Kumbe watanzania watu wa hovyo hivi!

Kumbe watanzania watu wa hovyo hivi!

Mh! Nchi imehuzunika, watu wengi wanaomboleza, watu wanalilia kura zao. Ole wao waliohusika....
 
Watanzania ni maskini wa akili mpaka mawazo. Na huo ndio mtaji wa ccm
 
Ki ukweli, watanzania kuna kitu tumelishwa au kunyimwa tukiwa wadogo, kinachosababisha tushindwe kuzitumia bongo zetu vizuri kuchanganua mambo ya msingi kabisa. Yaani wananchi wengi hawana uzalendo kabisa na wako tayari kurubunika kwa kushabikia vitu vidogo vidogo na vya kupita. Na hii inatokana hasa na kukosa elimu ya uraia, historia na hata kujitambua miongoni mwa watanzania wengi.

La kama si hivyo, basi tukiri kuwa CCM wamefuzu na kubobea sana katika suala zima la propaganda.

Cha kufanya, upinzani usikate tamaa bali na wao waanzie huko walikotoka CCM huku wakipitia kwa kutoa elimu kwa raia waijue siasa na umuhimu wake kwa ustawi wa jamii. Wananchi waelewe umuhimu wa vyama vya upinzani na pia wajue kutofautisha siasa safi na chafu. Upinzani ujikite kueneza vyama kwenye ngazi za chini kwanza kwa gharama yeyote ile, vianzishwe vyuo vya siasa na ikibidi wateuliwe baadhi ya wanachama kwenda kujifunza propaganda kwa wenzetu waliofanikiwa sana kwenye hilo.
 
Jamaa muongo sana, yaani huku mtaani watu wengi ni kama wako kwenye msiba, na wengi wamekata tamaa kabisa ya kupiga kura tena, maishani mwao!! Wanasema bila kupatikana tume huru ya uchaguzi, bora pasiwe na uchaguzi tu, iwe kama china wawe wanapokezana tu wao kuliko kusumbua watu.
Khaa!! wewe vipi bana? mie nazungumzia mtaani kwetu siyo huko kwenu :crazy:
 
Nimeshangaa sana,
Zaidi ya nusu ya vijana wa bodaboda waliokuwa wakipeperusha bendera ya CDM huku wakirandaranda mitaani leo wanafanya hivyohivyo huku wakiwa na bendera ya ccm.
Kina dada wote kwenye hii bar ya jirani waliokuwa wanashinda na vilemba na mitandio yenye rangi ya cdm hata wakati wajua kali, leo ndiyo hawa wanakata mauno hapa wakiwa na nguo zenye rangi za ccm!!
Huyu mangi jirani yangu ambaye kila ukienda dukani kwake haachi kukukumbusha juu ya mabadiliko leo anasema kidogo tupotee njia!!!
Watu wa hovyo sana hawa!!
Unaujua msemo wa "KULA CHADEMA KULALA CCM" hiyo ndio siasa welcome 2 the real world
 
Back
Top Bottom