Kumekucha: Balozi Dkt. Slaa na wenzake kuwasha Moto Temeke Jumapili 23/07/23

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,765
218,383
Taarifa iliyosambazwa leo Dar es salaam inaeleza kwamba ule mkutano kabambe ulioandaliwa na Wazalendo wanaopigania mali za nchi utafanyika Huko Temeke viwanja vya Bulyaga .

Inaelezwa kwamba hutakiwi kukosa Mkutano huo utakaohutubiwa na Wazito kadhaa Wazalendo kutoka vyama vyote ikiwemo ccm, Mkutano huo utaanza mapema saa 3 asubuhi ya Jumapili 23/07/23, hii ni kwa sababu watoa mada ni zaidi ya 50.

Unaambiwa huu ni zaidi ya mikutano ya hadhara uijuayo kwa vile kwa mara ya kwanza utakusanya watu wa vyama vyote , taarifa zaidi zinasema kwamba wako watumishi wazito wa Umma waliotaka kuja kuhutubia ili wafunue yaliyojificha, Lakini Kwa ustaarabu imeonekana Wanabanwa na Kanuni za Utumishi.

Taarifa yao hii hapa

Screenshot_2023-07-20-22-45-44-1.jpg
 
Mbona nembo ya Tangazo ni ya Chadema?
Hapo hata mimi pamenistua nikajua nyie wadau wa siasa pengine hii kitu kwenu sio mpya.

Chadema inazidi kukosea kwa kumruhusu huyo jamaa atoe hotuba zake chini ya mwamvuli wa Chama.

Kuna watu wa kuwapa second chance ila sio kwa huyu na mwenzake Lowasa.

Haya ni makosa makubwa Chadema inafanya.
 
Dr Slaa anaaminika na Wananchi wote
 
Mambo ya siasa ni muda sana tangu nifuatilie, kumbe ndugu zangu mmefika hadi huku?

Kwanini kwenye tangazo la hotuba yake imewekwa logo ya Chadema?

Kwamba huyu ni mwakilishi wa Chama?
Matangazo haya kila chama kimeyatoa , tangazo kutoka ccm nalo lina jembe na nyundo
 
Matangazo haya kila chama kimeyatoa , tangazo kutoka ccm nalo lina jembe na nyundo
CCM wana hiyo haki si mwanachama wao.

Ila hii kwa Chadema sioni kama inaleta taswira nzuri machoni mwa watu wenye busara zao.

Huyu jamaa alipoteuliwa na Magu alikuwa mtu mwenye roho mbaya hata kwenye mambo ambayo Magufuli alikuwa akikosea yeye aliunga mkono.

Sasa kwenye hili la bandari kwanini msijiulize kuwa huwenda upingaji wake ni kutokana na kukosa mgao?
 
Tumsamehe apambanie bandari yetu.. wapenda bandari wangapi tunajificha nyuma ya keybord tuu wanao jitokeza hivi wanafaa kuungwa mkono
 
Hapo hata mimi pamenistua nikajua nyie wadau wa siasa pengine hii kitu kwenu sio mpya.

Chadema inazidi kukosea kwa kumruhusu huyo jamaa atoe hotuba zake chini ya mwamvuli wa Chama.

Kuna watu wa kuwapa second chance ila sio kwa huyu na mwenzake Lowasa.

Haya ni makosa makubwa Chadema inafanya.
Sijasikiliza kwa jana wakati anatoa muongozo wa hiyo siku Dkt Slaa mwenyewe! Ila aliyeandaa hii issue sio Chadema ila huko clubhouse kuna room inaitwa Sauti ya Watanzania, mmoja wa admin ni yule jamaa alieyeandamana leo kwemye ubalozi wa Sweden kama umemuona, Sauti ya watanzania ndiyo wamehost mpaka hela zaidi ya milion 12 wao ndiyo walichanga na ata zile press conference anazofanya Dkt Slaa fedha inatoka Sauti ya watanzania.
 
Back
Top Bottom