THINKINGBEING
JF-Expert Member
- Aug 9, 2010
- 2,779
- 1,304
Leo ni mwaka wa pili toka aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa Daudi Mwangosi auawe pale kijiji cha Nyororo Mufindi wakati akiwa katika kazi yake ya kuandika habari.
Serikali sikivu ya CCM japo imeoneshwa kila aina ya ushahidi imepuuza kuwachukulia hatua stahiki waliofanya ukatili huu.Tumeambiwa waliofanya ukatili huu wamepandishwa vyeo na watawala wetu wasikivu.
Dhihaka nyingi zimefanywa juu ya kifo hiki hata kufikia hatua ya mpiga propaganda Habibu Mchange kusema mauaji yalifanywa na CHADEMA.Anataka tuamini eti watu waliovalia sare za polisi tunaowaona kwenye picha ya mauaji ni CHADEMA na magwanda yao.
Familia yake na ndugu zake, IPC, UTPC na wadau wengine hawawezi kamwe kusahau mauaji ya Daudi Mwangosi kwani yalikua ni mauaji ya kinyama na ukatili wa hali ya juu.
Kuna kila dalili kwamba wauaji wameshajitangaza washindi hapa duniani.R.I.P Mwangosi.