Kumbukumbu ya Martin Luther King Jr. , Watanzani wanamkubali?

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,745
5,446
Leo radio za VoA na DW walimzungumzia Mch. Martin Luther King Jr ambaye aliwaongoza Wamarekani weusi kupinga ubaguzi dhidi ya watu weusi huko Marekani miaka ya 1960. Harakati zake zilisababisha kifo chake kwa kupigwa risasi na wahafidhina. Je, watawala wetu na watetezi wanaowatetea kwa kila jambo wangesemaje juu ya harakati zake? Wangemuunga mkono au wangesema anachanganya dini na siasa?

Vv
 
I have a dream
 
MLK jr.png

DR. MARTIN LUTHER KING JR. (1929-1968)
MLK jr.png

- Alizaliwa na Kuitwa Michael King Jr.
- Baada ya baba yake mzazi ( Michael King Sr) kufanya ziara ujerumani alirudi akabadili jina lake na la mtoto wake kuwa Martin Luther + King ( Akichukua jina la Martin Luther Kasisi Mwanzilishi wa Uprotestanti).
- Alikuwa mpigania haki za kiraia za watu wenye asili ya Afrika,Alikuwa Maarufu sana hasa kwa njia aliyoitumia kudai haki za weusi ya kutokutumia Vurugu wala nguvu. ( Non - Violence).
- Aliwahi kuswekwa lupango zaidi ya mara 29!
- Aliongoza maandamano makubwa kabisa kupinga unyanyasaji na kususia usafiri wa Mabasi kwa watu wenye asili ya Afrika hasa pale Mwanamama Rosa Park alipogoma kupisha siti za mbele zilizotengwa kwa ajili ya Wazungu.
- Alifahamika zaidi kwa Hotuba zake zilizojaa Upendo na Hamasa ya kudai haki kwa njia ya amani.
- Hotuba yake Maarufu ni ile ya NINA NDOTO ( I have a Dream).
- Aliwahi kuwa Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel.
- Aliuwawa kwa kupigwa risasi 1968.
- Mama yake mzazi ( Alberta William King) pia aliuwawa kanisani kwao Ebenezer baptist Church kwa kupigwa risasi 1974. Inasemekana aliyelengwa alikuwa Mzee Martin King Sr. lakini siku hiyo hakuwepo Kanisani.
- FBI walifuatilia maisha yake yote ya harakati kwa miaka 12 kwa kunasa mawasiliano yake ya simu na maisha yake binafsi.
- Aliwahi kuhusishwa na Kashfa ya Ngono (kuwa na mahusiano nje ya ndoa)
- Alikuwa Kiongozi shupavu aliyevumilia mengi hasa kwa kuchagua kudai haki bila kusababisha matata kama jinsi vikundi au watu wengine wenye asili ya afrika walivyochagua kudai haki kwa nguvu na kwa njia yeyote ile (By any necessary means) kama kina Malcom X na The Black Panther Party.
Anakumbukwa kwa mengi mazuri na ya haki aliyoyawezesha kupatikana kwa jamiii yake ya watu wenye asili ya Afrika?Weusi.

Haya ni baadhi ya Maneno mazuri aliyoyatamka kuhusu Harakati za kudai Haki na Usawa.( Tafsiri yangu)
- Nimeamua Kujikita kwenye Upendo kwa Sababu chuki ni nzito kuibeba
- Tishio la haki popote ni tishio la haki kokote
- Chuki huzalisha chuki kenye giza totoro lisilo na Nyota,hivyo giza haliwezi ondoa giza ni Mwanga tu ndio unaoweza kuondoa giza.
- Kuna Nyakati kila Mtu anapaswa kuamua kwa kufuata Nini Ufahamu wake wa rohoni unamwambia ni sahihi kufanya na wala sio kutafuta Umaarufu au Maslahi ya kisiasa au ustawi ubinafsi.

Ongeza na wewe!
 
Watoto wetu hawamfahamu hata Moringe Sokoine watamfahamu Dr Luther kweli ??
Mbona unatuonea bure mkuu ???
Hilo swali ni kwa ajili ya wanasiasa na watawala wetu pamoja na wafuasi wao ambao hutaka kutuaminisha kuwa Wachungaji, Maaskofu na Mashehe hawapaswi kuzungumzia siasa.

Vv
 
View attachment 734716

DR. MARTIN LUTHER KING JR. (1929-1968)
View attachment 734716
- Alizaliwa na Kuitwa Michael King Jr.
- Baada ya baba yake mzazi ( Michael King Sr) kufanya ziara ujerumani alirudi akabadili jina lake na la mtoto wake kuwa Martin Luther + King ( Akichukua jina la Martin Luther Kasisi Mwanzilishi wa Uprotestanti).
- Alikuwa mpigania haki za kiraia za watu wenye asili ya Afrika,Alikuwa Maarufu sana hasa kwa njia aliyoitumia kudai haki za weusi ya kutokutumia Vurugu wala nguvu. ( Non - Violence).
- Aliwahi kuswekwa lupango zaidi ya mara 29!
- Aliongoza maandamano makubwa kabisa kupinga unyanyasaji na kususia usafiri wa Mabasi kwa watu wenye asili ya Afrika hasa pale Mwanamama Rosa Park alipogoma kupisha siti za mbele zilizotengwa kwa ajili ya Wazungu.
- Alifahamika zaidi kwa Hotuba zake zilizojaa Upendo na Hamasa ya kudai haki kwa njia ya amani.
- Hotuba yake Maarufu ni ile ya NINA NDOTO ( I have a Dream).
- Aliwahi kuwa Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel.
- Aliuwawa kwa kupigwa risasi 1968.
- Mama yake mzazi ( Alberta William King) pia aliuwawa kanisani kwao Ebenezer baptist Church kwa kupigwa risasi 1974. Inasemekana aliyelengwa alikuwa Mzee Martin King Sr. lakini siku hiyo hakuwepo Kanisani.
- FBI walifuatilia maisha yake yote ya harakati kwa miaka 12 kwa kunasa mawasiliano yake ya simu na maisha yake binafsi.
- Aliwahi kuhusishwa na Kashfa ya Ngono (kuwa na mahusiano nje ya ndoa)
- Alikuwa Kiongozi shupavu aliyevumilia mengi hasa kwa kuchagua kudai haki bila kusababisha matata kama jinsi vikundi au watu wengine wenye asili ya afrika walivyochagua kudai haki kwa nguvu na kwa njia yeyote ile (By any necessary means) kama kina Malcom X na The Black Panther Party.
Anakumbukwa kwa mengi mazuri na ya haki aliyoyawezesha kupatikana kwa jamiii yake ya watu wenye asili ya Afrika?Weusi.

Haya ni baadhi ya Maneno mazuri aliyoyatamka kuhusu Harakati za kudai Haki na Usawa.( Tafsiri yangu)
- Nimeamua Kujikita kwenye Upendo kwa Sababu chuki ni nzito kuibeba
- Tishio la haki popote ni tishio la haki kokote
- Chuki huzalisha chuki kenye giza totoro lisilo na Nyota,hivyo giza haliwezi ondoa giza ni Mwanga tu ndio unaoweza kuondoa giza.
- Kuna Nyakati kila Mtu anapaswa kuamua kwa kufuata Nini Ufahamu wake wa rohoni unamwambia ni sahihi kufanya na wala sio kutafuta Umaarufu au Maslahi ya kisiasa au ustawi ubinafsi.

Ongeza na wewe!
Najiuliza kama wanaokubaliana na chochote kutoka wa watawala wataipenda nukuu hizi.

Vv
 
Back
Top Bottom