Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,916
- 30,259
KUMBUKUMBU YA MIAKA 50 YA KIFO CHA ABDUL SYKES MAKALA ZA AISHA ''DAISY" SYKES BURUKU KATIKA GAZETI LA RAIA MWEMA LA JUMATANO
Kuanzia toleo la kesho tarehe 10 Oktoba Aisha ''Daisy'' Sykes Buruku anaeleza yale aliyoshuhudia nyumbani kwao wakati baba yake anaijenga TANU kuwa chama imara cha ukombozi wa Tanganyika:
''...ilikuwa katika kipindi hiki cha mimi kuanza kupata akili katika kukua kwangu ndipo nilipokutana na wanawake wazalendo waliokuwa wanaochipukia katika uongozi wa Tanganyika, wanawake kama Bi. Lucy Lameck kutoka Moshi, Mary Ibrahim na akina mama wa Kiislam kama Bi. Titi Mohamed, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Hawa bint Maftah, hawa kutoka Dar es Salaam, wote hawa kwangu mimi walikuwa bibi zangu.
Kitu cha kufurahisha ni kuwa hawa akina mama wa Kiislam wote walivutwa katika siasa na Bibi Chiku bint Kisusa, maarufu akijulikana kama Mama Sakina. Alikuwa Mama Sakina ndiye aliyewapa hawa wanawake wa Kiislam niliowataja hapo juu utambulisho na wakaja kuwa watu maarufu.
Baba yeye ndiye alikuwa kiongozi wa mikakati hii yote kwa sababu bila yeye kuwatia hima kwa kutumia ushawishi wake ingekuwa vigumu kuweza kuwatia hawa wanawake katika kuwahamasisha wanawake wenzao wa Kiislam na wao watoke majumbani kuja mstari wa mbele katika mikutano wakiimba na kutoa vibwagizo vya kuunga mkono TANU na kudai uhuru.
Hili jambo lilikuwa jipya, jambo ambalo katika utamaduni wetu kwa wakati ule halikutarajiwa na ni kinyume katika utamaduni wetu kwa wanawake wa Kiislam kulifanya katika siku zile.
Nimesikia mazungumzo mengi wakati baba na wenzake walipokuwa wakijadili majina na shughuli ambazo hawa akina mama walikuwa wahusishwe ili kuleta mvuto wa kisiasa katika mikutano yao ya TANU.
Nakumbuka vizuri sana jinsi baba alivyokuwa karibu sana na Mwalimu Sakina na ndugu yake Mwalimu Fatna (wote hawa watoto wa Mama Sakina), na jinsi alivyowaleta ndugu hawa karibu na Mama Maria na hawa wakamjulisha Mama Maria Nyerere kwa mama yao na mashoga zake Bi Hawa Maftaha, Bibi Titi Mohamed na Bi Tatu binti Mzee...''
Kulia ni Bi. Tatu bint Mzee, Bi, Titi Mohamed, na wa kwanza kushhoto ni Bi. Chiku Said Kisusa wakiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere Uwanja wa Ndege safari ya kwanza UNO 1955