Kumbukizi; Shukrani kwa JF members wote

MKONGORO

JF-Expert Member
Jun 15, 2014
325
263
Wakuu ni takribani miaka 8 sasa imepita toka 2015 nilipo kimbilia kwenu ninyi ndugu zangu members wa JF kuomba msaada.

Nikikumbuka mliponitoa wakati mwingine huwa machozi yananitoka, Wakati huo nilikuwa nimepoteza mzazi wangu kwa ugonjwa wa figo, Sina kazi, Kodi ya nyumba imeisha, mwenye nyumba aniambia nihame, familia inataka chakula.

Nilichanganyikiwa kabisaa!! Ninyi wanafamilia wenzangu wa JF kutoka njema na ndani ya nchi kupitia simu western union, Money gram mlinichangia kiasi cha pesa kilichoniwezesha kumalizia na kuhamia kwenye kibanda changu nitaendelea kuwashukuru daima.

Kwa sasa namshukuru Mungu nilipata kibarua kingine na familia inapata riziki kama kawaida. Kusema kweli kukosa ninyi ndugu zangu mwaka ule ningepata aibu ya karne na familia ingeteseka.

Hakika mliweka alama ambayo haitafutika katika kumbukumbu za maisha yangu na familia kwa ujumla Asanteni.

=> Ninadaiwa kodi ya nyumba na sina kazi kwa sasa, msamaria mwema nisaidie
 

Attachments

  • Screenshot_20220605-091405.png
    Screenshot_20220605-091405.png
    60.5 KB · Views: 14
  • Screenshot_20220605-100744.png
    Screenshot_20220605-100744.png
    57.2 KB · Views: 14
Mkuu hongera kwa kukumbuka yote mema ni muda wa wewe kufanya jambo kwa wahitaji wengine
 
Back
Top Bottom