KUMBUKUMBU 2019: Ofisi ya Makamu wa Rais imetunga Kanuni mpya za Usimamizi wa Taka Hatarishi

Papaa Muu

JF-Expert Member
Nov 6, 2018
243
292
Mataifa mengi ya Afrika yamegeuzwa kuwa madampo ya kutupia takataka hatarishi kutoka kwenye mataifa yaliyoendelea. Pia taka hizo huzalishwa humuhumu nchini.


Taka hizo, endapo hazitasimamiwa ipasavyo, zitaondoa uhai wa wanadamu, wanyama na viumbe hai vingine. Mfano wa taka hizo ni Oil chafu, magari, simu, petroli, na kemikali za aina mbalimbali.

Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira imeandaa kanuni mpya za Usimamizi wa Taka Hatarishi za mwaka 2019 kwa kuzingatia Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2009.

Kanuni hizi mpya zimeweka adhabu Kali zaidi ukilinganisha na zile za mwaka 2009 kwa makosa ya kutokua na kibali Cha kusimamia taka hatarishi nchini.

Adhabu hizo ni faini kuanzia Milioni tano hadi bilioni 10 au kifungo kisichozidi miaka 12 au vyote kwa pamoja.

Wataalamu wa mazingira duniani wamebariki kanuni hizo huku wakisema zitainusuru Tanzania kupata madhara yaliyotokea huko Ogoniland nchini Nigeria ambapo taka hizo zimesababisha maafa makubwa.
 
Back
Top Bottom