Malaika Mkuu
JF-Expert Member
- Nov 5, 2014
- 902
- 909
Unafahamu sisi ndio tuliendelea kutoka zana za mawe kwenda zana za chuma kabla ya mzungu. Kilichoturudisha nyumba ni uchoyo wa share knowledge. Familia ya Tereweni babu yao ni mfua vyuma, basi atachagua wajukuu wa kuwafundisha, ilipelekea famila hiyo kuzalisha jembe moja kwa mwaka. Wazungu walipogundua ujuzi wa vyuma walishirikiana na kuzalisha bidhaa nyingi zaidi, chuma walikifikisha kwenye level nyingine walipojenga reli.Eti mtu mzima na akili zake oo angalieni nchi za wenzetu, walichofanya na sie tuwaige,
Watu wenye kusemaga hivyo nawaonaga kama ni kna KAONJE, coz kutwa ni kujipendekeza kwa wajinga waliotutesea babu zetu, mtu akiwa USA Or EUROPE basi anaona yupo peponi #pumbavu...tofauti ni majengo(mchanga na cement)...
...
LETS STANDS FOR OUR CONTINENT, LETS BRING POSITIVE CHANGES IN ALL ASPECT WHICH WILL ENRICH OUR GRAND DAUGHTER AND SONS.
Nimekupata vilivyo mkuuUnafahamu sisi ndio tuliendelea kutoka zana za mawe kwenda zana za chuma kabla ya mzungu. Kilichoturudisha nyumba ni uchoyo wa share knowledge. Familia ya Tereweni babu yao ni mfua vyuma, basi atachagua wajukuu wa kuwafundisha, ilipelekea famila hiyo kuzalisha jembe moja kwa mwaka. Wazungu walipogundua ujuzi wa vyuma walishirikiana na kuzalisha bidhaa nyingi zaidi, chuma walikifikisha kwenye level nyingine walipojenga reli.
Hatuwezi kuacha kuiga maendeleo ya wazungu kwakuwa walitutesa, lakini tuwe huru kujivunia utamaduni wetu.
nadhani hii ni moja ya sababu kadhaa zilizokuwepo...Kwenye anthropology nilisoma chanzo cha wazungu kuachana na biashara ya utumwa na kuanza kuwalipa mishahara.
Ilikuwa hivi, walionunua watumwa walikua na mashamba makubwa kwa Jamaica yalikua mashamba ya miwa na ulaya, Marekani, Brazil yalikuwa mazao mengine. Watumwa walikua ndio matrekta ya kufanya kazi shambani. Watumwa wanawake ambao umri umekwenda kidogo walipewa kazi ya kupika, walilazwa kwenye nyumba kama mabweni, asubuhi waliamshwa kwenda kazini na mchana walipewa muda wa kwenda kula na kurudi kazini. Wakati wa mavuno mwenye shamba alipata faida yote, gharama kubwa ilikuwa kununua chakula.
Ilitokea njaa kali sana Ulaya na hii ilipelekea kufanya gharama ya chakula kuwa kubwa, waliokua na watumwa walipata wazo kuwa hawa watu tukiwalipa mshahara kila wiki na kuwaambia wakajinunulilie wenyewe chakula, haitatugharimu sana. Pesa waliopewa ilitosha kununua chakula tu na malazi yalikuwa bure. Kutoka hapo ndio mabadiliko yalianza na mashirika ya dini yalianza kuingilia kati swala la kuwaachia huru watumwa.
Ndiyo mkuu na ndiyo maana nilisema anthropology na sio history.nadhani hii ni moja ya sababu kadhaa zilizokuwepo...