Kumbe wanaume nao huingia katika Hedhi!

Kumbe wanaume nao huingia katika Hedhi!

34b27c739df03ba3245ce2eab4869a38.jpg

BERKSHIRE, UINGEREZA

KIJANA mmoja wa kiume anayesoma kwenye chuo Kikuu cha Reading kilichopo kwenye mji wa Berkshire huko uingereza, ameushangaza ulimwengu baada ya kudai kuwa hata yeye hupatwa na hedhi anayoiita ‘hedhi ya kiume’.

Mwanafunzi huyo anayeitwa George Fellowes mwenye miaka 22, anasema mara nyingi rafiki yake wa karibu, Amber May Ellis anapokuwa kwenye siku zake na yeye hupata uchungu wa hedhi kila mwezi.

Uchungu huo anasema huwa mkali hadi kulazimika kuchukua likizo ya kuwa mgonjwa, kwenye mahojiano na Newsbeat, George amesema kuwa, “Nadhani ni jambo la kifikra kwa sababu sisi ni marafiki wa karibu sana na tuna hisia sawa,” amesema.

Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita anasema kuwa amekuwa akipata uchungu wa hedhi na ishara hizo ni sawa na zile zinazowapata wanawake.

Alisema huwa anapata uchungu chini ya tumbo lake na katika kinena na kwamba huwa anajihisi vibaya na anakuwa mwenye hasira kwa marafiki zake na hisia za mhemuka huwa juu.

“Huwa sipendi kulia wakati huo lakini huwa na hasira nyingi, kuna kitu kimoja kinacho muathiri George hata hivyo sidhani kwamba wanaume wanaweza kupata hedhi bila kutokwa na damu. Wakati unapokuwa na rafiki wa karibu na mtu nadhani homoni zenu hufanana”.

Fellowes anaelezea kwamba wakati alipoanza kupata uchungu miaka mitatu iliyopita alitaka ushauri wa daktari wake. Lakini hakukuwa na maelezo hivyo basi alipewa dawa za kumaliza maumivu.
 
Huku ni kuwakosea wanaume kwa makusudi hili gazeti lituombe radhi haraka sana
 
Dah....nilivyosoma heading tu, swali la kwanza lilikuwa 'damu itatokea wapi'?......kumbe ni emotions zaidi.
hahahahahhahaha kwani kwa wanawake inatokea wapi??

jst kidding
 
Elli nimesoma nikaishiwa cha kusema maana duh ngoja nikajifanyie research maana ahhh ngumu kumesa
Mr Rocky habari za Magu,hebu mshauri huyu mleta MADA aache kabisa kutudhalilisha wanaume,na kama kuna mapepo yamemuingia basi kwa jina la YESU yashindwe kabisa,yaani sisi wanaume na BALLS zetu tuingie hedhi? ama kweli hizi ni zama za mwisho.Hedhi hilo neno ni zito sana,yatakuja tokea MABWABWA humu yatamuunga mkono na kukiri ati huwa yanapata hedhi kwenye TIGO katika siku kadhaa za mwezi.EEEEEE MOLA MUUMBA UTUEPUSHA NA MAJANGA.
 
1462999998163.jpg

Kubishana na gazeti nacho ni kipaji
 
34b27c739df03ba3245ce2eab4869a38.jpg

BERKSHIRE, UINGEREZA

KIJANA mmoja wa kiume anayesoma kwenye chuo Kikuu cha Reading kilichopo kwenye mji wa Berkshire huko uingereza, ameushangaza ulimwengu baada ya kudai kuwa hata yeye hupatwa na hedhi anayoiita ‘hedhi ya kiume’.

Mwanafunzi huyo anayeitwa George Fellowes mwenye miaka 22, anasema mara nyingi rafiki yake wa karibu, Amber May Ellis anapokuwa kwenye siku zake na yeye hupata uchungu wa hedhi kila mwezi.

Uchungu huo anasema huwa mkali hadi kulazimika kuchukua likizo ya kuwa mgonjwa, kwenye mahojiano na Newsbeat, George amesema kuwa, “Nadhani ni jambo la kifikra kwa sababu sisi ni marafiki wa karibu sana na tuna hisia sawa,” amesema.

Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita anasema kuwa amekuwa akipata uchungu wa hedhi na ishara hizo ni sawa na zile zinazowapata wanawake.

Alisema huwa anapata uchungu chini ya tumbo lake na katika kinena na kwamba huwa anajihisi vibaya na anakuwa mwenye hasira kwa marafiki zake na hisia za mhemuka huwa juu.

“Huwa sipendi kulia wakati huo lakini huwa na hasira nyingi, kuna kitu kimoja kinacho muathiri George hata hivyo sidhani kwamba wanaume wanaweza kupata hedhi bila kutokwa na damu. Wakati unapokuwa na rafiki wa karibu na mtu nadhani homoni zenu hufanana”.

Fellowes anaelezea kwamba wakati alipoanza kupata uchungu miaka mitatu iliyopita alitaka ushauri wa daktari wake. Lakini hakukuwa na maelezo hivyo basi alipewa dawa za kumaliza maumivu.
Tatizo watu wanapaniki
 
Back
Top Bottom