Kumbe wale wanaotaka order ya kiti moto kilo 1.5 na ugali huwa wanapanua utumbo tu

Huyu Mzee mwaka 1550 alijiona anachoka sana, Aliangalia chakula anachokula na kukipunguza kufikia 350g na 414 mls za wine kwa siku.

Kwa hesabu za haraka haraka alikula yai moja asubuhi kama kifungua kinywa.

Kipande cha nyama, kuku au samaki saa kumi jioni kikiwa na kiazi na mboga. Ukubwa wa kopo la Coca Cola aliweka wine. Maji ni muhimu hapa kati kati.

Tunakula vyakula vingi tusivyo vihitaji. Wakati wa WWII, wanajeshi wa Magharibi waliotekwa Japan walilishwa kibakuli cha wali na kipande cha nyama kila baada ya masaa 24. Wengi waliishi mpaka kurudi makwao wakiwa wamekonda sana.

Iliwachukua zaidi ya mwezi kuzoea milo mitatu kwa siku.
duh!!!! watu wanajua kuhudumia matumbo yao bhana lah!!!! yani kilo 1.5 ya kitimoto na ugali?

sasa wa hivo akienda chooni sianakunya ndoo nzima ya mavi?.
 
Maisha yenyewe yamejaa tozo, Kiukweli mi nashindilia,Nikiwa kwangu nikipika wali Ni kilo na nusu,Wala usishangae nikikwambia hua sushibi.
Acha nile duniani maana mbinguni havita kuwepo
 
Unaacha kula unavyotaka......unapata ajali Isevya unakufa. Unagongwa na boda boda unakufa, magaidi wanalipua sehemu nawe umo unakufa.

Life's too short. Tule tu.
 
Yule dokta Isack Ndodi, alikua anatufundisha ulaji ni msabato yule nilikutana nae sehemu anakamua coca baridi na pilau nyama na ana bonge la kitambi sasa wakati alikua anasema kitambi hakifai kabisa.
 
Maisha yenyewe yamejaa tozo, Kiukweli mi nashindilia,Nikiwa kwangu nikipika wali Ni kilo na nusu,Wala usishangae nikikwambia hua sushibi.
Acha nile duniani maana mbinguni havita kuwepo
😂😂 mkuu kilo na nusu unamaliza kwa siku moja?
 
Kuna mama mzungu ali muasili mtoto wa Kitanzania, ilimchukua muda mtoto kuzoea kiasi cha chakula kwenye sahani yake.

Alimfahamisha sababu ya kila walichofanya. Alimwambia nyama ni chanzo cha kuongeza damu mwilini lakini si vizuri kula nyama kila siku.

Nyama ilikua ni Jumapili na J5 lunch na jioni kipande cha mkate, salad na mayai mawili ya kuchemsha.
Mkuu kama hutajali unaweza kutupa orodha ya mbadala Wa hivi vyakula vyetu vya kushiba?

Kwa Mfano Jumatatu Nile Nini na Nini, Jumanne halikadhalika mpaka wiki iishe?
 
Maisha yenyewe yamejaa tozo, Kiukweli mi nashindilia,Nikiwa kwangu nikipika wali Ni kilo na nusu,Wala usishangae nikikwambia hua sushibi.
Acha nile duniani maana mbinguni havita kuwepo
Jirani yangu ananunua kilo tano za mchele kila mwisho wa mwezi na yuko single. Nilimwambia kilo tano kwangu zinakata miezi 4-6.
 
Mkuu kama hutajali unaweza kutupa orodha ya mbadala Wa hivi vyakula vyetu vya kushiba?

Kwa Mfano Jumatatu Nile Nini na Nini, Jumanne halikadhalika mpaka wiki iishe?
Kipande cha mhogo wa kuchemsha, hoho mbichi na nyanya na changu wa kukaanga.

Vijiko vinne vya wali, bilinganya na yai la kuchemsha.

Wali, maharage mchicha

Ndizi mbichi nyama hoho na carrots.
 
Nilikuwa nafanya mazoezi yule trainer akawa anasema usiku huruhusiwi kula pilau,Nilikuwa namcheka sana moyoni.
 
Back
Top Bottom