Kumekucha ubungo terminal

happiness win

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
2,461
1,384
Wakazi wa Ubungo Terminal (nyuma ya stand ya mkoa) wameitishwa kikao na kujulishwa kuwa wanatakiwa kuhama ili kupisha upanuzi wa stand ya mabasi Ubungo, suala ambalo wamelipinga vikali.

Hivi Stand ya mabasi ni lazima ijengwe Ubungo tu? Kwa nini Serikali isitumie maeneo mengine kama eneo la TBS, au Eneo la Viwanda Ubungo pale nyuma ya Twiga Cement au Chibuku kupanua stand na badala yake kuwahamisha wakazi ambao wameshajijenga?

Serikali iangalie uwezekano wa kujenga stand ya kisasa ambako kutakuwa na huduma kwa chini na kwa juuu kuliko kuhamisha walalahoi wa Ubungo. Mbunge wa Ubungo, Mnyika unalijua hili???????
 
stend ya ubungo haikustahili kuwepo pale[/QUOT

Sasa wanalazimisha iendeleee kuwepo! Sioni ulazima wa kufanya hivyo. Ni bora waihamishe kabisa. Wanataka kuwatia watu hasara zisizo na msingi. Inaonekana wazi kuna maslahi ya walafi wachache.
 
Wakati muafaka wa kuihamishia stand kuu nje zaidi,ikibidi ipelekwe KILUVYA,hii itasaidi kuondoa msongamano wa magari.

Mipango yetu kama taifa inapangwa kwa span ya muda mfupi sana,hata wakiwaondoa wakazi wa maeneo hayo muda si mrefu bado eneo litakuwa halitoshi,mapendekezo yangu ni kuhamisha hiyo terminal na kutengeneza parking za magari eneo hilo na kuanzisha mradi wa treni za ndani ya JIJI kupunguza msongamano,hii itasaidia watu wenye private cars waweze kupark pale na kupanda treni kuelekea city centre hii itasadia sana kupunguza msongamano wa magari city centre.
 
Wakazi wa Ubungo Terminal (nyuma ya stand ya mkoa) wameitishwa kikao na kujulishwa kuwa wanatakiwa kuhama ili kupisha upanuzi wa stand ya mabasi Ubungo, suala ambalo wamelipinga vikali.

Hivi Stand ya mabasi ni lazima ijengwe Ubungo tu? Kwa nini Serikali isitumie maeneo mengine kama eneo la TBS, au Eneo la Viwanda Ubungo pale nyuma ya Twiga Cement au Chibuku kupanua stand na badala yake kuwahamisha wakazi ambao wameshajijenga?

Serikali iangalie uwezekano wa kujenga stand ya kisasa ambako kutakuwa na huduma kwa chini na kwa juuu kuliko kuhamisha walalahoi wa Ubungo. Mbunge wa Ubungo, Mnyika unalijua hili???????
happiness win mawazo yako yanaweza kuwa mazuri ila unayasema sehemu ambayo tunaosoma sio tunaopanga mipango ya maendeleo; unaweza kuwasilisha mawazo yako kwa baadhi ya madiwani unaofahamu au wewe mwenyewe kagombee udiwani ili ukatetee kile unachokiamini
 
Last edited by a moderator:

Inaonekana wazi kuna UFISADI tu unafanyika hapa na si kwa nia ya maendeleo. Ingekuwa kwa nia ya maendeleo wangeihamishia mbali kama mawazo yako yanavyoshauri.
 
Unategemea nini toka serikali ambayo mipango yake ya maendeleo ni ad-hoc wala si endelevu? Inaishia kuhamisha watu, kuvunja nyumba zao na kuwalipa fidia ambazo haziwezeshi kujenga hata 20% (ya thamani) ya nyumba zinazovunjwa! Poleni ndugu zangu!
 
Hizo ni dalili za mawazo finyu kwani bado tuna sehemu zenye nafasi kubwa kwa ajili ya kujenga stand kama madau mmoja alivyo pendekeza KILUVYA.Huku ni kutafuta uraji tu.Kwa kumbukumbu zangu eneo hilo la UBT ni mali ya UDA labda kama umiliki wake ulibadilishwa.Nchi hii kila siku jambo jipya la maudhi,dah yaani kichwa kinauma sana!
 
happiness win mawazo yako yanaweza kuwa mazuri ila unayasema sehemu ambayo tunaosoma sio tunaopanga mipango ya maendeleo; unaweza kuwasilisha mawazo yako kwa baadhi ya madiwani unaofahamu au wewe mwenyewe kagombee udiwani ili ukatetee kile unachokiamini

Ni kweli Ndachuwa, tatizo ni kwamba hakuna wa kusikiliza mawazo ya wananchi. Ingekuwa tunasikilizwa mambo mengi yangeenda vizuri. Kwa mfano Ubungo, Mbunge - Chadema, Diwani CCM yaani hakuna maelewano. Wameshindwa hata kutuchongea barabara kwa sababu ya tofauti za vyama. Hiyo stand ya mkoa inatiririsha maji taka kwenye makazi ya wananchi kila kukicha, tumepiga kelele tumechoka! Labda niombe nauli nikamuone MJOMBA!
 
Mji lazima upangike. Iwapo panatakiwa stendi, watu kuondoka ni halali.

Huwezi kupanga mji kwa kuondoa wakazi ambao mji wao umepangika vizuri kama Ubungo. Lengo lao ni kupanua Stand ya Mkoa ili kupata maslahi kwa matumbo yao kama ilivyo sasa bila kujali hasara na usumbufu kwa wakazi.
 
Wakazi wa Ubungo Terminal (nyuma ya stand ya mkoa) wameitishwa kikao na kujulishwa kuwa wanatakiwa kuhama ili kupisha upanuzi wa stand ya mabasi Ubungo, suala ambalo wamelipinga vikali.

Hivi Stand ya mabasi ni lazima ijengwe Ubungo tu? Kwa nini Serikali isitumie maeneo mengine kama eneo la TBS, au Eneo la Viwanda Ubungo pale nyuma ya Twiga Cement au Chibuku kupanua stand na badala yake kuwahamisha wakazi ambao wameshajijenga?

Serikali iangalie uwezekano wa kujenga stand ya kisasa ambako kutakuwa na huduma kwa chini na kwa juuu kuliko kuhamisha walalahoi wa Ubungo. Mbunge wa Ubungo, Mnyika unalijua hili???????

Nyuma ya ile stendi mbele kidogo kuna bonde,je wanataka kuwahamisha wote mpaka kule bondeni au ni nyumba za jirani? maana nilisikia wanataka mabasi ya kwenda mikoani yawe yanatokea kule nyuma na kuungana na njia ya kutoka mwenge kuja ubungo mataa ili kusaidia kupunguza msongamano
 
Tanzania maigizo hayaishi!!! KIJITONYAMA/MAKUMBUSHO ilifunguliwa stendi; wakawekwa hadi askari JIJI kuhakikisha magari yanaingia kituoni.....Jinsi hicho kituo kilivyokufa ni dhahiri kuna mtu aliaamua kutumia nafasi ya kupafanya mahala hapo pawe kituo cha daladala kisha iwe rahisi kwake kubadili matumizi ya ardhi kutokea MANISPAA!!!! Sasa hivi kuna jengo kubwa la biashara linajengwa na kifo cha kituo hakizungumziwi....

MUNGU anisamehe; mtazamo wangu unanionesha kuwa kwa thamani ya UWANJA WA UBUNGO ilivyo hata kituo kikipanuliwa; sio miaka mingi mbele matumizi yake YATABADILISHWA KWA KISINGIZIO KUWA ENEO NI DOGO ingawa wajanja wanaotafuta eneo wakati huo WATAKUWA WAMEFANIKIWA....

Tunafanywa MAZUZU KI KWELI KWELI....
 
Wanahamisha wakazi wote usawa wa stand hadi bondeni. Kanisa nalo linahama.
 
Tanzania maigizo hayaishi!!! KIJITONYAMA/MAKUMBUSHO ilifunguliwa stendi; wakawekwa hadi askari JIJI kuhakikisha magari yanaingia kituoni.....Jinsi hicho kituo kilivyokufa ni dhahiri kuna mtu aliaamua kutumia nafasi ya kupafanya mahala hapo pawe kituo cha daladala kisha iwe rahisi kwake kubadili matumizi ya ardhi kutokea MANISPAA!!!! Sasa hivi kuna jengo kubwa la biashara linajengwa na kifo cha kituo hakizungumziwi....

MUNGU anisamehe; mtazamo wangu unanionesha kuwa kwa thamani ya UWANJA WA UBUNGO ilivyo hata kituo kikipanuliwa; sio miaka mingi mbele matumizi yake YATABADILISHWA KWA KISINGIZIO KUWA ENEO NI DOGO ingawa wajanja wanaotafuta eneo wakati huo WATAKUWA WAMEFANIKIWA....

Tunafanywa MAZUZU KI KWELI KWELI....

Kweli wanatufanya mazuzu kwa lengo la kushibisha matumbo yao! wakivimbiwa watahamia kwingine na kuwaacha wananchi wanahangaika!
 
Du! Bingo. Kibadamo atapewa Fidia Sh. ngapi!

Kwani Kibadamo ipo nyuma ya stendi wajameni? kibadamo ipo pembeni ya Stendi na kama upanuzi utakuwa ni wa pembeni basi si kibadamo na wakazi tu wataathirika bali pia hoteli mpya ya MIC, hosteli za masters,Royal Njombe,Benki NBC wataathirika pia
 
Upanuzi utakuwa nyuma ya stand ila kibadado itamegwa kidogo kwa pembeni kwa lengo la kunyoosha vizuri hiyo stand yao.
 
Back
Top Bottom