Kumbe wanaume nao huingia katika Hedhi!

Nilikuwa nampango kuanzisha uzi kule jf doctors...kuhusu hedhi kwa wanaume.. Inshot iko hivi hedhi kwa wanaume ipo na inatokea baada ya siku 28,nakabla ya kuingia huwa ana hasira zisizo na sababu yoyote zaidi goggle(do man have period?) mimi nimeshindwa kuweka link..



SALUTE MKUU, achana na hawa marijari feki wasiojua haya

cc Power G HARUFU Kongosho Mashaxizo masai dada na wengine msio na .......
 
Last edited by a moderator:
Nilikuwa nampango kuanzisha uzi kule jf doctors...kuhusu hedhi kwa wanaume.. Inshot iko hivi hedhi kwa wanaume ipo na inatokea baada ya siku 28,nakabla ya kuingia huwa ana hasira zisizo na sababu yoyote zaidi goggle(do man have period?) mimi nimeshindwa kuweka link..

Ndo leo nasikia hii
 
Mbona haingii akilini, na
Mbona mwanamme siku zote ana uwezo wa kupata mtoto kama anaingia kwenye heidhi
 
mara nyingi nimekua nikiamini kwamba yale tunayoyafahamu kuhusu maisha ni machache sana ukilinganisha na yale tusioyafahamu. Kiasi cha miezi kadhaa iliyopita nilisoma utafiti fulani kuhusu hedhi. Awali nilipousoma niliona ni hadithi tupu. Lakini nilipoona ni vyema kuujaribu kwa kutenda miezi minne baadae nilishangaa. Hata wewe najua utashangaa utakaposoma makala haya. Lakini ombi langu kwako ni kukutaka ujaribu kufanya mazoezi ili uthibitishe ukweli huo.

Miaka ya hivi karibuni imegundulika kwamba hata wanaume hupata hedhi-ingawa wanaume hawana alama za nje za kuwaonesha kwamba wako kwenye hedhi, kama walivyo wanawake ambao hutoka damu siku zao za hedhi zinapofika na kukamilika.

Kwa karne na karne hakuna mtu aliyekuwa akifikiria kwamba wanaume wangeweza kuwa wanapata nao hedhi kama wanawake. Kama mwanaume akiamua kuweka kumbukumbu zake kwenye dayari na kujiangalia kila siku hali yake inavyobadilikana kuwa ya kusikitika, ya kawaida, furaha na hasira……akiifuatilia hali yake namna hiyo kwa siku zote 28 za mwezi, halafu na mwezi unaofuata, akafanya hivyo hivyo, halafu mwezi wa tatu nao akatenda hivyo, na halafu ailinganishe miezi hiyo mitatu atashangaa.

Kuna siku tatu, nne au tano ambazo zitafanana katika dayari zote tatu, lini ana hasira ana masikitiko, ni mharibifu, na tabia nyingine kama hizo. Hivyo ndivyo vipindi vya hedhi kwa wanaume kama ilivyo kwa wanawake. Zoezi hili anaweza kufanya mwanaume yeyote, akishindwa kupata matokeo anaweza kuwasiliana na mimi na kuuliza ni kwa nini nimeandika uongo.

Ni jambo ambalo lipo na limeshafanyiwa tafiti mbalimbali, hata mimi binafsi nimefanya zoezi hilo kwa miezi minne na limetoa majibu kama hayo. Kwa kawaida mwanaume hana dalili za kimwili za kutoka damu kama mwanamke – ndio maana, karne na karne hakuna mtu aliyejali – lakini ni jambo la uhakika kwamba wanaume wanapata hedhi.

Dalili za mwanaume aliye kwenye hedhi ziko akilini zaidi na sababu ziko wazi: Mwanamke asili yake ni kimwili zaidi, kihisia zaidi, na mwanaume ana asili ya ubongo zaidi. Lakini mwanaume anapata usumbufu ule ule anaopata mwanamke anapokuwa kwenye hedhi. Tofauti ni moja tu, kwamba mwanaume hatoki damu. Lakini kila mwezi, baada ya siku 28, hali fulani ya kiakili na kihisia itakuwa inajirudia.

Na kama umejaribu kujichunguza kwa mwaka mzima, utashangaa kwamba, ulikuwa na hasira mgomvi, mwenye huzuni na vingine vya aina hiyo, si hivihivi tu bali ni kwa sababu ulikuwa kwenye hedhi. Kama ukishafanya zoezi nililokwambia la dayari, jiulize, kama ulipokuwa kwenye hali hizo ulikuwa umekerwa na yeyote au chochote. Utagundua kwamba hukuwa umekerwa bali ulikuwa unasumbuliwa na hedhi yako.

Mwanaume na mwanamke wameumbwa kwa ‘matofali' yaleyale, kwa maumbile yaleyale na baiolojia ileile. Tofauti yao ni kwamba mwanaume ni chanya na mwanamke ni hasi kama tungekuwa tunazungumzia umeme. Huwezi kupata umeme kwa kuwa na chanya mbili; wala ukitumia hasi mbili bali ukichanganya chanya na hisi. Hivyo, kama mwanamke anapata hedhi kama hatua muhimu kuelekea mwito wa kimaumbile, haiwezekani mwanaume asipitie hatua hiyo, ingawa kwa uchanya wake.

Kupata hedhi kwa mwanamke inaeleweka kwamba, ni kutokana na wito wa kimwili. Maana yake ni kwamba, alikuwa amefikia hatua ambapo kimaumbile alitakiwa kujamiiana ili apate ujauzito. Je, kama hakuna mabadiliko kwa mwanaume, itawezekana vipi mwanaume kujamiiana na mkewe ambaye yuko kwenye hitaji hili la kimaumbile?

Ina maana basi kwamba mwanaume naye ni lazima kila mwezi awe na mabadiliko ambayo yatamfanya aingie mahali ambapo atavutana na mwanamke kimapenzi. Hili ni suala la maumbile ili kufanya kuzaliana kuwepo. Utajuaje kuwa mwanaume ameingia kwenye hali hiyo? Ndiyo pale ambapo wataalamu wamegundua hizo siku nne au tano za mabadiliko ya kiakili kwa mwanaume!

kweli kabisa utafiti huo umefanywa...na tahadhali ikatolewa kwa wanawake kuzitambua siku za mwanaume wake na kuto mchokoza kwenye siku hizo
 
kabla huja sema mwongo umefanya utafiti kindly goggle kwanza then rudi sema

Sasa hilo linatofauti gani na kipindi ambacho mnyama huingia kwenye heat.? Na hatuiti yuko mwezini.Hata mwanamke kuna kipindi ambacho joto huwa hasira kuliko muda mwingine.mostly ni around siku ya 11-17..hivi.naturally mungu katuumba tushirikiane na kuongezana ukiangalia siku hizi ambazo mwanamke huwa na joto kali ni kipi ambacho huwa yuko kwenye hatari.waliochunguza wamesema na akijitokeza mmoja wa jf kuthibitisha hali yake katika siku hizo na siku za kawaida itakuwa vyema.

Kwa maana ya maelezeno yenu kuwa kupanda hamu ni kuingia mwezini,wakike huingia mara mbili...
 
huo utafiti wako mkuu hahahaha...mbona mimi huwa nahasira mwanzo mwisho nikiudhiwa tu kidogo naweza kumtoa mtu meno hivyo basi inamaanisha cycle yangu ya hedhi inajirudia mara kwa mara c ndio maana yake?alafu pili inamaana mwanamme akiwa kwenye hedhi inakua ngumu kumpa mwanamke mimba c ndivyo unavyomaanisha?NAWASIWASI WW UNAJINSIA MBILI alafu unashindwa kujielewa usidanganye watu mkuu
 
1.Ni uongo kama uongo mwingine... kwanza unajua maana ya hedhi??????? Hedhi sio PSYCHOLOGICAL ISSUE bali NI BIOLOGICAL
2. Haya ni maoni tu ya mchambuzi fulani kama wanavyofanya kwenye uchambuzi wa siasa.....

3. Hoja haina mashiko,, HATAAAA

Mara nyingi nimekua nikiamini kwamba yale tunayoyafahamu kuhusu maisha ni ...............
 
Back
Top Bottom