Kumekucha, sogea tunong'onezane!

Kumekucha, sogea tunong'onezane!

Mom Fay

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2014
Posts
1,059
Reaction score
316
Habari ya asubuhi waungwana!! Wa safu hii ya maloveee hope mmeamka salama!!

Asubuhi ya leo naomba tuongee kitu kuhusu mahusiano yetu hasa mnaoishi kwenye ndoa haijalishi ni kwa mda gani au level gani mnayoishi .

Tuongelee kitu UVIVU

wanawake wengi tunakuwa wavivu baada ya mda flani yale mahaba nibebe unitupe kwenye dimbwi la mapenzi yanapungua mwanaume ni mtafutaji na kichwa cha familia kama tunavyoelewa.

Japo pia kuna wanawake wanaamka sawa na wamme zao kwenda kutafuta cha mdomoni lkn asilimia kubwa ya wanawake wengi ni mama wa nyumbani.

Na shuhuli zao ni za hapa na pale, wanawake tunakuwa wavivu wa kuamka mapema kabla ya wamme zetu, nguo pamoja na chai anaandaa housegal, haya mme anaamka mpaka anataka kuondoka unamuagia kitandani tena kwa mkono mmoja huku unasinzia utafikiri mwanao.

Na hata jioni akurudi anakuta housegal ndo anamuandalia chakula!! Hakumbuki mara ya mwisho kula cha kwako ilikuwa lini anarudi upo kwenye video sijui marmar and serio mara marichui nani anakwambia mwanamke.

Na hapo pata picha mama mkwe kaja kusalimia japo siku mbili tatu anaona hadi nguo za mwanae anafua dada wa kazi..weekend ndo movieee mziki mara kwa shost ako.

Eeh hivi mmeo unamuweka kundi gani?

Akichepuka na housegal utasema kakosea ili hali wewe umeona jukumu lako ni kumpanulia tu kitandani na wakati mwingine unamuhesabia tutafika kweli?

Sasa ngoja nikunong'oneze bibie mwanaume ni kama mtoto wala huitaji kukoroga lumbwata!! Anapenda kudekezwa,kusikilizwa,kuheshimiwa,mambo madogo madogo ya ndani ndo ufanya hata lile tendo la ndoa kunoga.

We pata picha kashiba chakula chako hata mkiingia kulala akikusifia mke wangu kweli mpishi,nipikie na hata mama watoto nipagawe!!

Jifunze kuamka mapema muandalie vitu muhimu muamshe apate kuoga chai umeandaa wewe mpaka anaondoka mkiss huku unamtengeneza kola hata kazini apaone mbali awahi kurudi unampokea vyema anafurahi hata ladha ya mapenzi inakuwa zaidi.

Hata kama una majukumu mengi mwanamke jitahidi kubalance mda wako mambo mengine yasilale kisa mfalme wako!! Na vilevile mwanaume muwe mnaridhika sasa mwingine utamfanyia yoteee bado lazima achepuke hilo ni pepo kemea kabisa.

Pambo lako mkeo!! Ni rafiki yako,mama yako,kipenzi chako anakamilisha furaha yako kwa kukupa heshima ya kuitwa baba.

Maelewano muhimu na mungu awasaidie!!
Momfay
 
Nina rafiki yangu jana kaniambia anasubiri mwanae aanze kutembea amuache huyo mzazi mwenzie...mwanamke kisirani toka qmejifungua na kazi zote anafanya housegal yeye analala tu.
 
Venezuela is running out of toilet paper.
 
Nina rafiki yangu jana kaniambia anasubiri mwanae aanze kutembea amuache huyo mzazi mwenzie...mwanamke kisirani toka qmejifungua na kazi zote anafanya housegal yeye analala tu.

Ndo tunapokosea sasa!!
 
Ni kweli ni wavivu sana,kila kazi anafanya mdada wa kazi,matokeo yake mdada anafanya kazi kwa ufanisi zaidi kuliko mama mwenye nyumba,hapo sasa tafrani ndo inapoanza na kupelekea mdada wa kazi kupanda cheo na kuwa mama wa nyumba...badilikeni wanawake aaaagh...
 
Bora wakwangu mimi ananivalisha G-string...kwa kweli inatosha kabisa. Munkari waletee ile picha ya naniliuuu yenye kipepeo
 
Last edited by a moderator:
Leo Mama Fay umetoa ujumbe fasaha na tena murua.Mungu akubariki kwenye mahusiano yako.
 
Kwa hili la leo nakuunga mkono!
 
Bora wakwangu mimi ananivalisha G-string...kwa kweli inatosha kabisa. Munkari waletee ile picha ya naniliuuu yenye kipepeo

hahahaha!! Ukute unampikia hadi huyo G string wako!! Ngoja uungue dushe! Hahaha! Picha kamera kibaka kanipora jana ngoja ntafute ingine!
 
Last edited by a moderator:
Nina rafiki yangu jana kaniambia anasubiri mwanae aanze kutembea amuache huyo mzazi mwenzie...mwanamke kisirani toka qmejifungua na kazi zote anafanya housegal yeye analala tu.

mshauri asifanye hivyo
 
Nina rafiki yangu jana kaniambia anasubiri mwanae aanze kutembea amuache huyo mzazi mwenzie...mwanamke kisirani toka qmejifungua na kazi zote anafanya housegal yeye analala tu.

Hata mimi mtu mvivu hapana yaani mimi niwahi amka wewe ubaki umelala, kiukweli kwenu utarudi bila taraka hadi ukifundishwa ndo utarudi kwangu
 
Dah kweli ujue! Kuna jirani yangu hapa mvivu balaa jana wameshindia chips za kibandani familia nzima mchana na usiku,afu ni vuvuzela hakiyanani mmmewe mvumilivu!!
 
Dah kweli ujue! Kuna jirani yangu hapa mvivu balaa jana wameshindia chips za kibandani familia nzima mchana na usiku,afu ni vuvuzela hakiyanani mmmewe mvumilivu!!

Huwezi kupata maendeleo km una mwanamke kama huyo...namrudisha kwao akale viepe
 
wenyewe wanasema wanaishi ki-digital
 
Dah kweli ujue! Kuna jirani yangu hapa mvivu balaa jana wameshindia chips za kibandani familia nzima mchana na usiku,afu ni vuvuzela hakiyanani mmmewe mvumilivu!!

duh yaani unajua jirani yako kala nini mchana na usiku??!!
 
hahahaha!! Ukute unampikia hadi huyo G string wako!! Ngoja uungue dushe! Hahaha! Picha kamera kibaka kanipora jana ngoja ntafute ingine!

Aaah wapi..... ivi Munkari unajua joto la papuchi linavisha yai.....sasa kama ni dushe kuungua lingeshaungua siku nyiingi...au wakati wakugegedana ungekuta inatoka harufu ya nyama choma kwa joto lile. Dushe limeumbwa halishiki moto.
 
Last edited by a moderator:
Mbarikiwe!! Ni vema mkaufatilia na uzi wa " kiustarabu,ukiona inakufaa ichukue" mtapata.kitu
 
Back
Top Bottom