Kumbuka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbuka!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jan 5, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Kumbuka!  Usione vinaelea, vimeundwa![​IMG] Je, umawahi kujiuliza ni nini siri ya mahusiano yanayodumu kwa muda mrefu let say miaka nenda rudi na wahsika wakawa na furaha na kicheko bila unafiki?
  Tumeanza mwaka 2010 na tunahitaji kuwa na resolutions kwa kila idara ya maisha yetu na mahusiano iwe uchumba au ndoa ni muhimu sana kwani huwezi kukwepa mahusiano labda uwe.......

  Mwaka 2010 jitahidi kufanya yafuatayo naamini mahusiano yako yatakuwa imara na yenye afya

  Hakikisha unasifia zaidi kuliko kulaumu
  Ukiwa na rafiki zako hakikisha unaongea mambo 2 au 3 mazuri kuhusu mpenzi wako au mke wako au mume wako.
  Kumbuka kwamba kufanya vitu kila mtu kwa tofauti ni kitu cha kawaida kwani kuna njia nyingi sana za kumenya kiazi au kukunja nguo.

  Hakikisha mnakuwa na muda wa pamoja na mpenzi wako.
  Kama hujaoa au kuolewa hakikisha unaoana na mwanaume au mwanamke ambaye unapenda kumsikiliza na anavyoongea.
  Kumbuka ndoa wakati mwingine ni kitanda cha maua ya waridi na wakati mwingine ni ndoa ni kitanda cha miiba.

  Kumbuka zawadi nzuri sana kwa watoto wako ni kumpenda mama yao.
  Pia kumbuka kuhakikisha unajihusisha vizuri na kazi ndogondogo za nyumba kama ni mwanaume kama vile kufungua nguo, kusafisha nyumba nk.

  Ukiona kuna uwezekana wa kuzipiga kikwelikweli basi hakikisha mnapigana mkiwa uchi! Serious!
  Kubali, kutokukubaliana.
  Usitamke kabisa neon talaka
  Usiende kulala huku umekasirika labda iwe ni saa tisa usiku na umechoka huwezi kufanya chochote.


  Mawasiliano mazuri ni ufunguo wa ndoa na mahusiano yako.
  Usisahau kusema “Nakupenda”
  Uwe na kimbelembele cha kusema “Nimekosa nisamehe’
  Hakikisha ndugu (inlaws) wanakaa mbali na ndoa yako

  Usilinganisha ndoa yako au mahusiano yako na wengine kwani unachokiona nje haina maana kinaweza kupatikana ndani.

  Hakikisha si kitanda kilekile, milalo ileile, chumba kilekile, nyumba ileile, wakati uleule wa kufanya mapenzi na mke wako au mume wako kwani tofauti huleta maana.

  Mwisho!
  Uhusiano wako na Mungu ni muhimu sana katika mahusiano, Mungu ndiye mwenye upendo hivyo unavyozidi kuwa karibu na Mungu ndivyo unavyozidi kuwa na upendo na mtu unayejua kupenda.

  Mafanikio ya ndoa yoyote yanauhusiano mkubwa sana na uelewa kuhusu Yesu Kristo ni nani katika maisha yako.
  Usipuuze bila Yesu ni zerooo............................
   
Loading...