Kumekucha: "Msiba wa Taifa" Toleo la 4..

Leo nimesikia eti wapiga mbizi kutoka afrika ya kusini wanaelekea kwenye eneo la tukio kuona kama bado kuna watu ndani ya meli! Hivi kweli Tanzania hatuna jeshi la majini? Yaani miaka 15 iliyopita tuliomba wapiga mbizi wa africa ya kusini mv bukoba ilipozama na leo hii tena tunafanya kilekile?
hivi yule mpiga mbizi tuliokuwa tunamuona sabasaba enzi zile tuko watoto bado yupo?

Good observation... kwani ripoti ya Mv. Bukoba mmewahi kuisoma?
 
Mkuu wangu kusema kweli meli zote hizo zinatakiwa kuwa grounded.. Tunatakiwa kutoipanda kabisa, lakini utaweza vipi kuwashawishi wananchi ambao wamezoea kupanda mitumbwi na ngalawa wakuelewe vizuri?

Nilikuwa naangalia boti hapa za "search and rescue" na bei zake. Nilivyoziona (mpya na za zamani) nimegundua kuwa kuna tatizo mahali fulani katika fikra za watawala wetu.

Nimejiuliza kuwa meli imeanza kuzama saa saba na nusu za usiku: Inachukua muda gani kumobilize vyombo vya umma kuitikia witu wa SOS?
 
Nilikuwa naangalia boti hapa za "search and rescue" na bei zake. Nilivyoziona (mpya na za zamani) nimegundua kuwa kuna tatizo mahali fulani katika fikra za watawala wetu. Nimejiuliza kuwa meli imeanza kuzama saa saba na nusu za usiku: Inachukua muda gani kumobilize vyombo vya umma kuitikia witu wa SOS?
Tunarudi kule kule kwa usalama, kwamba tumelala kumbe milango ipo wazi. Tuna matatizo makubwa kifikra. Somo la Mv Bukoba lilitakiwa liwe 'template' kwa mambo mengi.

1. Kwamba usafiri wa majini ni muhimu kama ulivyo wa anga na nchi kavu

2. Kwamba hatukujiandaa kwa majanga licha ya ukweli kuwa maelfu ya raia wetu wanatumia vyombo hivyo baharini na kwenye maziwa

3. Usalama wa vyombo vyetu ni wa hatari sana na tulitakiwa tuwe na tahadhari kubwa kuliko ilivyotarajiwa
(a) KM KM (Navy) ndicho kikosi kikubwa cha majini nchini. Wakati wa vita vya kagera Navy ilitumainiwa sana. Iweje leo hawana
wapiga mbizi au vifaa vya uuukozi wasiakiapo SOS hadi tualike kutoka south africa. Kwanini KM KM iwepo then
(b) Kikosi cha wanamaji nacho hakina wapiga mbizi, sijui kazi yake ni kujenga maboti pale kigamboni au ni kuitikia SOS
(c)Kama miaka 50 hatupata wapiga mbizi na vifaa tukijua uwepo wa hatari ya vifaa vya majini tumejitawala nini.
(d) Huu nao ni 'ufisadi' wa maisha yetu kwa kutumia SUMATRA,Bandari ambao hawajui hata kukagua usalama wa vyombo vya majini.
nk.nk.
 
Kwanini magazeti yeti hayajaandika kwa undani tukio hili? Something seems to be very wrong.
 
Hivi viongozi wa Zanzibar hawaoni hata aibu kusema hawajui nani anamiliki hiyo meli? Wazanzibar muandamane maan hao viongozi wenu wala rushwa hawawafai hata kidogo! Huko Zanzibar hakuna hata ICU, yaani Intensive Care Unit ya maana! Hela za utalii na meli zinaenda wapi? Amkeni! Mwenyezi Mungu alaze roho za marehemu mahala pema peponi. Amen.:llama:
 
Hivi viongozi wa Zanzibar hawaoni hata aibu kusema hawajui nani anamiliki hiyo meli? Wazanzibar muandamane maan hao viongozi wenu wala rushwa hawawafai hata kidogo! Huko Zanzibar hakuna hata ICU, yaani Intensive Care Unit ya maana!
Sitashangaa nikisikia kwamba huu ni mpango maalumu wa muda mrefu wa Nyerere!!!!!!!
 
Nyerere hakununua meli ya kuokolea watu.
Na matatizo ya life jackets hakuyamaliza, akaja mzee Mwinyi hakuyamaliza, akaja mkapa hakuyamaliza pia, sasa kwanini serikali ilaumiwe leo hii!!

Ni kwasababu ya ujamaa wa Nyerere uliotutia umasikini ndio maana tuliamua kubinafsisha sekta ya huduma za umma, tukauza MV Mapinduzi na Mv Maendeleo ili kutoa fursa kwa wawekezaji wenye uwezo kuwekeza katika 'maritime'.

Na ni muungano wa Nyerere ndio umeleta matatizo haya, si unaona ilianza na MV Bukoba iliyo nunuliwa wakati wake sasa imeelekea alikokusudia katika mpango wake maalum ulioandaliwa kwa kushirikiana na Uingereza baada ya uhuru!!
 
Mkuu wa mamlaka ya bandari Zanzibar ni Mustafa Aboud Jumbe.

Kwa vile taifa letu linaongozwa kwa jina la koo sitarajii kuchukuliwa hatua.

Na nimesikia hata elimu yake ni ya kuungaunga
 
Taarifa za awali zilidai kuwa meli hiyo ilibeba abiria wasiopungua 1000 japo uwezo wa meli yenyewe wa kubeba mizigo na abiria ni chini ya hapo
Mwandishi kakoroga abiria na mizigo na abiria...
 
Back
Top Bottom