Kumbukumbu ya Mpira wa Makaratasi!

Kumbukumbu ya Mpira wa Makaratasi!

mkuu hiyo namba saba imenikumbusha mbali sana.sisi tulikuwa tunaiita 'fungulia mbwa' hapo ni wababe tu walikuwa wanabaki yaani ukianzishiwa mpira golini kwako unaenda nao mpaka golini kwao hadi kipa anakukimbia!ukikutana na kipa mjanja anahamisha magoli(kipindi hicho magoli ni mawe au vijiti)


Hah hah haaah Fungulia Mbwa au Fungulia Ng'ang'a
 
Tehteh Mkuu ndio umemaliza kabisa ukweli wa huu mpira nimecheka mpaka basi memory imefanya kurudi katika kurusha ndio inakuwa mtihani kwanza unaangukia mpira nje sehemu ya matakataka na miba na vigae huko upo Peku unaeenda kuuchukua urushe ila mnapigana kikumbo kuwahi kurusha sikilizia mrushaji sasa wooooote mnajaa Golini kama Magoli ni ya miti haya au Mawe ila utarushwa kwa nguvu hata usimguse mtu ukapita golini ulalamishi hapo ni Goliiiiiiii Dk 10 za ulalamishi.


Halafu ilikuwa hivi kama mechi itakuwa droo mpaka saa 18:40 jioni basi timu moja ikItokea ikapata Goli basi tangazo la haraka sana toka kwa timu iliopata goli hilo la jioni litasikika likisema ''KWALEO''

Hapo inamaanisha mpira kwishney
 
dah nishang'oa kucha vibaya mno kwa kupiga dochi Jiwe lililokuwa nimesimama kama lile jina la timu iliyoichapa Simba 1-0 Dar kisha wakaenda kuwacharaza goli 4-0 kule Angola.

tehteh lile jiwe lazima mtu uligonge na kucha labda timu ya kuvua iwe imewekesha manguo yao juu ya jiwe na usiombe wale wanaokaa nyuma ya goli wawe wanamchukia kipa wa timu ambayo sio yao lile jiwe linaongewa kiaina sasa funga goli alafu wastukie watu huo ulalamishi wa sio goli tupige hatua za goli tuone kama limezidishwa nakama lilipunguzwa sana mtemi atalazimisha ni goli japo limepita pembeni ya jiwe dah. hapo hatujaongelea Kitenesi au CHANDIMU tulikuwa tunakiita magoli madogo.
 
Mnakumbuka kipindi cha kujifunza ball control, skills mwenyewe unafunga kamba ndefu afu unaishikilia kwa mkono unaanza kuupiga mpira...
Dana dana unaanzia kujifunzia pajani..
 
Back
Top Bottom