Wakati wa awamu ya tatu ya raisi Mkapa katika kipindi chake cha pili, waziri wa mawasiliano na uchukuzi alikua prof. Mark Mwandosya.
Kule mbeya kulianza kujengwa uwanja wa ndege wa kimataifa songwe. Uwanja huo ungeweza kukamilika miaka miwili baada ya Kiwete kiungia madarakani. lakini kwasababu zai za kisiasa kwamba Mark hakua kundi la mtandao wakati Kundi hilo linasaka urais, uwanja huo ulisimama kujengwa mpaka ukaota vichuguu kwenye njia ya kurukia na kutua ndege na hilo watu wa mbeya wanajua ni akina nani wamesababisha uwanja huo usikamilike mpaka leo. Lakini juzi wameenda kumpokea kwenye uwanja hu ohuo ambao EL hakutaka ukamilike.
Pili, nchi za SADEC zilikua zimeamua kuchenga chuo eneo la soweto mbeya kwa ajili ya kusomesha wanafunzi wanatoka ukanda huo, kwasababu za kuwanufaisha watu wa kasikazini, akina EL waliamua kuhamishia chuo hicho arusha na kusababisha SADEC kuachana na mpango huo.
Tatu mwaka 2007 wakati wa chaguzi za ndani za ccm, kundi hillo hilo la wanamtandao wakiongozwa na lowassa walitumia kila njia kutaka kumuondoa prof. Mark Mwandosya kwenye ujumbe wa halmashauli ya ccm kupitia mkoa wa mbeya kwa kumtumia Tom Mwang'onda, lakini kwa nguvu aliyonayo Mwandosya walishindwa. (nakumbuka ushabiki na kampeni zilizokuwepo wakati huo zilisababisha mzee kingunge alipigwe makofi pale mbeya kwa kushiriki kuwashawishi wanaccm mbeya wamchague Tom badala ya Mwandosya.)
Sasa najiuliza kweli watu wa mbeya wanaweza kuwa wamesahau yote hayo kirahisi namna hii?. hili la uchaguzi wa ccm sio issue sana. lakini kucheleweshewa uwanja na kunyimwa chuo na akina lowassa je?