Kumbukumbu ya Brigedia Gen. Moses Nnauye!

Kumbukumbu ya Brigedia Gen. Moses Nnauye!

Lilisahaulika wakati taarifa inachapwa. Na miongoni mwa wakwe nimeona January, ni Makamba? Nape anashambuliwa sana hapa kuwa ni balaa tuliloachiwa na baba yake. Lakini ukweli ni kwamba huyu ni miongoni mwa watanzania wachache sana wenye ujasiri wa kusimama mbele ya mafisadi ndani ya chama chake cha mafisadi. Shutuma zote tunazomrushia zingeelekezwa kwa mwenyekiti wa chama chake.

Hapo nakuelewa ila ajitahidi kutokuwashambulia wapambanaji wenzake wakati anajua fika kuwa hukoccm atatolewa kafara soon.
 
Nimesoma mwanzo mpaka mwisho; hoja iliyotawala ni dini ya Mzee Nnauye na kama Nape ni mtoto wa Mzee Nnauye au hapana!!!!! Nini umuhimu wa yote hayo?! Kama Mzee Nnauye ni Mwislamu, Mkristo au Mpagani, nini umuhimu wa lolote katika hayo?! Likewise, kama Nape ni mtoto wa Mzee Nnauye au hapana, shida ipo wapi?! Kuna mdau mmoja, kasema kwamba kutokuwepo jina la Nape kwenye orodha iliyotolewa itawasaidia watu kumchafua kisiasa...ni mwana siasa gani mwenye kutumia hoja dhaifu kiasi hicho?! na kama atakuwepo hapo atathibitisha wazi kwamba hoja za msingi hanazo bali anajiegemeza kwenye hoja chakavu!! Kwani hata kama Nape ni mtoto wa nje ya ndoa, tatizo kwake yeye ni nini?! Wa kulaumiwa si wazazi wake?! Kwani alijizaa mwenyewe?! Mtu yeyote atakayemkashifu Nape kwa kuzaliwa nje ya ndoa (kama ndivyo) anatakiwa kujiuliza yeye mwenyewe alifanya jitihada gani ata akazaliwa ndani ya ndoa!!! Ajiulize, kuna chochote alifanya hata akazaliwa ndai ya ndoa au automatically tu alijikuta amezaliwa ndani ya ndoa?! Kumkashifu mtu aliyezaliwa nje ya ndoa, kinyume chake ni kwamba unajiona fahari kuzaliwa ndani ya ndoa! Ni upuuzi uliopita kipimo kujifaharisha kwa ki2 ambacho huku-contribute hata punje moja ya mchanga!
 
Answer:
Mbona kama umeongea kinyume mkuu,hao wanaoitwa mafisadi si maadui zake huyu au mafisadi gani pengine unaowazungumzia???labda na wewe un a tafsiri yako kuhusu ufisadi na mafisadi!

Anamwongelea mwenye Richmond yaani yule aliyetajwa wiki iliyopita na waziri mkuu mstaafu
 
Pia haiko wazi ni mtoto yupi, Nnauye ameach LUNDO la watoto!

Nnauye ...alikuwa na watoto karibu 20..,nalifahamu hili kwa kuwa msiba wake nilishiriki vilivyo kwenye maandalizi..Yake pale nyumbani kwa mzee makamba ....
Mwanaisha hakuwa mwanamke pekee wa mzee Nnaauye....ambaye alikuwa charismatic na ladies choice.....sijui ni waziri gani wa enzi za mwalimu ,mwanamke...wasichana makada wa enzi hizo ambao walikuwa "hawamhui" brig gen.Nnauye ....alikuwa simply wa wote.....hata wenzake enzi za walimu walikuwa wakimtania waziri wa wanawake.....and would make Nyerere lough....that something they have in common with KIkwete ....ila tofauti ni kuwa KIkwete amejitahidi kuishika familia Yake pamoja .....na ameweza kuwaorodhesha wengi wa watoto wake chini ya mama mmoja .....amedeclare Ana mke mmoja na watoto zaidi ya nane ....that was good.....
Na Ana uwezo wa kuendelea kuwaandikisha chini ya mama mmoja .....hii itasaidia familia Yake miaka ijayo kuondokana na aibu ya watoto wa mke wake kutaka kujiona bora ....kuliko watoto wingine....

May be we can share na members wanawake ...kwanini hawapendi watoto wa wenzao?.....kwetu sisi wanaume watoto wote ni halal.....hakuna haramu...kwani hujui atakaye kusitiri ni yupi...
 
MOSSES kwa kiswahili ni MUSSA, ninaye rafiki ambaye mwanaye amebatizwa kwa jina la Mussa (ni mkatoliki)
Mussa inatumika pande zote na ni aghalabu kumkuta mkristo akiitwa mussa lakini ni kioja kumkuta muislam akiitwa moses!muislam ni mussa tu!
 
BAADA YA UCHUNGUZI WA KINA WA TANGAZO HILI NIMEGUNDUA YAFUATAYO

-HABARI HII IMEWEKWA HAPA NA VUVUZELA,MTU WA MIPASHO NAPE NNAUYE

-NAPE SIO MTOTO WA MOSES KWA SABABU UKICHUNGUZA TANGAZO LA NDANI LENYE PICHA YA COMRADE MZEE MOSES WATOTO WALIOTAJWA PALE NAPE HAYUPO

-KUNA MJUKUU ANAYEITWA NNALEKANA AMBAYE YUPO KWENYE TANGAZO ILA KWENYE THREAD YA NAPE HAYUPO

-JANUARY MAROPE AMEOA MTOTO WA NNAUYE????

-THE ROMANTIC NI USER ID AMBAYO KILA SIKU INAINGIA NA KUPOST HUMU UTUMBO

-ROMANTIC NI USER ISIYO RAFIKI NA CCM HATA KIDOGO my take NAPE HAKUBALIANI NA JK NA HIVYO ANAITUMIA ROMANTIC KUMPONDA NA KUELEZA LILILO MOYONI MWAKE SIO MDOMONI

-NAPE NI MNAFKI KWANI KWA ID HII YA ROMANTIC AMEONYESHA KUWA MKWELI ILA AKIWA MBELE ZA WATANZANIA ANAONGEA KAMA WALE JAMAA WANAOTOA ULE MTANDAO WA NUSU SHILINGI

badilika braza siku zimeisha

"-NAPE SIO MTOTO WA MOSES KWA SABABU UKICHUNGUZA TANGAZO LA NDANI LENYE PICHA YA COMRADE MZEE MOSES WATOTO WALIOTAJWA PALE NAPE HAYUPO"

Du kwa hiyo kwa kuwa hajatajwa kwenye tangazo basi ndio determinant yako kwamba jamaa sio mtoto wa mzee nnauye sio!kweli unahitaji kukazwa kitako hasa kuelemishwa...



 
Mussa anaweza kuwa mkristo vilevile; unless una uhakika na unachokisema, otherwise, kwa hilo jina bado hakuna concrete evidence kwamba huyo brigedia alikua muislam!!

Na ile INNALILLAAHI WAINNA ILLAIHI RAJUUN ambayo imeandikwa kwenye tangazo la wanafamilia wa nyumba kubwa nayo haikushawishi pia?
 
Sasa kuitwa Mussa ndio kusema kina mussa wote ni waislam... WadaNGANYIKA tabu sana. Kwa kifupi ukiwa kanisani ibada ya kiswahili atasemwa Mussa na ibada ya Kiingereza atasemwa Moses.... Nadhani umeelewa vizuri.

Nimeelewa vizuri sana...ila sijaelewa kama na msikitini nako mussa anaweza kuitwa moses!
 
Na ile INNALILLAAHI WAINNA ILLAIHI RAJUUN ambayo imeandikwa kwenye tangazo la wanafamilia wa nyumba kubwa nayo haikushawishi pia?

Huo uswahili wa watoto wa the so called nyumba kubwa ...unaendeleza bifu Hadi kwa marehemu....?....Hadi kuwatenga nyie wengine
 
Ngoja nibadilishe mfano maana waDAGANYIKA huwa wagumu kuelewa. Kwa kifupi swala la Mussa au Moses ni lugha tu. E.g. Kiongozi wa dini ya kiislam akiwa anaongea English katika msikiti hapa London atasema Moses na akiwa Mwembechai kwa waswahili anasema Mussa. Hapa nadhani umenipata Daudi (Ah ah ah DAVID hapa london)

Nakumbuka nilisoma chuo kikuu kimoja na mtu kutoka Egypt ambaye ni mkristu na kwa kuwa kulikuwa kuna utaratibu wa kwenda kanisani asubuhi siku moja ilikuwa tabu sana alipoandika "Yesu ni Jibu"kwa lugha ya kiaarabu maana watu wengi wanadhani kiaarabu ni uislam.... Basi nilipomaliza chuo akanizawadia tshirt moja inayosema "Yesu ni Jibu" na nilipotua bongo nikawa naitinga basi mazuzu wakawa wanasema duu huyu jamaa siku hizi ni muislam. HUU NI MFANO TOSHA KWA WANAODHANI UKIITWA MUSA WEWE NI MUISLAM NA UKIITWA MOSES WEWE NI MKRISTU.

KWELI NI MFANO TOSHA KWA HAO "WANAODHANI",Lakini mi si katika hao,mzee mnauye alizikwa kwa taratibu za kiislam pale kisutu chini ya usimamizi wa ndugu yaka yusuf makamba,bado sio kigezo???wabongo tunapenda sana ligi za ubishi wa kitoto!
 
matangazo kama haya wayapeleke bango mda ni mdogo sana kudiscuss marehemu hapa.
Tunashukuru sana kwa mchango wako katika mjadala huu japo umedai nafasi ni ndogo lakini tumegundua unayo!asante sana kwa kutumia muda wako wa thamani kujadili.
 
moses ni jina la kiislamu, malima ni jina la kiislamu. wapi walibadili majina? . na huyu mtoto wa nauye anayeitwa joseph , na huyu mariamu nao walipewa hayo majina ili wasome kwa mission? mawazo hafifu haya. wote hawa wanao soma hizo shule za mission mpaka leo hii wanabadili majina?. ni yatima wangapi walilelewa kwenye nyumba za malezi za makanisa wakifahamika kabisa ni yatima wa kiislamu?.
kinachonitatiza siku zote ni kuwa haya yanasemwa na watu juu ya watu. lakini hakuna aliye muhanga wa haya yanayosemwa akasimama hadharani na kusema kuwa either asingekuwa alipo kama asingeficha identity yake au asingekuwa alipo kama angeficha identity yake.

leo ukienda pale kwa nyumba ya yatima msimbazi utaona watoto na majina yao ambayo yanasema imani zao, lakini bado sisi ambao tunatakiwa kuusema ukweli tunapindisha kwa sababu ya either fikra duni au kwa nia ya kupotosha tu ukweli

we unazungumza mabo ya jana na leo?!!!hali haikua hivyo huko nyuma,muulize babu yako kama unae yupo hai,kighoma malima aliacha kutumia jina la Ally ili asome....
 
Kwenye orodha ya warithi wa marehemu alikumbukwa lakini?.Ukitaka kuwa maarufu pambana na mtu maarufu, oa au olewa na mtu maarufu, chezea timu maarufu, tafuta cheo maarufu, soma kozi maarufu, jenga urafiki na watu maarufu n.k. Umaarufu wa Nape uko mikononi mwa EL. Wakimvua gamba au kushindwa kumvua gamba hatutamsikia Nape tena.

Na huenda kuanzia sasa asiongelee tena kujivua gamba kwani muda tuliosubiri EL aseme aliyotakiwa kuyasema Monduli kwa waandishi wa habari kayasema NEC Dodoma.

Ujasiri wa Nape anaweza kuuonesha sasa kwa kumtuhumu pacha wa nnne na kufuta kauli ya Mapacha watatu na kupata msemo mpya wa Mapacha manne. Alichotakiwa kufanya Nape baada ya EL kutoa ya moyoni alitakiwa kujitoa CCM siku ile na kumshambulia pacha wa nne. Hakika angekuwa maaarufu ya hapa alipofikia.

Tunachosubiri sasa ni graph yake kuanza kushuka. Namtabiria akiita waandishi atakuwa anawakosa na hata wakienda atakuwa hapati ukurasa kwenye gazeti na hata akipata siku hiyo mauzo hakuna.

Angefanya unavyotaka angekuwa maarufu kama mrema sio?

 
Answer:
Mbona kama umeongea kinyume mkuu,hao wanaoitwa mafisadi si maadui zake huyu au mafisadi gani pengine unaowazungumzia???labda na wewe un a tafsiri yako kuhusu ufisadi na mafisadi!
CCM YA SASA NDO BABA WA HUO UFISADI.Wanachogombana kwa sasa ni nani ale zaidi.
 
Picha inaonyesha kuwa anamwagilia kaburi la baba yake, full stop! haisemi kama andio amekumbuka wala nini? we are not sure kama kila mwaka alikuwa anakwenda kumwagilia hilo kaburi. Again, there is no eveidence kwamba ilikuwa ni siku ya mazishi, kama ni kweli, alipata wapi maji na can huko makaburini? Na kingine, kama ni wakati wa mazishi, mbona hakuna watu wengine pembeni?

Kwa kifupi hii picha inaonyesha Nape akimwagilia kaburi (linaloaminika kuwa ni la baba yake, liko mbali na maneno hayasomeki) and nothing else!

Waislam kwenye mazishi yao huwa wakimaliza kufukia kaburi wanamwagia maji mzee,sasa hayo maji inawezekana yalibaki kwa mzee penza ndio nape akaomba birika nayeye akamwagie kwenye kaburi la babake mzazi.
 
sielewi ujasiri wa Nape unatoka wapi! Nape alianza kusikika wakati akijiandaa kugombea uenyekiti wa UVCCM alipopigia kelele ushiriki mbovu wa EL kwenye ujenzi wa ghorofa la umoja wa vijana.

Kila mwenye akili timamu alijua Nepi anatumika kunufaisha kundi fulani hasimu kwa EL ktk mradi huo wa jengo la vijana. Baadae akadakia singo ya Slaa ya mafisadi ndan ya Mume wa KAFU.


Jk alipokurupuka na dhana ya kusadikika ya kujivua gamba na yeye Nepi akakurupuka kuzunguka nayo lakini kwa kuhakikisha anamkata makali EL. Sasa ujasiri wake ni upi wakati anafanya shughuli zake kwa misingi ya chuki na kukomoana akinufaisha makundi flan ya wanaotaka urais?

Tuwe wakweli. kijana ni jasiri na anafaa kuwa kiongozi. hana dhambi ndiyo maana anasimama kweupee kusema anachoamini. big up nape.
 
Anamwongelea mwenye Richmond yaani yule aliyetajwa wiki iliyopita na waziri mkuu mstaafu

Hapana umejichanganya mzee,sio waziri mkuu mstaafu ni waziri mkuu aliyejiuzulu kutokana na Kashfa ya RICHMOND!Full stop.
 
Tuwe wakweli. kijana ni jasiri na anafaa kuwa kiongozi. hana dhambi ndiyo maana anasimama kweupee kusema anachoamini. big up nape.

Naona watu mmekazana Nape ni mtoto wa nje...sasa tatizo liko wapi hapo??Ana tofauti gani na Riz1??au mamilioni wengi tu kwenye familia zenu/zetu waliozaliwa nje???Suala la mtoto wa nje au wa mama mdogo ni irrelevant katika mustakabala wa maendeleo ya nchi...shame on you "great thinkers" kujadili very shallow issue...
 
Back
Top Bottom