Usipite bila kufanya chochote kwa watu hawa

Genio the great

Senior Member
Aug 29, 2022
159
491
Habari za majukumu wakuu wa Jf Leo nimeona niongelee hili swala tunapoelekea mwishoni mwa mwaka Ili ikiwezekana mwaka unafuata kama hukuwa na utamaduni huo ikukumbushe kufanya na kama ulikuwa na utamaduni huo basi endeleza ulipoishia.

Kumekuwa na wimbi kubwa la wahitaji wa Namna tofauti katika jamii tulizo nazo, wapo wahitaji halisi lakini pia wapo matapeli wanaojificha kwenye mwamvuli wa wahitaji halisi

Wako ombaomba mtaani lakini pia wapo wafanya biashara ndogo ndogo za mitaji ya elf 5-10 kuendesha familia zao ,Kuna mahali unaweza pita ukakutana na Mzee au mama ana mtoto mgongoni halaf kabeba beseni la maembe anauza , yaani kiukweli hata kama Sina haja na embe moyo wangu Huwa unanisukuma kununua nikampe hata mtu ila tu yeye aweze kupata kitu.

Kimsingi hatupangiani Maisha nini Cha kufanya ila Kuna muda ubinadamu ni muhimu sana, wakati wewe unakula Milo mitatu Kuna mtu anakula katikati ya mchana na usiku Ili kufidia magap yote matatu.

Na Kwa ujumla swala la kutoa mm binafsi niwe muwazi ni muumini wa dini lakini kutoa Kwa wenye mahitaji mfano, yatima, wajane, wagonjwa, n.k nimeona majibu ya ulichokifanya yanakuja haraka sana kuliko hata aliyetoa pesa kwenye Nyumba za Ibada nasema hvyo kwasababu nimefanya yote na nimeona wapi kuna impacts ya haraka.

Sisemi kutoa kwenye nyumba za Ibada ni kosa no nieleweke vizuri nimezungumzia matokeo ya haraka lakini pia siku nikipata neema nitakuja kuleta uzi kwanini watu wengi wanatoa kwenye nyumba za Ibada na hakuna matokeo chanya kosa liko sehmu gani, kuna maeneo nitagusa Namna nzuri ya utoaji naamini utaanza kuona matokeo chanya hata huko maana ni swala la principles tu.

Kwanini nasema kutoa Kwa wahitaji Kuna impact ya haraka nilipokuja kufuatilia kwanini huku kuna impacts ya haraka nikapata na maandiko kutoka kwenye Biblia ya kunipa support juu ya Hilo

Mithali 19:17.
Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA; Naye atamlipa kwa tendo lake jema.

Yakobo 1:27.
Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.

Nakumbuka Kuna siku moja karibu na nyumbani kwangu Kuna Mzee mmoja anaishi nikipita tu hapo kwake inayofuata ni nyumba yangu, na anapoishi ni mazngira mabaya sana ni nyumba ameijenga Kwa majani kama vile vibanda vya mashambani waliowahi kulima au kupita kwenye mashamba wanaelewa vile vibanda yaan juu majani pembeni majani na anaishi peke yake.

Siku moja nilipokuwa narudi nyumbani nilipofika pale kwake moyoni mwangu nikasukumwa mpe pesa yoyote uliyonayo mfukoni itamsaidia, yule Mzee Kwa makadirio kiumri anaweza akawa kama 55+ na kazi pekee ambayo Huwa anaifanya namwona Kila nkipita ni kuchonga vitanda vya miti vile vya asili vya kamba.

Basi nikaingiza mkono mfukoni nikatoa noti ya sh elfu 2 nikamfuata nikamwambia babu chukua hii itakusaidia kununua mboga.

Sitosahau vile babu alishukuru alitamka maneno ya kunibariki ambayo naamini kama Kuna Baraka zangu zilikuwa zimezuwiwa pale zingefunguka bila kizuizi maana aliongea kwa hisia Kali sana ya kutoka ndani ya moyo kama anataka kulia. Mm nkaitikia amen nkaondoka.

Nilipofika nyumbani nimepunzika kama nusu saa gafla namuona mkewangu anakuja mbiombio kutoka sebulen ananionyesha msg ya CRDB bank Kuna pesa ameingiziwa alikuwa anadai kazini kwao muda mrefu sana na ni pesa nyingi tu. Aliponionyesha mm alarm moja Kwa moja ikapiga kichwani ni ule msaada niliotoa hizi ni sehemu ya fadhila naanza kupewa.

Sitaandika matukio mengi ila Nimekuwa nikiona mambo mengi yanafanyika Kwa namna tofauti kabisa pale ninapogusa mahitaji ya watu.

Nikaona nisibaki nalo hili tunapoumaliza huu mwaka niliseme kwako yawezekana Kuna mambo Yako mengi yamekwama ila kupitia kugusa mahitaji ya wengine basi na mahitaji Yako yataguswa pia na Mungu akubariki

Nawasilisha Kwa moyo wa unyenyekevu mkubwa kabisa

Uwe na tafakari njema tunapoikaribia 2024.
View attachment 2854683
09256ed7f5dfdd2b75227227c5589144.jpg
View attachment 2854684View attachment 2854685
 
mkuu pesa mke wako alikuwa anaidai?
Ndio alikuwa anadai kazini kwake ila hakukuwa na taraja la kulipwa na ishapita zaidi ya mwaka , kifupi ni kama alishaisahau na ndio maana hata ilipoingia hakuelewa imetoka wapi Kwa mara ya kwanza.

In short hakukuwa na tarehe maalumu ya kusema itaingia ni deni ambalo waliambiwa litalipwa ofisi ikija kukaa stable kifedha na ndio maana lilipotokea ndani ya siku na ndani ya lisaa la tukio nikajua Kuna nguvu ya msukumo imetumika,
 
blessed be the hand that giveth than the one that taketh
 
Unajidanganya sana. Wewe saidia tu watu wenye uhitaji kwa kadiri ya uwezo wako bila kuwaza hata hayo ma feedback. Usifikirie sana fadhila baada ya kutoa.
 
Saidia bila kutegemea kupata chochote , ukitoa umetoa na sio kujumlisha.
 
Back
Top Bottom