Kumbukumbu ya miaka 50 ya kifo cha Abdul Sykes makala za Aisha ''Daisy" Sykes Buruku katika gazeti la Raia Mwema la Jumatano

Bwana Ndjabu,
Tuendelee na Sykes...

Siku moja nikapokea simu kutoka BBC wakaniuliza kuhusu War Diaries za Kleist Sykes.

Wakanambia wanataka kuadhimisha miaka 100 ya WWI na wamepewa taarifa kuwa mie
ninazo War Diaries zake za WWI na wangependa nishiriki katika kipindi cha BBC TV
ambacho watarekodi British Council Library na wanategemea nitawaeleza nini kimo katika
hizo diary.

NIkawaeleza kuwa hakika nina kitu kama hicho ambacho nimenyanyambua kutoka mswada
alioandika na ndani yake ameeleza yalitotokea wakati yeye na ndugu yake Schneider Plantan
walipokuwa vitani wakipigana chini ya Kamanda Von Lettow Vorbeck.

Jamaa wa BBC homa ya Sykes imewapanda wananiomba lazima nishiriki kwani hawana ''first
hand,'' info. kama hiyo ya askari Mwafrika aliyepigana dhidi ya Waingereza Afrika na akaandika
kwa mkono wake mwenyewe yale aliyopitia vitani.

Siku nyingine nimejiwa na ugeni ambao sikuutegemea lakini wameletwa kwangu na mtu namjua.

Hawa jamaa wao ni watengenezaji filamu na ''documentaries,'' wanataka kutengeneza filamu ya
Sykes kuanzia walikotoka Mozambique 1880 hadi kufikia 1950s mjukuu wa Sykes Mbuwane,
Abdul Sykes anakutana na Mwalimu Nyerere katika siasa za ukombozi wa Tanganyika.

Jamaa wananiambia wanataka kuanza kijijini Kwa Likunyi, Msumbuji hadi Pangani na kufata
nyayo hadi Baganoyo wakati wa Vita na Bushiri hadi Kalenga walipopambana na Chief Mkwawa
hadi Mto Ruaha alipofia Sykes Mbuwane.

Historia nzima ya Wazulu walioingia Tanganyika hadi kufikia watoto wao.
Nikawa nawaeleza ninayoyajua na wananiuliza maswali.

Homa kali ya Sykes imewapanda wakaniuliza na wao pia kuhusu War Diaries WWIIza ndugu
wawiliAbdul na Ally.

Nikawaambia ninazo diaries za Ally Sykes akiwa Burma WWII kanieleza kwa kinywa chake
mwenyewe na nimenadika maisha yake.

Jamaa wananiambia, ''You know Mohamed you have an epic story here.''

Kwa kweli hawa jamaa walikuwa taaban pale nilipowataja marafiki wakubwa wa Ally Sykes -
Peter Colmore na Jim Bailey na kuwaonyesha historia zao nilizoandika kuhusu maisha yao
Afrika.

''Mohamed did you actually meet and talk to these people?''
''Yes I did.''

Hawa jamaa walishangaa kusikia kuwa mimi hawa watu nilikuwa najuananao kwani wana
historia ya pekee katika Afrika.

Mimi nilibaki kucheka tu niliwaonyesha picha mimi na Peter Colmore niko nyumbani kwake
Muthaiga, Nairobi mwaka wa 1996.

Bwana Ndjabu,
Siko peke yangu niliyestaajabishwa na historia hii ya akina Sykes.

Huna haja ya kutukana ikiwa huipendi usisome kwani kuna wengi sana kwao wao historia
hii ni, ''one epic story.''
 
Back
Top Bottom