni changamsha genge tu?
Zipo. Hata shule niliyosoma ni hivyo. Ni hivi: vyoo ni shimo kubwa la mstatili, lililochimbwa likiwa na urefu na uapana wa eg mita 12 kwa 4. Halafu wanasakafia na kuacha matundu 24, kumi na mbili upande mmoja na 12 upande mwingine. Matundu yakajengewa vyumba vidogo vidogo vya bati, n juu paa la bati. Sasa mchana jua linapokuwa kali sana, kile kinyesi kinapata moto mkuu, na kuchemka kama malighafi ya kupikia gongo. Ikifika jioni sasa nenda uingie chooni, ufanye shughuli zako, huku ule mvuke wa hatari kabisa ukikupuliza. Halafu toka ingia ndani usikie shughuli. Kila mtu anakukimbia kwa ile pafyumu. NB: Enzi hizo ukisoma shule kama hii mtaani unaonekane wewe kweli ndiyo umesoma shule ya kikomandoo na ni mjanja. Ila tulikuwa hatuvui nguo ki-ukweli japo mtaani tulikuwa tunaongeza chumvi ile kunogesha story.
 
Kuna mahali nimesoma kwamba kuna mojawapo ya sekondari nchi hii ilikuwa ukiingia chooni lazima uvue nguo uziache nje vinginevyo utanuka sana harufu ya mavi kwa muda mrefu sana!

Story yenyewe inaelezewa kwa bashasha sana kana kwamba ni jambo mojawapo la kujivunia na wala sio la kusikitisha la shule hiyo! Pia hii ni story ya pili nasikia shule za aina hiyo.

Ni kweli kumewahi kuwepo na shule zenye vyoo vya aina hiyo au ni changamsha genge tu?
Pugu secondary school ndio kinara vizazi na vizazi 🤣🤣🤣
 
Kwamba shule za Boyz tu ndo zilikua na haya mambo? Mbona sioni wadada wakileta shuhuda zao Depal leta shuhuda
 
Back
Top Bottom