KUMEKUCHA..!! Watu 400 wavamia mgodi wa North Mara.

SHAMAC

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2017
Posts
1,340
Reaction score
3,565
Kundi la watu zaidi ya 400 kutoka baadhi ya kata zinazopakana na mgodi wa dhahabu wa North Mara wilayani Tarime wanaotakiwa kuhama kupisha shughuli za uchimbaji, wavamia mgodi huo leo ( Jumapili) wakidai malipo ya fidia.

Wananchi hao ambao maeneo yao yalifanyiwa tathimini tangu 2014 bila kulipwa hadi sasa, wanadaiwa kuchukizwa na kitendo cha majina yao kukosekana kwenye orodha iliyotoka hivi karibuni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa Tarime/ Rorya, Andrew Sata amethibitisha kutokea kwa jaribio la kuvamia mgodi uliodhibitiwa na polisi kwa mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.

Hakuna aliyejeruhiwa wala kushikiliwa kwa tukio hilo. Habari kwa kina fuatilia mitandao ya MCL na magazeti ya mwananchi..!!!
 
Mbunge wao atawapa plan B.

Mwenye habari ya hawa walipoanzia, naomba mnipe.
 
Deal done!..Walipewa route kule dodoma
 
Daah bora watulie tu watatolewa sadaka bure...!!
 
Haya mambo ya kunyanyasa watu na mali zao bado yanaendela kwenye utawala huu. Walipwe pesa yao. Mgodi mpaka unaanza inawezekana vipi watu wasilipwe. ndio maana mnawapa sababu wakina TL za kuongea tu.
 
North Mara iko chini ya Acacia wezi wa makinikia...Barrick watawalipa tu Dr John Magufuli alishatoa tamko la matumaini.

Tusubiri negotiations ianze na kumalizia kwa mafanikio.
 
Kundi la watu zaidi ya 400 kutoka baadhi ya kata zinazopakana na mgodi wa dhahabu wa North Mara wilayani Tarime wanaotakiwa kuhama kupisha shughuli za uchimbaji, wavamia mgodi huo leo ( Jumapili) wakidai malipo ya fidia.

Wananchi hao ambao maeneo yao yalifanyiwa tathimini tangu 2014 bila kulipwa hadi sasa, wanadaiwa kuchukizwa na kitendo cha majina yao kukosekana kwenye orodha iliyotoka hivi karibuni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa Tarime/ Rorya, Andrew Sata amethibitisha kutokea kwa jaribio la kuvamia mgodi uliodhibitiwa na polisi kwa mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.

Hakuna aliyejeruhiwa wala kushikiliwa kwa tukio hilo. Habari kwa kina fuatilia mitandao ya MCL na magazeti ya mwananchi..!!!
Wengine hawa hapa
1497806006613.jpg
 
Back
Top Bottom