Kumekucha CCM vs UKAWA

Daahh ni muda sasa ffu hawajawa bize sasa wamepata kazi
 
Huyo mtoto wa Mura hajui wala hana mamlaka na hicho anachokiongea. Labda kwao tu Tarime jambo hilo kwa kiasi wanaweza kujaribu kulifanya wakiwa na huto tupanga twao na wataipata fresh.

Mimi nina watoto kadhaa wakubwa kuliko huyo Mura, nusu ni wana CCM na nusu ni wana UKAWA, na tunaishi pamoja kama familia. Inawezekanaje eti wasishirikiane kwa sababu eti kuna Mura mmoja aliyeajiriwa BAVICHA katoa tamko. This is more than ridiculous!
 
Kuona watu anataka comments mana kwamba wako choking. No kweli kwamba hayo mahafali alikuwa ya kaskazini? Hii nchi mnaipeleka wapi? Nawashauri viongozi wenzangu tumlilie Mungu ashuke mwenyewe sasa maana busara na hekima ya binadamu imeshindwa kufanya kazi. Anayeweza sasa ni Yeye mwenyewe tu
 
haya mambo usiyadharau sana.
 
Hatari sana ,, yaaani vyama vifanye tushindwe hata kuzikana ??
 
Kama ndugu yako ni ccm na amefariki utafanya nn na wewe cdm
 
Nimetafakari kwa kina sana na nimefikia maamuzi ya kuunga mkono maamuzi ya BAVICHA , lengo langu kuu likiwa ni kuepusha shari zaidi , waendelee na yao na sisi tubaki na yetu , kujiepusha na hatari ni njia bora zaidi ya kubaki salama .
 
Tatizo wewe mwenyewe siasa umeigeuza kuwa dini!
 
Kama ndugu yako ni ccm na amefariki utafanya nn na wewe cdm
Tamko la vijana limezingatia yote haya , aliyetamka naye anao ndugu waliosalia gizani , bali ameona hali halisi , kama unaye ndugu ambaye ni sehemu ya wanaokunyanyasa unaogopa nini kuachana naye ? Undugu ni lazima uwe wa pande mbili .
 
Hao Bavicha bangi tu hawawezi kuharibu umoja aliotujengea mwasisi wa Taifa Hayati Baba wa Taifa. Mie nyumbani mdogo wangu CHADEMA, mjomba wangu UDP, Mama yangu CCM sasa mama yangu akipata tatizo mdogo wangu asimsaidie kisa CCM? Nadhani hizo zitakua ni akili za kushikiliwa na DJ Mbowe
 

Dini zenyewe zimeshindwa kututenganisha sembuse upuuzi wa vyama vya siasa.
 
Mie mbona nimeshaanza kutoshirikiana nao mwana JF yeyote wa CCM ninayemjua akianzisha thread sichangii.
ha ha haaaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…