Kumbe wanaume ndio wapo hivi!?

Pole. Ndio, people should still have close relationships with their parents hata baada ya kuoa/kuolewa ila mbona kama mume wako amepitiliza... Tena kwa anavyofanya inaonyesha kabisa he doesnt care about your feelings
 
Ushauli wangu ili uweze kwenda sambamba na mmeo kwa vile ana mapenzi makubwa na mama ake basi nawe huna sababu ya kuludi nyuma kuonyesha upendo uliopitiliza kwa mama mkwe tena kipindi wanaongea we unapaswa kuwa karibu zaidi nae namaanisha uwe ubavuni mwake hakika hutojuta na ndoa yako, lakini kama utakuwa unamwona mmeo wapo karibu na mama ake we unanuna utakonda sana.
 
KUWA MPOLE MKUU,HIZO NI CHANGAMOTO TU ZA NDOA,CHA MUHIMU JARIBU KUPOTEZEA HIYO HALI NA KUISHI BILA STRESS.PUUZIA VITU VIDOGO VIDOGO UTAISHI KWA AMANI.
 
Seriously??? Dume 30+ unaenda na mama yako sokoni???

Mnakaa kwenye nyumba yenu na mumeo au ni nyumba ya huyo mama?

Kama si yenu ni bora muhame/mjenge muende mkaishi mbali na hapo ili muwe mbali na huyo mama.
 
habari za maisha wana jf! naombeni kushare na nyie kuhusu hichi kitu kinachonikabili kwan naamini naweza kuelewa maisha jinsi yalivyo kwa kuwa kila siku tunajifunza.
Mimi nmeolewa miaka 6 iliyopita n am 31 now! mume wangu ndio kila kitu kwangu nampenda sana namhurumia namthamini pia...vile sina wazazi na nmezaliwa peke angu bas mume wangu nmemchukulia km ndo kaka, baba, mama, dada na kila kitu!
yaan jinsi nilivyo yaan simfichagi hata kitu ktk maisha yangu...furaha huzuni kila kitu anajua....napenda sana kupiga nae stori umbea n.k yaan tukianza kusengenya mtu weeeeee! nmezoea kwake kwan sinaga hata rafiki wa karibu sina mazoea na watu saaaanaaa..
Lakiniiii kitu ambacho kinaniumizaa bwana ni life style yy na bi mkubwa wake...mama ana tabu huyo cjapata ona! nmpenda sana lkn hapendeki! yaan sielewi ana tatizo gani....anamwekea mtoto ake biz sana kiasi kwamba ile furaha yangu nahisi inatoweka! na mtoto nae (mume) yy na mamake humuelezi kitu! anatupangia tuishi vile anavyotaka yy...sisi tukiplan kitu chetu yy anaenda anaharibu...hafla unamuona mtu hakupatilizi tena!
ni mda mrefu hili tatizo nmelifanyia uchunguzi nmegundua ni mama ndie anaharibu!
ni stori ndefu sana cpendi kuwachosha lkn sasaiv mume wangu sina stori nae....anaongea na mamake na sim mda wote! hata sokoni wanaenda wote napangiwa budget na ma mkwe tena anambia kabisaa nyanya hizo mwezi mzima!
kwanini imekuwa hivi ikiwa me ni mke nna kazi nna biashara najua kutafuta na mume wangu kipato chake kidogo sana! nikijaribu kumuuliza anakasirika ndo ctoongeleshwa cku tatu mtu kanuna!
mara mama mtu amfate mwanae asbh cjui wanaenda wapi!!? siambiwi wala siulizi! utakuta tumekaa watatu hafla wanaanza kunong'onezana...jamaniiii!!!??
baadhi ya watu wameshaiona hii picha naskiaga ckiaga tu wanasema mhhhh yule kaka anamsikiliza sana mamake naskia hata rafiki zake wanamwambia awe na msimamo na maamuzi yake...lakn wapiiiii!!!! jamani sina furaha...
hivi ndio wanaume wote walivyo au ni huyu wangu tuu?? naombeni ushauri kwani naumia sana hlafu nahisi kupoteza mapenzi na huyu mama...nmevumilia mengi sana kwake!
Mmh hapa unaweza uka-reply kitu ukaonekana wa ovyo!

Yawezekana kuna mahaba kati yao, si bure.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom